Kudhalilishwa ofisini kwa Said Mwema

Kudhalilishwa ofisini kwa Said Mwema

Umesikia maelezo kutoka upande wa pili?

Una uhakika gani anayoongea huyu mzee ni ya kweli au ni mzushi

.........Wee umerudisha hela za rambi rambi au unadhania watu wamekusahau? Huna haki ya kuongelea mambo ya kiusalama au yanayohusu Polisi maana yalikushinda ukatimuliwa kama Mbwa. Huna jipya!!
 
uwezo wako wa kufikiria unatia shaka!!
..........Kwa kifupi alikuwa Polisi hapo zamani, akatimuliwa. Kwa upande wangu simshangai kuwa na uwezo mdogo wa kufikiria ( Polisi maana yake alifeli f4 au f6 kwa kipindi hicho)
 
SAJEN ALIKO JACKSON
MWANJONDE MWARILINGO
MWAIBATA MWAKYOMA
C/O TAWI LA CCM
LUGURUNI KATA KWEMBE
S.L.P. 9601 KINONDONI
DAR ES SALAAM

KUMB TA/JM/M/188 05/10/2013

MHE. RAIS DR. JAKAYA KIKWETE 0756563169
S.L.P. 20
DAR ES SALAAM

K.K:
MH: MKUU WA WILAYA
MKOA WA PWANI


YAH: KUDHALILISHWA OFISINI KWA MHE. SAID MWEMA MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIA NA AFISA WAKE KUWAAGIZA POLISI KWAMBA AKIJA HUYO MZEE MWANJONDE MLETENI OFISINI KWANGU.

Kwa heshima naleta malalamiko yangu kwako nakuomba uunde tume ikiongozwea na Katibu tawala mhe. Mkuu wa wilaya Bagamoyo kwa malalamiko yangu hapo juu.

Tarehe 4/10/2013 nilifika ofisi ya Mhe. Said Mwema pale mapokezi afisa wa polisi aliyevaa unifomu za polisi akasema mzee mwanjonde usiende ofisini. Kwa kuwa tumeletewa taarifa kwamba ukija tumuite bosi wetu, mara akaja bosi wao akasema mzee hutakiwi kuingia katika ofisi mhe. Said mwema. Twende kwa bosi wangu na kunishika shati kama mharifu. Baada ya kufika kwa bosi wake akasema mzee shida yako nini ya kuja mara kwa mara hapa?

Nikamjibu kwamba ninafuata ya barua zangu. Akasema kuwa sitaki kusikia habari za barua. Akasema kuwa yeye ndiye bosi wa jengo hili. Nimeagizwa ni marufuku kuingia kwenye jengo hili. Yule polisi aliyenileta kwake akasema tekeleza amri hii.

Akanishika shati twende mzee. Tukatelemka mpaka chini kwenye ofisi ya mapokezi. Pale kaunta palikuwa na askari watatu (3) mmoja kavaa nguo za kiraia. Akawauliza wenzenu wako wapi? wakajibu wako kule nje akawaita wote njooni, walipofika wote pale mapokezi akawaambia kwamba ni marufuku huyu mzee Mwanjonde kuja hapa ofisini, na raia walikuwepo wakishangaa kwa umri wangu huu na ndevu nilizonazo nyeupe umri wa miaka 77 akanishika twenda mzee mpaka kule nje. Na wengine kule nje wananifahamu hivyo wakawa wanashangaa kwamba huyu mzee kafanya nini huko ndani?

Baada ya kutoka, wale wafuasi wa CHADEMA wakasema umefanya nini huko? Wakaniambia siku zote tunakwambia ondoka CCM wewe unang’angania huko CCM, haya sasa yamekupata je utaendelea kukaa CCM? Nikawaambia ndiyo nitafia huko huko CCM. Siendi kwenu ninakwenda kwa rais wangu Mhe. Rais Dr. Jakaya Mlisho Kikwete na kwa Mhe. Abdallah Haman, katibu mkuu wa CCM Taifa bara.

Na kwa barua hizi za tarehe 05/08/1998, 30/01/1995. Najibu la Ikulu kumb PP/181/39 ya tarehe 7/4/1995. Na 23/09/1997 NA 30/07/1997 jibu la Ikulu Kumb Na. 480/15/10/1997.
Kumb TA/JM/M/199 ya tarehe 23/09/2009
Kumb TA/JM/M/186 ya tarehe 21/09/2013
Kumb TA/JM/M/44 ya tarehe 30/09/2013
Kumb TA/JM/M/25 ya tarehe 30/04/2013

Gazeti la Dar leo la 17/05/1999 milioni 200 za ukarabati wa barabara zazua kasheshe Tanga. Akitoa ufafanuzi kuhusiana na utata huo Mhe. Mkuchika alisema kwa kuwa Wizara ya Ujenzi iliwahi kuunda tume ya kuchunguza tuhuma hizo ni vyema kikao kuagiza ripoti ipelekwe na kusomwa mbele ya wajumbe.

Halafu itolewe adhabu kwa wahusika Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete adhabu iliyotolewa ni kuwahamisha kituo na kuwapandisha vyeo bila kuwachukulia hatua. Nao wabunge wa mkowa wa tanga waliokuwa katika kikao katika hotel ya Mkonge Tanga walimtisha Rais wao Mhe. Rais Mkapa.

Wafanyakazi wa Wizara ya ujenzi walimuandikia Rais mstaafu Mkapa na barua hizo wakaniletea mimi nidpo nikazileta Ikulu. Na Rais Mkapa akanituma kwa Mhe. Adadi Rajabu Mkurugenzi makosa ya jinai nchini Tanzania.

Sababu za kunipiga marufuku viongozi wa wizara ya ujenzi mkoa wa Tanga waliuza Computa, mipira ya magari, spea za magari wakahonga polisi wa kituo cha chumbageni na mahakimu wa chumbageni mwezi wa 10/2006 RCO (M) ambaye alikuwa anawalinda maafisa wake Kinondoni ofisi ya kamanda wa polisi yupo mpelelezi anapenda rushwa nimempelekea Mhe. Robarti Manumba ndio maana hawanitaki. Pokea kopi ya Mwl. Julius Nyerere Kambarage yenye Kumb RM/12/D ya tarehe 02/12/1997 nilikwenda kumpelekea barua ya tarehe 30/07/1997 wafanya kazi wa Wizara ya Ujenzi ombi kwenu wote nawaomba mchango kupitia A/C J2445883100 CRDB/TAWI LA TANGA ombi la nafasi ya Mhe Said Mwema asipewe mchango na ya Mhe. R. Manumba.

Naomba tume utakayoiunda ije kwangu ili niwaeleze yote yaliyotokea huko Tanga na yaliyotokea huko Wizara ya mambo ya ndani.


Kidumu chama cha Mapinduzi
Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko

WENU RAIA MWEMA
SAJEN ALIKO JACKSON MWANJONDE.
Nakala:
Mhe. Bilali Makamu wa Rais
Mhe. Mizengo Pinda Waziri Mkuu
Mhe. Immanuel Nchimbi Waziri wa Mambo ya Ndani
K.K: Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na sababu ni kwa sababu nimepigwa marufuku ofisi ya Said Mwema. Nataka kufika kwake nakuomba wewe ndo unipeleke.
Mh. Abdallha Mari K/M/CCM Taifa
Mh. Phillipo Mangula M/K/CCM Taifa Bara

Kwa harakaharaka nimesoma huu ujumbe sikuuelwa vizuri lakini kwa hichi kidogo nilichoelewa nafikiri huyu mzee anastahili alivyotendewa.
 
Huyu Mzee anachoongea sijakielewa kabisa na si Anatoka kwenye kata lililopo Shamba letu Kwembe Sasa huko Tanga kunani? Ningeomba Mtu ayaweke madai yake na habari kamili ili ieleweke..... mimi nilichoelewa kuwa alipigwa Tanganyika Jeki ndio kesi yake mara Nyerere mara Raisi Mstaafu Mkapa??? now Kikwete! ooough!
 
Mzee akae na mwanasaikolojia mmoja na mwanasheria mmoja wamsaidie. Mwnasheria atasaidia kama akili za huyu mzee zipo sawa. Mwanasaikolojia ata chip in incase akili ya mzee huyu itaonekana ina matatizo -kitu ambacho nami nina wasi wasi.
 
Mungu wangu.Said Mwema Ambaye nu Msomi mwenye Shahada ya Sheria ndiye anayehalakisha mambo ya kipuuzi kama haya?

Ndugu yangu kupata uhakika juu ya kinachozungumzwa ni muhimu hivyo acha mawazo mgando na hasi kwa kusikiliza upande mmoja
 
huyu mzee hata sijamwelewa anataka nini hasa?tupate taarifa na upande wa polisi pengine picha inaweza kamilika
 
Huyo mzee ni 'bushlawyer'. Mabushlawyer wanaweza kupotezea muda watu kwa usumbufu wa mambo yasiyokua na ushahidi. Wanahitaji msaada wa wanasheria kuona kama madai yao ni sahihi. Tatizo mabushlawyer ni wabishi wanajua bila kwenda shule.
 
Umesikia maelezo kutoka upande wa pili?

Una uhakika gani anayoongea huyu mzee ni ya kweli au ni mzushi

Hiki kizee kichochezi, sidhani kama askari hawana akili kumshika mtu shati kama mtuhumiwa wakati ni mgeni.

Tusikie na upande wa pili wa shilingi.
 
Mbona sijamwelewa hafu angalia hata uandishi wake na hoja zake anaonesha anamatatizo flani ya kinafki na kujikomba hawa wazee smtms wanafikiri kila jambo ni la miaka hiyo lakin am sure hajaeleza yote itakuwa walimwambia sababu ya kupigwa marufuku ila yy hajaandika hapa
 
haya nimesoma mchango wa wanajamii forum kuhusu mzee wetu mwanjonde ,wengine wanachangia wakiwa na chuki kiasi cha kushangaza kabisa na wengine ndo wale ambao siku zote kwao mipango ya serikali ni mibaya hakuna zuri.natoa ushauri mfuatilieni,onaneni naye,zungumzeni naye naamini hamtaingia kwenye mtego wa `MWANAJESHI FAKE aliyepiga picha na viongozi wa juu wa CDM.binafsi namfahamu mzee huyu anapita kwenye maofisi mengi anachoongea hakieleweki mwisho huomba nauli mshaurini atulie nyumbani .
 
maelezo ya huyo mzee yanajikanganya! Haeleweki anamlalamikia nani! Mara Mwema,mara DCI,mara Ujenzi Tanga,mara Mwal Nyerere,Ah! Nadhani uzee wake umekuja vibaya.
Macc mnamtetea kada wenu ee!
 
Back
Top Bottom