Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Mengi yanasemwa kuhusiana na Clouds Media na uanzishwaji wa Wasafi Media. Mada yangu haitajikita huko, nimeutoa huo kama mfano tu, tuchukulie tu ule kama mfano wa jambo ambalo lipo sana tu katika mifumo yetu ya biashara.
Mada yangu inaongelea pale watu wawili au zaidi wanapoingia makubaliano ya kuanzisha biashara ya pamoja, partnership au limited company, lakini baada ya muda, kwa sababu moja ama nyingine, mmoja au baadhi wanawazunguka wenzao na kwenda kuanzisha biashara ya aina hiyo hiyo au inayofanana na hiyo bila kuwashirikisha (m)wenzao.
Katika nchi zilizoendelea, huwa partners au shareholders wanawekeana kitu kinachoitwa exclusive agreement. Yaani partner kwenye huo mkataba, haruhusiwi kwenda kuanzisha au kujiunga kama partner katika biashara yoyote ya aina hiyo au yoyote ile inayoleta ushindani wa moja kwa moja na biashara wanayoanzisha. Nadhani hata pale partner/shareholder anapojiondoa katika makubaliano hayo, bado anakuwa anafungwa na vifungu hivyo kwa miaka fulani.
Kipengele hiki kinaondoa udanganyifu na uwezekano wa partners kuzungukana.
Je, kwa sheria zetu za mikataba, kipengele kama hiki kinawezekana na kinatambulika?