Kuchelewa kwa Mishahara ya watumishi wa umma mwezi October 2012

Kuna tatizo kwenye mfumo wa utoaji mshahara endelea kuvuta subira baada ya wiki mbili mambo yatakuwa shwari. Sawa.....!!?
:coffee::coffee::coffee:
 
Mishahara ni midogo kiasi watu wanashindwa kuweka akiba ya wiki moja au mbili baada ya mwisho wa mwezi ili kuweza kuhimili dharura za mshahara kuchelewa kama hivi.
 
Hivi ni kitu gani kinasababisha mishahara ya watumishi wa umma inachelewa sana siku hizi!
Kwa mafano kuna wizarra hadi leo hazijalipa

Haya ni madhara ya kutokufikiria mambo kwa kina wanakurupuka kuongeza mishahara kila mwaka badala ya kukabiliana na mfumuko wa bei matokeo yake yanaongeza matumizi ya serakali huku uwezo wao wa kukusanya kodi ukiwa mdogo sasa ndio madhara yake yamkini itafikia wakati watashindwa kulipa mishahara kama ilivyokuwa kwa serekali ya ugiriki ambapo ililazimika baadae kupunguza mishahara ya watumishi wake na kupunguza wafanyakazi. Hata enzi ya mwinyi kunawakati walilazimika kupunguza wafanyakazi ili kupunguza matumizi ya uma. Mkapa yeye katika yeye alizibiti mfumuko wa bei lakini hakuajiri ikiwa ni katika harakati za kubana matumizi ya uma. Sasa sijui hawa jamaa wanaoongeza ajira na mishahara kila kukicha huku uwezo wao wa kukusanya kodi ukiwa mdogo sijui watafanyaje?
 
Hivi ni kitu gani kinasababisha mishahara ya watumishi wa umma inachelewa sana siku hizi!
Kwa mafano kuna wizarra hadi leo hazijalipa

Hiyo ni kukutahadharisha kuwa jitahidi uwe mjasiriamali ili kuepuka kutegemea usumbufu kama huo ambao upo chini ya uwezo wako!
 
Bado pesa zimeingizwa kwenye fixed Acount,zikiwa tayari tutalipwa,maana hata kwenye
halmashauri bado hawajalipwa.
 
Acha kulalamika unatia aibu watumishi wa umma

Mh kutia aibu gani wewe ndio unatia aibu kuficha ukweli ...tunajadili chanzo nini si tuliambiwa mambo hayo tena ni bai2!Amka ndugu yangu mfumo huu ukikakaa kimya utaliwa wima!
 
Samahani watumishi wa umma, huenda pesa ya mishara yenu ilitumika kwenye ziara ya mkuu huko Oman. Subilini dicember!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Lakini ni muhimu pia kujua mwezi uliopita zililipwa tarehe ngapi hivyo ikifika tarehe hiyo na kupita ndipo unaweza kuuliza. Kwa mfano ninapofanya kazi mshahara ni kila tarehe 18 ya mwezi hivyo mshahara wa October tulishapokea tarehe 18.10.2012. Kwa maana hiyo tarehe 18.11.2012 tutapata wa November.
 
Hadi leo,bado wengi hawajapata isipokuwa wachache wenye akaunti katika Benki ya Makabwela,yaani NMB. Nyaraka za mishahara zinaonesha kuwa wale wafanyakazi walioshushwa mishahara wataendelea na 'adhabu' yao. Pia 'arrears' hakuna. Hakujapatiwa suluhisho kama aliyoahidi Profesa Rwekaza S. Mukandala,Mkamu Mkuu wa UDSM. Mambo yaleyale,watawala walewale...
 
Tangu alipopelekwa hapo prof.uchwara mukandara chuo kimeharibika vibaya mno!
 
Wadau hadi leo tarehe 2 november kahama bado hatujalipwa mishahara ya mwezi october na wanajitetea kuwa payroll ilikosewa na hivyo kurudishwa hazina,lakini kwa taarifa kutoka mbeya zinasema kuwa na wao payroll ilikosewa ikarudishwa hazina ila wao wameshalipwa tangu jana tarehe 1 november,,,Je kwa kahama ni viburi vya viongozi wa halmashauri ya kahama ambavyo tumevizoea kila siku??
Pili kwa kuwa serikali tukigoma wafanyakazi inatupeleka mahakamani kuzuia kila kitu,je kwa hili na sisi watumishi wa kahama tuiburuze halmashauri mahakamani???au tuandamane ili aliyesababisha huu uzembe ang'oke madarakani coz nahisi anataka kuchezea maisha ya watu..
Wanasheria tupeni mawazo ya kisheria ili tuweze kuwadhibiti hawa watu wazembe serkalini coz watu wameshasema kesho jumamosi kama hawataingiza ni lazima j3 asubuhi siku ya kazi watumishi wote ni kutinga halmashauri ya wilaya kahama ili watukabidhi mtu aliyekwamisha mishahara yetu..
 
Mkipata mutwambie na si mpaka mkikosa hiyo miishahara yenu ndio mje hapa,mbona mkipata hamtutangazii,sasa unataka sisi ambao hatuhusiki tufanyeje,au unataka tulie wote oh jamni Kahama hawajapata mishahara ,jamani Kahama ooh,haya basi nimekusaidia kulia ,utapata mshahra wako na lazima uniambie bana si nimekusaidia kulia
 
Ok nimekuelewa mkuu lakini utambue kuwa nchi yetu bila maandamano huwa haiendi,,hivyo hapa hatulii bali tunawaeleza ukweli wale wahusika wakuu kuwa wakiona kimya wasidhani tumeridhika na hali bali wajue tunawavutia muda tu.
pili kuajiriwa sio utumwa bali ni sawa na ujasiliamari mkuu isipokuwa kuajiriwa ni ujasiliamari kwa tusio na mitaji.
 
Back
Top Bottom