Kubet ni janga jipya, labda ni pacha wa shisha

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,032
2,000
Jinamizi jipya limeanza kutanda nchini kwetu hasa katika miji mikubwa.
Dar Es salaama imeshakuwa ktk hali ngumu Zaidi.

ukimtazama mh. Makonda alivyotolea macho issue ya shisha (sisemi kuwa ni issue ndogo) ila kuna tatizo kubwa Zaidi ktk kubet!

hii ni kamali kama zilivyokamari nyingine zote. Ni halali kwa kuwa watoa huduma wamesajiliwa, ila technically ni mchezo haramu maana kwa baadhi inakuwa kama uteja!

kwa kukosa maadili watoto wadogo na vijana yaani age around 16 - 24 ndio wengi wapenzi wakubwa wa ku-bet EPL na karibu kwa wiki mara 10 na Zaidi, sasa vijana hawa wanaoishi kwa Kamari itakuwaje!

Bora shisha zipo mitaa ya vibosile, ila hii ku-bet ipo kitaa, uswahilini kabisa na huku ikisindikizwa na zile za kubet kwa simu!

nadhani tathmini ya kina inahitajika kuitazama hii michezo na kujenga sheria za kuregulate kwa maana ya maeneo, wateja na adhabu kwa atakayekiuka masharti, vinginevyo tutaangamiza vitoto vyetu!
 
2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,032
2,000
betting watu wanabet popote hasa kupitia smart phone ukisema wa regulate maeneo ya kubet ni kazi bure tu....
any way wacha vijana watafute pesa.. wasipobet unataka washinde wanapiga puli au?
Online betting au any other electronic form including using mobile services ni rahisi to control sababu owner wa cellphone au mchezaji ana declare umri au anaposajiliwa unaweza to verify umri!
napozungumzia uswahilini unapaswa uje uone hizo betting stations na vijana wanaoshinda hapo!
hii issue mimi naizungumza kitaifa, sio issue ya individuals, sijui taifa linalotegema vijana wacheza Kamari litafanikiwa vipi!
fikiri kwa makini, tumia brain please, sio lips au fingers!
 
2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,032
2,000
Acha tu inaongeza pato la nchi . Kwan shisha inaongeza nini kwa taifa letu
Gambling kuwa ni sehemu ya pato la taifa?
mnawatajirisha wahindi tu!
Lakini dunia nzima Kamari zipo, ila shida umri wa watu wanao-bet hapa kwetu!
Msikilize Jambazi anakwambia dogo wa miaka 19 ameshinda 1.6m!
Just imagine mzao huo ukishaamini maisha ndio yanaendeshwa kwa Kamari, huku wengine kwa singeli, huku BSS!
hili taifa miaka 30 ijayo litaendeshwa na hao wacheza Kamari kweli?
fikirieni ktk taswira kubwa zaidi
 
Kapyungu A

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
3,510

litakuwa taifa la wachache
 
Kelvin X

JF-Expert Member
Jun 28, 2011
1,197
2,000
kuna zile madude unaingiza coin ni za mchina zipo kwenye mabar zile ndo balaa zaidi
 
GUI

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
1,848
2,000
betting watu wanabet popote hasa kupitia smart phone ukisema wa regulate maeneo ya kubet ni kazi bure tu....
any way wacha vijana watafute pesa.. wasipobet unataka washinde wanapiga puli au?
Mkuu nimeona hapa Mbeya pale stand ya kabwe ghorofani kila nikipita vijana wamejaa pale sana.
Huu mchezo umevuta vijana wengi sana kiukweli
 
msumeno

JF-Expert Member
Aug 3, 2009
2,833
2,000
Nilipata kumchukua Kijana wa mtaani toka kwa single mother ili nimleee na kumpa elimu kama mtoto wangu, huwezi amini niliishi nae kwa miezi zaidi ya sita na kwa kiasi kikubwa ali improve sana katika masomo pale MEMKWA, ndio Betting ikaanza , kidogo anitumbukizie na mtoto wangu katika uraibu huo, nauli ya shule nna pesa ya kula shule alibett , akadrop shule akawa anashinda vibandani , SIKUA NA JINSI NIKAMTUMUA HOME NA SHULE IKAISHIA HAPO nilifanya hivyo kumnusuru mtoto wangu, sorry
 
CleverKING

JF-Expert Member
Apr 24, 2014
8,520
2,000
Gambling kuwa ni sehemu ya pato la taifa?
mnawatajirisha wahindi tu!
Lakini dunia nzima Kamari zipo, ila shida umri wa watu wanao-bet hapa kwetu!
Msikilize Jambazi anakwambia dogo wa miaka 19 ameshinda 1.6m!
Just imagine mzao huo ukishaamini maisha ndio yanaendeshwa kwa Kamari, huku wengine kwa singeli, huku BSS!
hili taifa miaka 30 ijayo litaendeshwa na hao wacheza Kamari kweli?
fikirieni ktk taswira kubwa zaidi
Mkuu tatizo watu wengi wanasoma mada ili wareply na sio kuelewa,una point ya msingi sana kama mtu atakusoma kwa makini,

Hata kama wanaondesha hizo betting zenyewe wanalipa kodi but still kwenye kucheza kamari hakuna kitu chochote kinachozalishwa! Hakuna bidhaa yeyote inayozalishwa na kuingia kwenye society kwa kubet!

Mfano mkulima atalima na atauza mazao yake na kulipa kodi,mkulima atapata fedha,serikali itapata kodi na hapo hapo bidhaa iliyozalishwa na mkulima itawaendea walaji ila kubet hakuna production ya bidhaa yeyote hapo!

Namuunga mkono mleta mada, tuisome na kuitafakari kwa umakini hii mada.
 
2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,032
2,000
Nilipata kumchukua Kijana wa mtaani toka kwa single mother ili nimleee na kumpa elimu kama mtoto wangu, huwezi amini niliishi nae kwa miezi zaidi ya sita na kwa kiasi kikubwa ali improve sana katika masomo pale MEMKWA, ndio Betting ikaanza , kidogo anitumbukizie na mtoto wangu katika uraibu huo, nauli ya shule nna pesa ya kula shule alibett , akadrop shule akawa anashinda vibandani , SIKUA NA JINSI NIKAMTUMUA HOME NA SHULE IKAISHIA HAPO nilifanya hivyo kumnusuru mtoto wangu, sorry
Labda utasaidia wachache kuelewa kuwa kumbe kuna "uteja" wa kubet!
Mi nadhani watu wengi hawajaelewa nini kinaendelea ktk ku-bet!
watoto wanaiba nyumbani, vijana wanakaba na kufanya uhalifu wa kutosha kwa ajili ya hii Kamari! lakini pia wapo pia wenye bodaboda ambao pesa zao zote zinaishia huko!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom