Inasikitisha sana, viongozi wetu wanayajua haya bali ni kwamba hawapo kwa maslahi ya wananchi na nchi hii, wao ni kulimbikiza mali tu na familia zao
Maskini watoto hawa, tena wapo eneo nyeti linaloingizia hii nchi mamilioni ya shilingi kwa mwaka. Watoto wa umasaini wakiwa darasani. Nini cha kujivunia miaka 50 ya uhuru kama hali bado mbaya hivi? hizo fedha wanazoandalia sherehe ya uhuru ( nimeona vijana wa bongo fleva wanjifua uwanja wa taifa mahususi kwa sherehe hii) zingetumika kutatua matatizo kama haya.
Hii siku ipite kimya kimya tu maana so far hamna cha kujivunia zaidi ya majuto. Hata ile amani CCM wanayojidai nayo imetoweka.
Hivi hilo ni darasa au zizi?
Hivi hilo ni darasa au zizi?
Hicho kiboxi ni cha nini?
JK na familia yake, hata zizi haliko katika hali hiyo. Mifugo ya JK iko kwenye hali nzuri sana kuliko hawa malaika waliolundikwa kwenye hilo banda eti wanasoma. Hizi picha zinazidi kunifanya nichukie CCM.
Maskini watoto hawa, tena wapo eneo nyeti linaloingizia hii nchi mamilioni ya shilingi kwa mwaka. Watoto wa umasaini wakiwa darasani. Nini cha kujivunia miaka 50 ya uhuru kama hali bado mbaya hivi? hizo fedha wanazoandalia sherehe ya uhuru ( nimeona vijana wa bongo fleva wanjifua uwanja wa taifa mahususi kwa sherehe hii) zingetumika kutatua matatizo kama haya.
Hii siku ipite kimya kimya tu maana so far hamna cha kujivunia zaidi ya majuto. Hata ile amani CCM wanayojidai nayo imetoweka.
Nimeamini kila shule ya msingi itakuwa na kompyuta.
Baba wa taifa (RIP) alisema ikifika miaka 10 ya uhuru tutawaita mje muone maendeleo yetu. Leo tunaweza kusema hayo maneno kweli?
Hatuna jeuri hiyo, miaka 50 baada ya uhuru ni kama vile tuko enzi za kina mkwawa, kimweri, milambo , halafu mtu na akili yake anasimama kusema tutumie mabilioni kusherehekea uhuru.
Mkuu kuna Halmashauri moja wanapanga kufanya sherehe za kuukaribisha mwana mpya wakati tumefikia kati kati ya mwaka na hapo watatumia mamilioni wakati kwenye wilaya husika shule hazina madawati wala vitabu