cacico
JF-Expert Member
- Mar 27, 2012
- 8,362
- 7,797
Fixed Point, yaani bila kufanya hivyo kwa wiki tu ni balaa haswa kama unakaa mbali, especialy ukiwa na watoto, yaani lazma kupiga simu ikifika jioni, dada watoto wamevaa masweta?, chakula cha baba kwenye ma-hotpot haraka, mtoto mkubwa apewe dawa za jioni! chumba cha twins kipulizwe dawa, hapohapo utanisikia dada kesho nje kulimiwe watoto wakilala mchana nikirudi nisikute majani, na mabuibui yatolewe! yaani ofisini kwetu huwa wanacheka nikisafiri nao! hata kama ni wapi! mwenzio nishawahi kuwa mkoa kwa wiki 3, na bado nyumba iliwekwa tiles nikiwa hukohuko, yaani naongea na muuza tiles dukani apeleke hm, malipo kwa m-pesa! naongea na fundi akaweke hizo tiles, malipo kwa m-pesa, na dada naye awafungie watoto rum kwangu ili wasipate vumbi la cement! mpaka nyumba iliisha! so my dear you are not alone hata kidogo! am one of them!Wanachit-chat nawasalimu.
kuna hili jambo huwa linanitokea sana.
Utakuta nimesafiri, sipo nyumbani kwa siku, wiki, miezi kadhaa, lakini huwa nina tabia ya kuendesha maisha ya nyumbani kana kwamba sijaacha mtu. kila siku lazima nipige simu kuulizia/kutoa maelekezo (mmepika nini?, watoto wamekula?, jioni mtawapa nini?, kesho toa net uzifue......). sasa najiuliza hii ina maana gani? ni mimi tu au hata wamama wenzangu mnafanya hivi?
wababa wanalipokeaje? wanashukuru kuwa tunawasaidia kuendesha nyumba hata kama hatupo nyumbani au wanaona hatuwaamini?
Last edited by a moderator: