Kuendesha nyumba kwa remote control

ukiweza kupata ambaye alishazaa, kaolewa akaachika tayari anajua mtoto ni nini? na anajua shida ya maisha. kwahiyo hatakuletea za kuleta sana kama hivyo vimodal ulivyo navyo, tena kabla ya kulala ni ratiba kama sipo wanasali nao! nikiwepo tunasali wote, so kukaa nao chini kuongea nao pia Fixed Point ni muhimu, kuwakumbusha wajibu wao na kusikiliza shida zao, atakwambia tu mshahara hautoshi, mwambie jirekebishe hapa na hapa, nakuahidi next month nitakuongeza, utaona atakavyobadilika, akifiwa na ndugu zake nakwenda msibani, au kama wana mgonjwa nakwenda hospitali na kapesa kidogo! basi utaona watoto wako anakaa nao vizuri, anakuthamini, coz ataona na we pia unamthamini! likizo mara mojamoja huwa namwambia walete wanao waje wacheze na twins, wanakuja mwezi mzima, wakiondoka nawafanyia kashoping, utaona anafurahi na kukuheshimu kweli!
hivyo vimodo unafikiri vina shida na hela? hata kidogo. kila kitu vinapata, na shule vinaenda, basi tu vibweka vyao
 
My dear we acha tu, hata uwabebe mgongoni hawana shukurani........
Wa kwangu kila jumapili yupo huru(ingawa nahofia asidungwe mimba mtaani)
likizo namlipia nauli ya kwenda na kurudi na vijizawadi......
Mshahara kila mwezi nampa.....

Ila hawaishi vituko.... Wepesi kulaghaiwa..... Kununa nuna bila sababu...

Ndo maana nikisafiri lazima niulizie hali huku nyuma, na nikiwepo kazi karibia zote zilizoko mbele yangu nafanya, hii husaidia kidogi kucontrol, pia nini kipo sawa nini kimepinda....i? Ila sio guarantee kabisa...

Ukipata hg mzuri unashukuru
BADILI TABIA hapo kwenye red ndo penyewe. kuna wakati mdada wangu alikuwa ananiletea viburi vya mara kwa mara, nikamwambia isewe tabu, naona umechoka kuishi na mimi, fungasha kilicho chako, nikampa kila kitu chake nikamwambia kesho kutwa unarudi kwenu. akaniambia mama naomba usinikatie tiketi, niache hapa hapa kama wewe umenichoka kuna watu watataka kukaa na mimi. nikamwambia anayekutaka atakupa nauli ya kukutoa kwenu kama mimi nilivyofanya. wewe sio mzigo, nilikuchukua kwenu na nitakurudisha kwenu, ukaage tena kwenu kuwa unaenda kwa bosi mwingine.
si akamwambia yule dada aliyekuwa anamdanganya, enzi hizo naishi Moshi, mdada kwao Songea, akapiga hesabu nauli ya Songea akaona parefu, alitaka vya bure, akamwambia basi atatafuta mwingine pale pale. mdada akaja kuniomba msamaha eti anaomba abaki tu, nikamwambia NO
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Hata siku ukisafiri usipotoa maelekezo yoyote
kila kitu kitakwenda sawa sawa tu.

Wababa wengi kutokuwepo kwenu ndiyo amani yao,
wanapata muda wa kuchati na wajakazi.
ha haaaaaaaaa, wachati tu, kwa raha zao.........................
ninachotaka nikiwepo wanangu na nyumba yangu iendelee kupata matunzo kama nikiwepo, hayo ya baba hata nikiwepo si ajabu anatafuta hiyo quality time na kijakazi
 
Angalia angalia na kwingine, asije kufanya nungayembe bure

Mafunzo yenyewe ndiyo haya... charminglady usithubutu hata kumsalimia Kongosho...awafunde haohao wa magomeni

He he he, unataka niwe kungwi wako na wewe? Nakupa basi Bishanga, mie ratiba yangu imejaa hadi Dec next yia
Bishanga kungwi...? Kwa hiyo anavaa kanga moja na kumfunda mwali? duh! makubwa............Mimi...Kidume nilipozaliwa tu kila kitu kimekomaa.
 
dah, i wish. nataman life style yenu @Fixedpoinu, cacico.. Kongosho. . . hv we hupendi hayn maisha platozoom hebu fanya fasta nikighairi utaisoma namba!
ha haaaaaaaaaaaaaaaa, unamtishia mkubwa nyau? hatishiki.
Asante my dear, kwa kweli ni maisha mazuri ya kuyatamani kuingia............................
NB: yako yasipokuwa kama yangu usini-quote
 
no Fixed Point c lazma yawe km yako kwa 100% hapo ninamaanisha maisha ya kuwa mama tena mwenye majukumu na anayetambua wajibu wake kwa mumewe na wanawe!
 
Last edited by a moderator:
dah, i wish. nataman life style yenu @Fixedpoinu, cacico.. Kongosho. . . hv we hupendi hayn maisha platozoom hebu fanya fasta nikighairi utaisoma namba!


Unafikiri wana raha hao...ukifika usiku kama jehanam imeingia, tena kama Kongosho kwake ameweka patisheni chumbani mume huku mke kule.....tule maisha kwanza
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom