Kubet ni janga jipya, labda ni pacha wa shisha

wazee wa Mikekaaaaaaa. Ninyi Msitafute Kazi Endeleeni Kutandaza Mikeka.

Mtakuwa watumwa wa wenye Nacho, ni hatari sana kwa Taifa kuwa na Wategemea Kamari na sio wachapa kazi.

Ni mjinga tu atakae sema heti Mkeka ni Ujasiria Mali!

Hivi mjasiria mali uwekeza maali ambapo anajua kupata ni Bahati na sibu?

Ujinga Mtupu.

Ningekuwa Rais hata kwa dakika 1 ningekamata wote wacheza Mikeka niwacharaze Bakora na Kuwatupa JKT kwa Mwaka 1 wakafundishwe Satadi za kazi.
makampuni ya kubet yalianzia ulaya kwa wazungu hao tunaowasujudia kila siku teh teh teh mimi kwa siku naingiza zaidi ya 30,000 kwa kubet, kama ni hasara hakuna biashara isiyokuaa hasara....mpaka mabenki yanapata hasara mfano crdb pamoja nak na wasomi na PHD zao.....
 
nitajie taifa lililoandaa misingi mizuri ambalo alina ukosefu wa ajira

sihitaji kukutajia maana yapo mengi sana.. natunaposema ukosefu wa ajira usifikiri tunaongelea watu kumi au wawili hapana tunaangalia asilimia za ukosefu wa ajira na uelewa wa hao waliokosa ajira..

Hili somo ni pana sana kwa wewe kuweza kulielewa hapa, lakini elewa kitu kimoja.
1. kuna watu kukosa ajira kutoka na umbumbumbu wao, namaanisha kiwango wa wajinga.
2. kuna watu kukosa ajira kwa sababu za kiteknolojia, idadi kubwa ya wataalam na wageni kufuata malisho mazuri.

Tanzania watu wake hawana ajira kwa kiasi kikubwa ni ujinga walionao maana hata hao waliosoma hawakupata elimu bora ila wamepata bora. Ajira inahusisha na kujiajiri, fulsa za kujiajiri tanzania ni nyingi kiasi cha kupunguza hili tatizo ila kiwango cha ujinga,umbumbumbu,uvivu, uchawi nk kinafanya watu wake washindwe kuzitumia fursa.
Wasomi waliosoma mpaka vyuo vikuu nao kwa sababu ya elimu duni waliopata wameshindwa kujisaidia na kusaidia wengine kupunguza au kusolve tatizo kabisa maana na wao ni mbumbumbu tu kichwani...

Ni asilimi chache sana ya watanzania wanaopata elimu ya msingi na hata hao wanaopata sio bora kuweza kufuta kiwango chao cha ujinga na kusaidia kupambana na mazingira yao.. mfano. "watafiti kuuwawa eti kwa kudhaniwa ni wanyonya damu"
Wasomi waliofika mpaka vyuo vikuu nao wameshindwa kupata maarifa ya kiteknolojia mbalimbali kuweza kujiajili na kuajili wale wasiosoma na mwisho wa siku kupunguza au kuondoa tatizo - maana yake ni elimu duni walionayo haiwezi kuwasaidia au kusaidia.

SULUHISHO; MFUMO WA ELIMU UNATAKA MAPINDUZI MAKUBWA ILI KULETA MATOKEO.
SHULE ZIJENGWE ZA KUTOSHA ILI KILA MTANZANIA AFUTE UJINGA NA KUPATA MAARIFA.

 
Betting betting betting. Achana na hii kitu kabisa. Mimi ni mwanachama active sana wa kubet, lakini sijawahi na simshauri mtu aingie katika kubet. Watu wanachoshindwa kuelewa, betting ni hisabati. Bila kuwa vizuri upstairs na kuweka bidii katika trend za game unazobet huwezi fanikiwa katika kubeti.

Wengi wanadhani betting ni bahati, lakini kiuhalisia betting siyo bahati. Ushindi katika betting unategemea utumiaji mkubwa wa akili kuliko bahati. Michezo kama russian roulete, black jack, keno etc inategemea akili kuliko bahati.

Ukija kwenye michezo ya soka, basket, tennis hii ni fifty fifty na inategemea sana NEURAL networks na probability. Wale waliosoma hisabati wanatambua hiki ni kitu gani. Na ni hii topic ya NEURAL network ipo nyuma ya betting systems na betting softwares. Hata Bookmakers hutumia hii kuandaa odds za timu.

Kwa minajili hii ndo inakuja concept kuwa betting ni proffessional na haipo kwa ajili ya kila mtu kubet. Mtu kama Donald Trump ni gambler mzuri tuu na anamiliki cassino za kubet, huwezi kumuunderestimate mtu kama donald trump kisa tuu eti anacheza kamari.

Kiujumla, betting ni mbaya sana tena mbaya kuliko kama hujui nini unafanya katika betting. Na siwezi kumshauri mtu abet. Na si njema kutegemea betting kama primary source ya income. Though kubet kwa kiasi kama secondary source ya income ni poa as bettng ni kazi na ukitulia inaweza kukuingizia pesa. But ili kunufaika na pesa ya betting, discpline ya hali ya juu inahitajika.
 
Utafikiri wanafanya mtihani
 

Attachments

  • BET 2.jpg
    BET 2.jpg
    35 KB · Views: 58
  • BET.jpg
    BET.jpg
    22.4 KB · Views: 53
Nilipata kumchukua Kijana wa mtaani toka kwa single mother ili nimleee na kumpa elimu kama mtoto wangu, huwezi amini niliishi nae kwa miezi zaidi ya sita na kwa kiasi kikubwa ali improve sana katika masomo pale MEMKWA, ndio Betting ikaanza , kidogo anitumbukizie na mtoto wangu katika uraibu huo, nauli ya shule nna pesa ya kula shule alibett , akadrop shule akawa anashinda vibandani , SIKUA NA JINSI NIKAMTUMUA HOME NA SHULE IKAISHIA HAPO nilifanya hivyo kumnusuru mtoto wangu, sorry
You don't have to be sorry, you did what you had to, to protect your own. Mtoto wa mwenzio akilia mrudishe kwa mama yake lakini akilia wa kwako utabembeleza mpaka jasho litakutoka.
 
Mkuu tatizo watu wengi wanasoma mada ili wareply na sio kuelewa,una point ya msingi sana kama mtu atakusoma kwa makini,

Hata kama wanaondesha hizo betting zenyewe wanalipa kodi but still kwenye kucheza kamari hakuna kitu chochote kinachozalishwa! Hakuna bidhaa yeyote inayozalishwa na kuingia kwenye society kwa kubet!

Mfano mkulima atalima na atauza mazao yake na kulipa kodi,mkulima atapata fedha,serikali itapata kodi na hapo hapo bidhaa iliyozalishwa na mkulima itawaendea walaji ila kubet hakuna production ya bidhaa yeyote hapo!

Namuunga mkono mleta mada, tuisome na kuitafakari kwa umakini hii mada.
We nae.....unadhani kulima rahisi?, we unalima wapi?
 
Labda utasaidia wachache kuelewa kuwa kumbe kuna "uteja" wa kubet!
Mi nadhani watu wengi hawajaelewa nini kinaendelea ktk ku-bet!
watoto wanaiba nyumbani, vijana wanakaba na kufanya uhalifu wa kutosha kwa ajili ya hii Kamari! lakini pia wapo pia wenye bodaboda ambao pesa zao zote zinaishia huko!
Una uhakika?
 
We nae.....unadhani kulima rahisi?, we unalima wapi?
Unaonekana kua uwezo wako wakupambanua mambo ni mdogo sana,
wapi nimesema kulima ni rahisi au ni kazi ngumu? Rudia tena kuisoma hiyo comment yangu uliyoiquote huenda ukaielewa,kulima nimetolea mfano tu na ndio maana nikaanza kwa kuandika mfano..........
 
Jinamizi jipya limeanza kutanda nchini kwetu hasa katika miji mikubwa.
Dar Es salaama imeshakuwa ktk hali ngumu Zaidi.

ukimtazama mh. Makonda alivyotolea macho issue ya shisha (sisemi kuwa ni issue ndogo) ila kuna tatizo kubwa Zaidi ktk kubet!

hii ni kamali kama zilivyokamari nyingine zote. Ni halali kwa kuwa watoa huduma wamesajiliwa, ila technically ni mchezo haramu maana kwa baadhi inakuwa kama uteja!

kwa kukosa maadili watoto wadogo na vijana yaani age around 16 - 24 ndio wengi wapenzi wakubwa wa ku-bet EPL na karibu kwa wiki mara 10 na Zaidi, sasa vijana hawa wanaoishi kwa Kamari itakuwaje!

Bora shisha zipo mitaa ya vibosile, ila hii ku-bet ipo kitaa, uswahilini kabisa na huku ikisindikizwa na zile za kubet kwa simu!

nadhani tathmini ya kina inahitajika kuitazama hii michezo na kujenga sheria za kuregulate kwa maana ya maeneo, wateja na adhabu kwa atakayekiuka masharti, vinginevyo tutaangamiza vitoto vyetu!


Sambamba na hilo kuna kundi kubwa linashinda kwenye runinga kuangalia movie tangu asubuhi hadi usiku, hili nalo lisipotazamwa kwa jicho la tatu huenda mwisho wake usiwe mzuri kabisa
 
Back
Top Bottom