Sir robby
JF-Expert Member
- Jun 22, 2022
- 2,400
- 4,074
Tanzania chini ya CCM imeshindwa kabisa kukibadilisha kilimo cha wananchi wake. Nakiri kusema toka imepata uhuru wake mwaka 1961 imekuwa na wakulima wadogo wadogo wanaolima kwa kutumia jembe la mkono na mbolea ya kubahatisha miaka yote mpaka leo 2023.
Kilimo hicho ni kigumu sana kwani kinategemea mvua ambazo hazina uhakika. Mavuno ya kilimo hicho ni duni sana kiasi ambacho nguvu kubwa inatumika lakini mavuno hafifu na ndio maana watu wengi wanakimbia kilimo.
Tanzania kama tunataka tuondokane na bei ya vyakula kupanda ni lazima tubadili kilimo chetu tunatakiwa tufanye uwekezaji mkubwa kwenye kilimo. Kilimo kiwe cha kibiashara na cha zana za kisasa kama vile matrekta n.K. Badala ya majembe ya mikono.
Bila kufanya hivyo tutakuwa tunadanganyana tunaimba wimbo na kwa sasa kilimo chetu siyo tena uti wa mgongo tena.