Tunatumia mabilioni kwa ajili ya chai kwenye ofisi za serikali, michezo ya wizara, ziara za mafunzo, Magari ya kifahari yasio ya lazima, tafrija za kila namna wakati wanachi wako hivi. Hio ni shule bado hatujaona hospitali, barabara mahakama, huduma za maji, ustawi wa jamii.
Halafu inafika tunaenda kwa wafadhili kuomba fedha za kuendesha nchi.
Kwa kweli hii ni nchi ya masihara.
Wafadhili wenyewe kwa sasa wamechoka maana wanavyokuja huku na kuona matanuzi yetu wanaishiwa hata hamu ya kutoa msaada maana Mkuu wa Mkoa ambaye shule zake kadhaa anaziombea msaada wa vitabu anaenda kutembelea shule hizo na the same mfadhili wa vitabu akiwa anaendeshwa kwenye V8 la milioni 200 wakati mfadhili amekuja na Land Rover 109 iliyoozeeka
Hapo unaona tofauti ya mtoa msaada na mpokea msaada