Kudorora mapokezi ya Rais Samia kutoka Marekani Tatizo limeanzia hapa...

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,017
Sote ni mashahidi tangu juzi kuna kakikundi ambako sidhani kama ni watanzania kweli au wachumia tumbo tu wanaolipwa kushibisha nafsi zao au la!

Tangu juzi tumeshuhudua kukurukakara za hapa na pale za kutaka kuaminisha watanzania wachache kuwa Rais Samia Suluhu alitoa hotuba ya kihistoria. Ile ni hotuba ya kawaida sana.

Kwanza niwajulishe tu walioona na kusoma hotuba ya Rais ni watanzania wachache tena wanasiasa ambao wana access ya Mitandao ya kijamii. Huko vijijini na mikoani wala hawama habari na kinachoendelea. Wengi ktk mikoa ya kanda ya ziwa na magharibi hiki ni kipindi cha kuandaa mashamba ya kilimo ktk msimu wa mvua ujao.


Hata hivyo kumekuwa na jitihada za kutaka kulikuza jambo hili kwa kile kilichoandaliwa kama mapokezi ya Rais kutoka Marekani.

Mbali na vijitangazo vidogo vidogo sijaona tukio lolote mahali popote likishangiliwa na watanzania. Sijaona Tv wala mtandao wa social media hata ule wa vijigazeti la chama.

Watanzania wamesusa. Wamesusa kwa sababu hawafurahishwi na kinachoendelea nchini

Matukio ya kubambikiza watu kesi za ugaidi yamewachukiza sana watanzania wapenda amani, haki na maendeleo. Watanzania wamekatishwa tamaa na namna nchi inavyoendeshwa kupitia Tozo na kodi lufufu.

Watanzania hawawezi kufurahia tukio la Mtu na kikundi cha watu wachache kwenda marekani huku wakiacha uvunjifu mkubwa wa haki za kikatiba kama uhuru wa vyombo vya habari, haki za kukusanyika na kufanya shughuli za kisiasa na uchumi.

Nimuombe Mama Rais Samia Suluhu hajachelewa. Arekebishe mienendo yake ya utawala. Ajikite kulinda haki za wananchi makundi yote wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, watumishi wa umma na wanasiasa.

Akifanya hivyo hatahitaji nguvu kubwa kusherehesha watanzania. Wakiwa na Furaha watampokea mgeni bila kutumwa.

Si Whatsapp, twitter, facebook, youtube wala instagram huoni shamra shamra. Wikendi imepoa sana kama hakuna kitu.
 
Tokea yalipo elezwa ya kua anakwenda kuandika historia kwa kuhutubia baraza la umoja wa matiafa nikajaribu kurudia ya mkapa Kikwete na mwalimu nyerere walipokua wakifanya kitu kama hicho kwa kweli sijaona jipya au cha muhimu kuzidi walio mtangulia, na pengine walio mtangulia walikua Bora, mathalani hotuba ya Kikwete wakati fulani baraza la 66 ile hotuba ilikua bora kuliko, nadhani ilikua ya 2011, huko alielezea kuhusu Tanzania na nchi jirani na Tanzania na hata Afrika kwa ujumla.mengi aliyaongelea yaliokuwa yanavuta attention kuendelea kusikiliza tena.

Huyu wa kwetu zaidi ya promo kwa kweli na ujinga wangu kwenye mambo hayo sijaona la mno!
 
Back
Top Bottom