Kuendesha nyumba kwa remote control

Fixed Point

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
11,304
12,744
Wanachit-chat nawasalimu.
kuna hili jambo huwa linanitokea sana.
Utakuta nimesafiri, sipo nyumbani kwa siku, wiki, miezi kadhaa, lakini huwa nina tabia ya kuendesha maisha ya nyumbani kana kwamba sijaacha mtu. kila siku lazima nipige simu kuulizia/kutoa maelekezo (mmepika nini?, watoto wamekula?, jioni mtawapa nini?, kesho toa net uzifue......). sasa najiuliza hii ina maana gani? ni mimi tu au hata wamama wenzangu mnafanya hivi?
wababa wanalipokeaje? wanashukuru kuwa tunawasaidia kuendesha nyumba hata kama hatupo nyumbani au wanaona hatuwaamini?
 
Mie nawaongoza kwa kiasi.

Ila lazima nipige asubuhi na jioni
Na lazima nikumbushe usafi as if naondoka na mifagio

Ila lazima nikumbushe watoto walale mapema ili wasisumbue kuamka asubuhi kwenda shule

Kuhusu wamepika nini huwa siulizi, sijui kwa nini.
 
Asante sana Kongosho, kumbe sipo peke yangu.
yaani hapo kwenye post nimeandika kwa kifupi tu, maana ningeanza kuelezea watu wangechoka kusoma. ni kama natoa ratiba ya kila kitu cha nyumbani.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Hii ni dalili ya kuwa unajali sana nyumba yako, hasa ikiwa una watoto. Pia inaonesha nyumbani unaye msaidizi. Ikiwa anatekeleza majukumu yake na unaridhika, hupati malalamiko toka kwa watoto na mume wako/mwenzako, sioni kama kuna tatizo kwa upande mmoja. Kwa upande wa pili, tatizo linaweza kuwepo kwa kwa huyo unayemkabidhi majukumu - Ni dada wa kukusaida kazi tu au ni jamaa yako? Ikiwa ni dada wa kukusaidia kazi, je, pia "Anamtunza" baba vizuri?
 
Asante MAMMAMIA. hayo ya kumtunza baba vizuri sitaki kuyajua. Nadhani kiuhalisia, ninaposafiri nyumba huwa namwachia baba, dada wa kazi atabaki kuwa msaidizi tu. sasa nilikuwa nawaza labda akina baba watatuambia, wanadhani tunapofanya hivi ni kwamba hatuamini kama wanaweza kuendesha nyumba kama sisi?
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Asante MAMMAMIA. hayo ya kumtunza baba vizuri sitaki kuyajua. Nadhani kiuhalisia, ninaposafiri nyumba huwa namwachia baba, dada wa kazi atabaki kuwa msaidizi tu. sasa nilikuwa nawaza labda akina baba watatuambia, wanadhani tunapofanya hivi ni kwamba hatuamini kama wanaweza kuendesha nyumba kama sisi?
In red unafanya vizuri, ukichunguza ni sawa na kutafuta na atafutaye hupata, hata ikiwa halipo atalibuni. Kuhusu kuachiwa majukumu siwezi kusema mengi kwani nimepata fursa chache, lakini ninapoachiwa huwa ninapokea maagizo kwa kila jambo na silalamiki kwa kuelekezwa au kukumbushwa. Pengine katika 10, japo moja atakuwa amefanya vyema kunikumbusha.

Nahisi wamama wengi wako kama wewe - wanatumia remort ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.
 
Kumbe tuko wengi eeehhhh........

Mie naona yangu ni mengi kuliko yako maana huwa nauliza
watoto anekula chakula chote ulichomuwekea, kashiba, kanywa
maji, kaoga, mpeleke akalale..............Na mengine meeengii

@
Kongosho sio kudeligate hatuwezi nafikiri unajua wasichana
wetu usipowasukuma aahhh mtoto atalala bila kula na akimuamsha
mara moja mbili haamki yeye anampeleka kitandani kulala hajali kivile......
 
safi sana kama haiwakeri, maana mimi nilidhani sijui anajisikiaje? ni kama naona yeye hawezi kufanya ninavyotaka mimi!
 
Dena Amsi kumbe haya mambo yapo kila nyumba! mara nyingi watoto afya zina-shake sana mama akisafiri, wadada wengi hawajali milo ya watoto, na ukizingatia watoto wetu wa siku hizi kula mpaka umuimbie, nani atafanya kazi hiyo mara 5 kwa siku!
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
safi sana kama haiwakeri, maana mimi nilidhani sijui anajisikiaje? ni kama naona yeye hawezi kufanya ninavyotaka mimi!
Cha muhimu ni kuwa ikiwa kila kitu kinafanywa "in a good faith", bila gubu wala malalamiko yasiyo ya lazima, kuelekezana na kuelewana, kila kitu kinakwenda smooth.
 
Dena Amsi, wakati bado wadogo nilibahatisha dada mzuri kwa kulisha watoto.
Alikuwa anajua kiasi chao ila ratiba ndo ilikuwa inampiga chenga hadi kukumbusha wape sasa hivi.

Ila sasa vitu vingine alikuwa mmmh, saidia siku ziende
 
Last edited by a moderator:
Dena Amsi, wakati bado wadogo nilibahatisha dada mzuri kwa kulisha watoto.
Alikuwa anajua kiasi chao ila ratiba ndo ilikuwa inampiga chenga hadi kukumbusha wape sasa hivi.

Ila sasa vitu vingine alikuwa mmmh, saidia siku ziende
Kongosho, huyo dada basi ujue na yeye alikuwa anapenda msosi. sasa wadada wetu wa siku hizi, wenyewe wanasema wanafanya diet, kwa hiyo msosi haupikwi nyumbani, watoto ni mwendo wa viporo tu mchana kutwa
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom