Kubet ni janga jipya, labda ni pacha wa shisha

Gambling kuwa ni sehemu ya pato la taifa?
mnawatajirisha wahindi tu!
Lakini dunia nzima Kamari zipo, ila shida umri wa watu wanao-bet hapa kwetu!
Msikilize Jambazi anakwambia dogo wa miaka 19 ameshinda 1.6m!
Just imagine mzao huo ukishaamini maisha ndio yanaendeshwa kwa Kamari, huku wengine kwa singeli, huku BSS!
hili taifa miaka 30 ijayo litaendeshwa na hao wacheza Kamari kweli?
fikirieni ktk taswira kubwa zaidi

Ujui kuwa wanalipa kodi? Mbona unakua mjinga ?
 
Acha tu inaongeza pato la nchi . Kwan shisha inaongeza nini kwa taifa letu
Unga, kokeni na heroin zinazalisha mno pesa, kwanini basi taifa lisiwekeze huko kama lengo letu ni kupata pesa yeyote hata haramu!
hatuhitaji kila pesa, bali zile chache zilizokuwa na misingi ya kukuza uchumi na taifa lenye malengo makubwa Zaidi!
 
Hizo hela za kubeti wanapataga wap jamani? Na je kila siku hao vijana wanashinda.?
 
Jinamizi jipya limeanza kutanda nchini kwetu hasa katika miji mikubwa.
Dar Es salaama imeshakuwa ktk hali ngumu Zaidi.
ukimtazama mh. Makonda alivyotolea macho issue ya shisha (sisemi kuwa ni issue ndogo) ila kuna tatizo kubwa Zaidi ktk kubet!
hii ni kamali kama zilivyokamari nyingine zote. Ni halali kwa kuwa watoa huduma wamesajiliwa, ila technically ni mchezo haramu maana kwa baadhi inakuwa kama uteja!
kwa kukosa maadili watoto wadogo yaani age around 16 - 24 ndio wengi wapenzi wakubwa wa ku-bet EPL na karibu kwa wiki mara 10 na Zaidi, sasa vijana hawa wanaoishi kwa Kamari itakuwaje!
Bora shisha zipo mitaa ya vibosile, ila hii ku-bet ipo kitaa, ushahilini kabisa na huku ikisindikizwa na zile za kubet kwa simu!
nadhani tathmini ya kina inahitajika kuitazama hii michezo na kujenga sharia za kuregulate kwa maana ya maeneo, wateja na adhabu kwa atakayekiuka masharti, vinginevyo tutaangamiza vitoto vyetu!
Tumefika hapa kwa sababu ya mawazo mgando ya viongozi wetu wanaofikiria kazi ni kilimo tu. kubeti ni biashara kama biashara nyingine duniani kote ipo na wanalipa kodi kama biashara nyingine wezetu wanaoiheshimu kama biashara ime add value kwenye uchumi wao,sisi kila kitu kazi yetu ni ku beza tu kama tunavyo beza michezo wakati majirani zetu kama kenya wanatumia michezo kutengeneza ma milionea.
 
Kwenye Bunge la Bajeti ZZK alishauri wizara ya habari na michezo iwekw sheria itakayodhibiti mapato ya betting hili yaweze kuendesha shughuli za kimichezo hapa nchini. Nashangaa uyu kiazi anakuja kupiga kelele hapa uku ajui kama inaingoza pato la taifa.
 
Bora tu wapoteze mda kwenye kubet kuliko kuishia kubwia unga au kuvuta mabangi
Bora ku~bet eeeeh....!? Kuna majanga huko usiombe. Kwa mfano kama ww mpenzi/mmeo ana~bet then siku hiyo katia mzigo wa kutosha alafu ngoma zisipeleke anaweza shindwa piga ipupa akirudi nyumbani sasa sijui kama uta~enjoy akishindwa piga hiyo kitu. Betting dah (SHAKAMOOH MHINDI)
 
Mkuu tatizo watu wengi wanasoma mada ili wareply na sio kuelewa,una point ya msingi sana kama mtu atakusoma kwa makini,

Hata kama wanaondesha hizo betting zenyewe wanalipa kodi but still kwenye kucheza kamari hakuna kitu chochote kinachozalishwa! Hakuna bidhaa yeyote inayozalishwa na kuingia kwenye society kwa kubet!

Mfano mkulima atalima na atauza mazao yake na kulipa kodi,mkulima atapata fedha,serikali itapata kodi na hapo hapo bidhaa iliyozalishwa na mkulima itawaendea walaji ila kubet hakuna production ya bidhaa yeyote hapo!

Namuunga mkono mleta mada, tuisome na kuitafakari kwa umakini hii mada.
Wewe na mleta mada hamjui kitu, hiyo unayoandika ni simple mind brain,,,, kama unaweza au una akili ya kuona mbali ukajifunza, basi michezo ya bahati nasibu au gambling unavoita ndio hustengeneza watu wanaothubutu kutafuta,,,,,, mfano mkubwa ni ulaya na hasa uingereza,,, sio kwamba pesa wanazopata wote wanaishia kutapanya la hasha ndio wakipata mitaji wanayochangiana wanafanya hayo uliyoandika. Ndio mana serikali siyo wajinga kuruhusu haya mambo,,, i can't explain more......
 
Had leo sijui how to bet,ila online betting ni janga zaid kwa watoto.Wanafunz wana bet sana na wanapuuza masomo kabisaaa
 
Dar es salaam watu wamezaa bila mpango hela hakuna, wazazi hawajiwezi! Acha vijana wabeti tupate ela ya kula! Naweka jero timu nne kila siku sikosi mpunga wa supu! Ukinia hela ya mtaji naacha
 
Wewe na mleta mada hamjui kitu, hiyo unayoandika ni simple mind brain,,,, kama unaweza au una akili ya kuona mbali ukajifunza, basi michezo ya bahati nasibu au gambling unavoita ndio hustengeneza watu wanaothubutu kutafuta,,,,,, mfano mkubwa ni ulaya na hasa uingereza,,, sio kwamba pesa wanazopata wote wanaishia kutapanya la hasha ndio wakipata mitaji wanayochangiana wanafanya hayo uliyoandika. Ndio mana serikali siyo wajinga kuruhusu haya mambo,,, i can't explain more......
How can gambling affect your life? | GamCare
unaweza kuipitia tu kwa ajili ya kujiongezea ufahamu!
 
Back
Top Bottom