Vijana wa sasa na ndoa ni sawa na 'kubet'

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,514
Habari wakuu,

Niende moja kwa moja kwa mada yetu tajwa yenye kichwa cha habari kisemacho, vijana wa Sasa na ndoa ni sawa na 'kubet'.

Vijana wa sasa wengi wao wanaoingia kwa ndoa wanaingia kwa woga, kwakuwa washaona mabroo na mashangazi walivyokanyaga nyoka hivyo na wao wanapoona jani wanastuka.

Vijana wengi huingia kwenye mtanange wa ndoa kama wanaenda 'kubet' mpira.

Kama ilivyo kwenye kubet' kuna kupata na kukosa ndivyo na ndoa za vijana wa sasa zilivyo yaani hazieleweki, wengi wao hukosea zaidi na ndoa haijaribiwi.

Kule ukiingia umeingia, sio sawa na kubet' kwamba utakosa alafu ujaribu tena, hapo ndio panakuwa patamu.

Tena wanakuwa washajipanga kabisa kuwa nikibet tu huyu mwanamke akiwa poa basi ndoa hii nakaa, ila kama ndoa ikiwa moto basi naacha.

Hii ni kwa vijana wote wa kike na wa kiume yaani wanabet tu ndoa wanajua ikibuma si wanaachana tu kila mtu na lake.

Vijana wa kike nao ndio hubet zaidi maana wao wanakuwa na machaguo yao ya kutosha na mwishowe wanapata ila wanapata potea.

Sasa kinachokuja kutokea kwa kubet' huko ni kumekuwa na mvurugano wa wanaotaka kuoa na wale waliloingia na kutoka nduki nduki.

Wengi wao wanawatisha wale ambao wanataka kuingia kwenye ndoa maana tayari washaona yaliyomo yamo.

Kumeibuka kundi la vijana wa sasa ambao nao wana kauli yao pendwa ya 'kataa ndoa', vijana hawa wanajifariji kwa kupinga ndoa bila kujua faida yake.

Vijana wa Sasa acheni kubet mpira na ndoa, ndoa sio mchezo wa mpira, ndoa inahitaji uvumilivu wa hali ya juu.
 
Sasa unasema ndoa inahitaji uvumilivu, hao waoa na waoelewaji wenyewe uvumilivu hawana maana wameshindwa vumilia kuvuana kyupi mpaka ndoa sasa unakuwaje na matarajio kuwa watakuwa na uvumilivu kisa cheti cha ndoa
 
Ndoa unaifunga kwanza kabla hata haujampata mwanamke au mwanume. Na unaivunja pia

Hizi mbinu ndo huwa natumia kupitia subconscious mind kuendesha maisha huwa natafuta katika invisible eyes then nikikipata I find it in visible world iwe pesa , kazi au mahusiano.
 
Ndoa ni leseni ya mwanamke kufanya utapeli huku akilindwa na sheria. Vijana wa kiume wameshtukia tena na huu ugumu wa maisha ndio kabisa ndoa tupa kule. Kwanza wanawake wenyewe wamekua cheap sana sasa hivi maungo yao yote tunayajua yaliyotakiwa kufichwa tunayaona hadharani na tukiwataka tunawatafuna kwa kitu kidogo tu sasa ndoa ya kazi gani. If i get free milk why buy a cow?
 
Back
Top Bottom