Kudorora mapokezi ya Rais Samia kutoka Marekani Tatizo limeanzia hapa...

Eti 'Watanzania wamejasirishwa kukamatwa kwa mbowe!'. Mdugu, HV unaishi Tanzania au?!!! Maana tz hii kwa sasa hakuna kabisa anayemzungumzia mbowe zaidi ya mbowe mwenyewe na misukule yake. Ukisikia sana basi ni habari ya kesi yake kupitia baadhi ya vyombo via habari
Watanzania siku hizi hawana maneno mengi Ni vitendo tu.
 
Hawaaminiki unaweza kuta dreamliner ilitumika. Kwani wanalipa kodi? Kwani wanaijua chungu ya mizigo ya tozo wanayotutwisha?
Matumizi mabaya ya tozo. Sisi tunafunga mkanda tujenge nchi watu wanazitumia kwenda kulia bata marekani.
 
Sote ni mashahidi tangu juzi kuna kakikundi ambako sidhani kama ni watanzania kweli au wachumia tumbo tu wanaolipwa kushibisha nafsi zao au la!

Tangu juzi tumeshuhudua kukurukakara za hapa na pale za kutaka kuaminisha watanzania wachache kuwa Rais Samia Suluhu alitoa hotuba ya kihistoria. Ile ni hotuba ya kawaida sana.

Kwanza niwajulishe tu walioona na kusoma hotuba ya Rais ni watanzania wachache tena wanasiasa ambao wana access ya Mitandao ya kijamii. Huko vijijini na mikoani wala hawama habari na kinachoendelea. Wengi ktk mikoa ya kanda ya ziwa na magharibi hiki ni kipindi cha kuandaa mashamba ya kilimo ktk msimu wa mvua ujao.


Hata hivyo kumekuwa na jitihada za kutaka kulikuza jambo hili kwa kile kilichoandaliwa kama mapokezi ya Rais kutoka Marekani.

Mbali na vijitangazo vidogo vidogo sijaona tukio lolote mahali popote likishangiliwa na watanzania. Sijaona Tv wala mtandao wa social media hata ule wa vijigazeti la chama.

Watanzania wamesusa. Wamesusa kwa sababu hawafurahishwi na kinachoendelea nchini

Matukio ya kubambikiza watu kesi za ugaidi yamewachukiza sana watanzania wapenda amani, haki na maendeleo. Watanzania wamekatishwa tamaa na namna nchi inavyoendeshwa kupitia Tozo na kodi lufufu.

Watanzania hawawezi kufurahia tukio la Mtu na kikundi cha watu wachache kwenda marekani huku wakiacha uvunjifu mkubwa wa haki za kikatiba kama uhuru wa vyombo vya habari, haki za kukusanyika na kufanya shughuli za kisiasa na uchumi.

Nimuombe Mama Rais Samia Suluhu hajachelewa. Arekebishe mienendo yake ya utawala. Ajikite kulinda haki za wananchi makundi yote wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, watumishi wa umma na wanasiasa.

Akifanya hivyo hatahitaji nguvu kubwa kusherehesha watanzania. Wakiwa na Furaha watampokea mgeni bila kutumwa.

Si Whatsapp, twitter, facebook, youtube wala instagram huoni shamra shamra. Wikendi imepoa sana kama hakuna kitu.
Daaaaa kumbe kipusa ana rudi leo du watz tuna roho mbaya hata kumpokea kipusa katoka un
 
Heri angeenda kuuza nyungu au bupeji au hata NIMRICAF.

Value ipi kaongeza kwenye mkutano ule?

Ajabu eti anaongelea dilemma ya kulinda maisha dhidi ya uchumi.

Kuna dilemma hapo? Awaulize wanaume wa shoka kina Museveni na kina PaKa kama kuna dilemma hapo.

Tumekuwa kituko!
😅 bora hata sijapoteza MB zangu kuangalia
 
Aisee!
Screenshot_20210925-144357_1.jpg
 
Back
Top Bottom