Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,592
- 29,721
Mimi ni mwana CCM hai.
Kitendo cha watendaji/ wasimamizi wasaidizi kuwaengua wagombea zaidi ya asilimia 90 wa serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji ni wazi kimeibua publicy sympathy dhidi ya wapinzani nchini.
Minong'ono iliyopo mitaani ambapo hata wanaCCM wengi wanaguswa na hili hivyo linaweza kusababisha kura za hasira kuiadhibu CCM endapo uchaguzi utafanyika baada ya maridhiano kati ya serikali na vyama vya siasa.
Mchakato wa uteuzi wa wagombea kupitia CCM uligubikwa na sintofahamu nyingi na hata kupelekea wagombea wengi wasiokubalika na wananchi kuteuliwa huku ubabe wa kuhakikisha ushindi ukifanyika.
Watendaji ama wasimamizi wa uchaguzi walipofanya maamuzi hayo, waliamini kuwa wanakisaidia Chama Cha Mapinduzi lakini uhalisia ni kuwa wamemsaidia chura kwa kumpiga teke.
Vyama vikubwa vya upinzani CHADEMA, ACT, CHAUMMA, NCCR MAAGEUZI vimejiengua kushiriki uchaguzi wa Novemba 24. Lakini Waziri mwenye dhamana ameagiza walioenguliwa wote warejeshwe kwenye orodha ya wagombea hivyo kuongezeka mkanganyiko zaidi.
Upigaji kura ni sehemu ndogo ya demokrasia ambapo maeneo mengine ni namna vyama na wagombea wanashiriki ama kushirikishwa kwenye michakato kwa njia za wazi na haki. Lakini kinachofanyika ni maamuzi yasiyoshirikisha pande zote kuu za uchaguzi. Ni maamuzi ama maelekezo ya upande mmoja pekee.
Ushauri.
Mosi.
Tamisemi kwa kushirikiana na wizara ya Katiba na sheria wakutane na vyama vyote vya siasa kuweza kujadili mustakabali wa hili lililotokea kwa lengo la kutafuta suluhisho lake.
Pili.
Uchaguzi usitishwe kwanza ili kutoa nafasi kwa majadiliano na maafikiano ya vyama shiriki kisha tarehe itokane na maafikiano hato
Tatu.
Chama Cha Mapinduzi kitumie muda huo kushughulika na makandokando ya uchaguzi wa uteuzi kwa sababu upangaji ssfu za wagombea ni kansa inayokitafuna chama kwa muda mrefu.
Mwisho
Upinzani unapata nguvu sana sasa kuliko kipindi chochote kutokana na haya yanayotokea na haiyumkiniki inawezekana wapigakura wakakiadhibu chama tawala endapo hakutakuwa na juhudi za makusudi kirekebisha kasoro zilizojitokeza.