Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Leo asubuhi kama nimeona kichwa cha habari kuwa dr Slaa amejiuzulu au sijiu ndio macho yangu na utu uzima

lakini I am certain...


Unaweka chuki na mtu ana kikundi cha watu pasipo sababu hata thamani yak mbele ya macho ya watu inatoka .Chuki za kazi gani hizi ndugu yangu ?Ama ndiyo kum provoke mzee wa watu kila mara malipo yako yanaingia kaka ?
 
Hii nukuu muanzisha mada bila shaka kaiona kwenye 'Mtanzania' ya leo front page ambapo Mzee Slaa amenukuliwa akisema kwamba Ukatibu Mkuu Chadema yeye sasa basi anawaachia wengine,amesema hakuna mahali kwenye Katiba ya Chadema panaposema utaongoza milele.Kwa hiyo essentially sio kujiuzulu bali ni kumwachia mtu mwingine UKATIBU MKUU pindi ikiundwa sekretariati mpya baada ya uchaguzi.
 
Wakati huu Chadema wako kwenye mchakato wa chaguzi za ndani, Dr. Slaa ameashiria kwamba itakapofika uchaguzi wao wa Taifa hataendelea na Ukatibu Mkuu.

Dr. Slaa mwenyewe ni member humu javini bila shaka atakujaeleza vizuri. Tunaamini Chadema inao vijana wa kutosha kuendeleza mapambano.
 
Inawezekana kwani hadi sasa kuna mapambano yachini kwa chini ndani ya chadema kuondoa ving'ang'anizi.
 
Ikiwa Dr. Slaa hatagombea Ukatibu mkuu basi bila shaka atakuwa na aim high!.. Mhhnnnnn!.
Yaani naisubiri kwa hamu 2010, baada ya Ramadhan nitakuwa njiani kurudi home.. sitaki kupitwa drama ya mwaka huo.
 
Ikiwa Dr. Slaa hatagombea Ukatibu mkuu basi bila shaka atakuwa na aim high!.. Mhhnnnnn!.
Yaani naisubiri kwa hamu 2010, baada ya Ramadhan nitakuwa njiani kurudi home.. sitaki kupitwa drama ya mwaka huo.


kugombea urais?
 
Leo asubuhi kama nimeona kichwa cha habari kuwa dr Slaa amejiuzulu au sijiu ndio macho yangu na utu uzima

lakini I am certain...

Ungejaribu kumuomba aliye karibu yako kukusomea maana inawezekana miwani uliyokuwa unatumia lenzi ikawa emeeksipaya.
 
Kwa nini GT unatutakia mabaya? Dr. Slaa ni nguzo imara Chadema na amekiimarisha chama wakati wa ukatibu wake. Akifuata misimamo ya Chadema, Dr Slaa ameimarisha demokrasia Tanzania kwa michango yake Bungeni na nje ya Bunge.

Mungu ampe afya njema, aendelee kukiongoza Chama katika nafasi yoyote Mkutano Mkuu ujao utakayampa. Tunamhitaji.
 
Mkuu GT, imekuwaje tena??? Unajua unapoanzisha thread za watu muhimu kama Dr. Slaa inabidi uwe makini kabisa!! Pole sana kwa ubovu wa macho!!!!!!! Pata lense muafaka!!!!! Jamii hapa haijakuelewa kabisa!!
 
labda Dr.kaona kwa uzoefu alionao anaweza kugombea nafasi nyingine katika chama labda ya juu zaidi kwahiyo akaamua kuachia hiyo ya ukatibu mkuu
 
kama hatagombea ukatibu mkuu na ana-aim high, then good luck to him. and may he blessed kwa anachotaka kufanya
 
Mi nasubiri ushahidi wa kukanusha au kuthibitisha.

Mbona aliyeanzisha Tetesi za kingunge kuchana waraka hamumshambulii?
 
Habari ambazo nimezinyaka hivi punde toka chanzo cha ndani kabisa ndani ya CHADEMA zinasema kuwa Mhe. Zitto Z. Kabwe anatarajiwa kuwa mmoja wa wagombea nafasi ya Uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Zaidi nitawafahamisha kadiri muda unavyokwenda
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom