Kubenea na siasa za Kyela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kubenea na siasa za Kyela

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtanzania, Dec 23, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kubenea,  Najua ni mwana JF; hata kama una mapenzi na mtu mmoja kwenye siasa za Kyela lakini magazeti yako hayana haki kuingia kuchafua watu wengine bila sababu zozote. Ulichoandika kwenye makala hii hasa kuhusu Mwakalinga ni majungu na uongo mtupu. Nitafafanua zaidi hapo chini.


   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  haya mtanzania!
  kwanza poleni na barafu
  pili anza utetezi wako WITH IMMEDIATE EFFECT!
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145


  George Mwakalinga sio kijana kama unavyotaka kuonyesha, ana miaka 44 ambayo ni zaidi ya kuwa kijana.

  Mwakalinga alimaliza shule mwaka 1997. Aliajiriwa na Lucent Technologies miezi michache kabla ya kumaliza shule yake. Baada ya kufanya kazi Lucent miaka minane, December 2005 alihamia Huawei Technologies ambako yuko mpaka sasa. Mwakalinga hajawahi kukosa kazi hata siku moja tokea alipomaliza masomo 1997. Sasa huo ni uanafunzi gani baada ya miaka 12? Lengo ni lile lile kudanganya watu waone Mwakalinga ni kijana tu! ni mwanafunzi tu.  George Mwakalinga hakufuatwa London na Mwakipesile au Mwang'onda. Sijui hata kama Mwakipesile amewahi kuwa London miaka ya karibuni. Mwakalinga aliamua kugombea ubunge tokea mwaka 2007 na March mwaka huo alituma watu kuonana na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kyela, bwana Mwakasumi na kumwambia dhamira ya Mwakalinga kugombea ubunge Kyela mwaka 2010. Picha na uthibitisho mwingine wa mkutano huo ambao ulifanyika pale Sativa Kyela vipo. Kumbuka hiyo ilikuwa mwaka mmoja kabla hata report ya Richmond kusomwa bungeni.

  Mwakilishi wa Mwakalinga alikutana na Mwakipesile mwaka 2009, February kumwambia kuhusu dhamira ya Mwakalinga kugombea ubunge Kyela. Hiyo ni miaka miwili tokea Mwakalinga aanze harakati za kuwaambia baadhi ya wadau wa Kyela kwamba ana mpango wa kugombea. Team Mwakalinga iliamua kumwona Mwakipesile baada ya kupata uhakika wa kiasi kwamba Mwakipesile hana mpango wa kugombea. Kabla ya hapo hakukuwahi kuwa na mawasiliano yoyote kati ya Mwakalinga na Mwakipesile. Kuna watu wengine mbalimbali wa Kyeala, wanasiasa na wasio wanasiasa ambao team mwakalinga imekutana nao kuwaambia juu ya dhamira yake ya kugombea. Kama kukutana na mwana Kyela yeyote London au TZ ni makosa, si wataje wote niliowahi kukutana nao wakiwemo waliotumwa kunishawishi nisigombee? Watajeni akina Kifukwe, na wazito wengine huko jeshini.  Wana JF wanajua maana hiyo safari ilijadiliwa vikali hapa JF. Mwakalinga alikuwa Kyela kwa siku sita. Alifika yeye pamoja na familia yake siku ya Jumatatu (24/07/09) na kuondoka Kyela Jumamosi usiku (30/07/09). Kwahiyo, mwezi August Mwakalinga hakuwa Kyela wala hakukaa Kyela mwezi mzima.


  Mwakalinga kila mara anaporudi nyumbani na familia yake yote hufanya sherehe ya pamoja kama njia ya familia yote kukutana pamoja maana kunakuwa hakuna muda wa kutembelea kila mtu katika siku hizo chache. Mwaka 2003 pia alipoenda na familia yake alifanya sherehe nyumbani na kuhudhuriwa na ndugu wote pamoja na majirani. Mwaka huu pia alienda nyumbani na familia ikiwa ni pamoja na mtoto wake wa mwisho ambaye alifika nyumbani kwa mara ya kwanza. Sherehe ya mwaka huu ikaongezewa nguvu na uamuzi wake wa kutangaza nia ya kugombea ubunge. Sherehe ilihudhuriwa na ndugu na wananchi wengine wa maeneo ya jirani. Hakukuwa na speeches wala maneno ya kwamba anaingia vitani.


  Uongo! alitembelea kata 19 kati ya 21. Hakutoa msaada wowote wakati wa ziara nzima. Mwakalinga anatoa misaada mashuleni kwa muda wa zaidi ya miaka 15 sasa. Kuna kitabu cha misaada yote kiko pale Kyela Business Center (KBC) na anayetaka kuangalia anaweza kuhakiki na kuona lini alitoa msaada gani na wapi. Misaada yote hutolewa kiuwazi ila bila sherehe maana muda wote alikuwa hataki publicity.


  I wish Mwakalinga angelikuwa na pesa zote hizo. Uwongo mkubwa sana! Hakuna hata mwananchi mmoja wa Kyela anayeweza kuthibitisha kwamba alipewa pesa kati ya shilingi 10,000 na 100,000. Kama yupo aende polisi kutoa taarifa. Tunamtafuta huyo Edson Matai ili kama kweli ni raia basi tumsaidie kumpeleka polisi ili akatoe ushahidi. Tumechoka Kyela kusingiziwa mambo ya ajabu. Inabidi tuanze kuwashughulikia wale wanaoona wanaweza wakasema au kuandika lolote bila ya chembe ya ukweli.  Hata ukimwuliza kichaa Kyela anajua kuna sehemu panaitwa KBC. Sasa mwandishi gani huyu na uchunguzi wa muda mrefu hata hajui kwamba hiyo kampuni inaitwa Kyela Business Center (KBC)? Hiyo KDC labda ni kampuni ya Kubenea ya kufikirika. Unajua habari za kupewa na watu wengine huwezi kuwa sahihi nazo.

  Sasa huyo Mwakipesile, yeye mwenyewe anagombea ubunge na mara anaratibu shughuli za ubunge za Mwakalinga, mbona hayo maajabu?

  Ni aibu kwa mtu kama Kubenea ambaye unajifanya mpiganaji, kuanza kutumia gazeti lako kuchafua watu wengine bila sababu zozote. Najua ni msomaji wa JF na kwa vyovyote unajua anayeongelewa kuhusu siasa za Kyela ni Mwakalinga mwana JF. Umeshindwa nini kuniuliza mimi Mwakalinga aka Mtanzania kujua ukweli? Mmezunguka kutafuta uchafu wowote na mmeshindwa sasa mnataka kumchafua mtu kwa kumhusisha kwa karibu na watu ambao mnawaona wachafu. Tatizo lenu ni kwamba hamuwezi hata sehemu moja kupata mahali ambapo Mwakalinga yuko karibu au hata anafahamiana na akina Lowassa, RA, Karamang au huyo Patel.

  Mlianza na kusema Mwakalinga amepewa milioni 400. Mmeona wana Kyela wote wamewadharau baada ya kuona hizo milioni 400 hawazioni na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza hata akasema amepewa laki moja na Mwakalinga. Sasa mnaanza majungu mengine ya kijinga, lakini na yenyewe yataishia patupu maana hamna data na uongo haudumu hata siku moja.

  Acheni majungu na fitina; waache wana Kyela wachague kiongozi wanayemtaka kwa utashi wao. Kama mna ugomvi na Mwakipesile, pelekeni nguvu huko, kuanza kujaribu kumhusisha kila mtu haitawasaidia maana wana Kyela sasa wanajua nani anasema ukweli na nani anakimbilia magazetini kila saa kupaka wana Kyela wenzake.

  Kumbe ndio maana watu wengine mnamwagiwa tindikali shauri ya kuandika majungu ambayo hayana ukweli hata mdogo. Ni taaluma gani hizo za kutumiwa na wanasiasa kuandika kila wanalotapika?

  Shame on You Kubenea and your Newspaper!
   
 4. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mhh
   
 5. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Habari nyingi za Kubenea siku hizi zimejaa majungu na uongo sana, what happened to his journalistic expertise?
   
 6. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  bwa ha ha ha

  journalistic expertise ndio nini sasa...
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Dec 24, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,866
  Trophy Points: 280
  Movie;

  Be aware!

  na magazeti ya Kubenea na Kibanda kwenye chaguzi za vyama mbalimbali, na nafasi yao katika jamii!-HATARI!

  Ikiwa tunapiga kelele Mengi na vyombo vyake vya habari! mara RA na vyombo vyake vya habari!

  Then haya magazeti ya akina Kubenea na Kibanda hayana tofauti na ya akina RA na Mengi, wote wanafanya kitu kile kile.AFADHALI mara mia Mengi na RA!

  Kwa waandishi wa habari wahariri kuonyesha personal interest kutumia nafasi zao ni hatari zaidi, hasa katika jamii ambayo hapo kwanza iliwahi kuwaamini! Ulimwengu alishafannya kama haya alijuta baadaye na Rai yake

  semeni yote; Kubenea and Kibanda is another ticking bomb, simply kwa sababu walificha makucha yao, wakaiteka jamii sasa wanajifunua wazi wazi ni akina nani!

  Yaani nchi hii kila mtu atakuwa na gazeti lake sasa!
   
 8. S

  Samwel JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2009
  Joined: Mar 25, 2007
  Messages: 224
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  .

  1.Mwakyembe ka-divorce na Mengi na sasa ameoana na Kubenea.Huyu bwana ndiyo maana alimwagiwa tindikali usoni.Ata gazeti lake limeanza kukosa ubora tena.Limejaa majungu,unafiki na uongo.

  2.Inasemekana Mwanadishi wa nakala hiyo ni Mwakyembe mwenyewe na hiyo ni tabia yake.Alikuwa akiifanya ata kwenye gazeti la Nipashe bila kutaja jina la mwandishi.Sasa huko wamemshitukia alipoandika habari za uzushi kuhusu kuchomwa kisu ili watu waamini eti anaandamwa na mafisadi.

  3.Wapo maswahiba wake hapa(MWAFRIKA NA MASANILO) watatufafanulia zaidi kuhusu Ujinga wa mbunge huyu mwenye mdomo mkubwa.Kulia kwenye media ndiyo kutatua matatizo yake.
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Dec 24, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,866
  Trophy Points: 280
  Tunaruhusiwa kupenda na kuchagua, siwalaumu wapenzi wa Mwakyembe hapo kabla,Ila sidhani baada ya comment yake ya juzi 'kuwa kikwete anafaa kwa urais' bado Mwafrika na Masanilo wanamfagilia huyu jamaa!
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hivi ni huyu Kubenea nilipata habari zake juzi hapa JF? Yuko wapi MkamaP atupe habari zaidi?

  Kubenea, heri tufafanulie hili la ACID ni mke wa mtu au kuandika majungu? Naona SHUJAA wetu siku hizi ungelikuwa Sweden wangelikuambia "Inge Peng'aa" aka kufulia.
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,551
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Waungwana ni bora tubandike hoja kwa hoja na tuachane na mambo personal. Sidhani kama ni jambo la busara kuhusisha crime aliyofanyiwa mtu na mpambano wa hoja hapa JF,binafsi naamini hiyo ni foul...Kama Kubenea angekuwa amepigwa kisu ama risasi,basi huwezi kuja hapa na kusema kuwa ndiyo maana ulipigwa risasi ama ulichomwa kisu,ni sawa na mnapodai kuhusu kumwagiwa tindikali,kama hayo ya kumwagiwa tindikali hayahusiani na dhumuni hasa la mjadala huu ama hoja zake,basi si vyema kuzi bring up kwa style hiyo kwasababu ni kama uonevu,kwani kumwambia kuwa alifanyiwa shambulizi la kinyama kwa kukosa hoja ni sawa na kumdiscourage na yeye kutoa hoja zake hapa JF,na kama shambulizi hilo alifanyiwa kwasababu nyinginezo kama inavyokuwa speculated kuhusu mke wa mtu,je hilo linahusiana kivipi na uandishi wake?Ama uwezo wake wa kuchangia hapa JF?ama linahusiana vipi na makala yake hiyo kuhusiana na kina Mwakalinga?Na kwahiyo watu mnaojiita great thinkers mnakubaliana na watu kujichukulia sheria mkononi?Kuna mtu humu ndani ambaye hajawahi kumuudhi mtu mwingine the same way Kubenea alivyomuudhi mshambuliaji wake?Na kama wamo watu ambao wameshawaudhi wengine kwa namna moja ama nyingine,je muna encourage kuwa wajichukulie sheria mkononi?Na kwahivyo basi hata yule aliyem mwagia tindikali Kubenea kama na yeye anapita hapa JF basi anafurahia tu na kuona amefanya jambo la maana.

  So naamini kabisa ujumbe ungekuwa umefika bila ya kum "Blackmail" victim wa crime kwenye mijadala,hiyo ni personal issue,ni shambulizi lililomwathiri kwa kiasi kikubwa na si ustaarab kufurahia mabaya yanayompata mtu na on top of that unam nyanyapalia.
  Ma two cents.
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  jmushi1,

  Unayayoyasema ni kweli. Ila jamaa hapa kaBOIL sana au katumiwa.

  Angeliweza kumuandikia moja kwa moja Mwakalinga na kumuuliza ili apate habari kamili. Angeliuliza hata watu wanaoonekana kumfahamu Mwakalinga na tungelimpa habari zote. Sasa mtu kafanya kazi miaka kibao na wewe bado unaandika NI MWANAFUNZI? KBC unaandika KDC na unaipa hadi kirefu chake kilicho na makosa pia.

  Sorry, mie mtu kama huyu namuona kama St. Claus anayeleta nyumbani zawadi ya majungu. Dawa si kuikataa au kuijadili hiyo zawadi yake. Dawa ni kumnyang'anya hiyo fimbo yake na kumtandika na mwisho unaMSUKUMIZIA hilo fimbo lake sehemu sehemu na kumtoa baru hadi huko kwake Finland na asirudi milele.

  [​IMG]
   
 13. K

  Kijunjwe Senior Member

  #13
  Dec 24, 2009
  Joined: Mar 3, 2007
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kweli Kubenea kaenda mbali katika hilo la Kyela, lakini najaribu kusoma na kuelewa yaliyoko mbali zaidi ya ulichoandika naona another Kubenea wa upande wa Mwakalinga.

  Viva politiks za Tanzania!!!!!!!!!!!!!!
   
 14. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,269
  Likes Received: 22,029
  Trophy Points: 280
  jamani hivi kyela kuna nini?
  mbona kuna majimbo mengi sana ya uchaguzi hayaongelewi?
  kila kukicha ni kyela, mwakipesile na mwakalinga
   
 15. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  EEH!
  ndaga nungwe!
   
 16. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #16
  Dec 24, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  huyu sio tu ni upande wa mwakalinga, ndiye mwakalinga haswaaaaa
  soma hapa najua ni msomaji wa JF na kwa vyovyote unajua anayeongelewa kuhusu siasa za Kyela ni Mwakalinga mwana JF. Umeshindwa nini kuniuliza mimi Mwakalinga aka Mtanzania kujua ukweli?
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Dec 24, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyu Mwakalinga tulisha muonya wapambe alio kuwa anawatumia ndio walikuwa wapotoshaji wakuu maana kabla hajaenda hata Kyela ilisha fahamika Mwakalinga yupo Kyela mara yupo Arusha wapambe tu ndio walio kuwa wana report yawezekana jamaa katumia data zile za wapambe wa Mwakalinga. Wakuwalaumu ni hawa wapambe walizidisha mno nuksi na kama hawajapata laptop basi itakuwa balaaaaa kabla ya uchaguzi watamwaga sana sumu.
   
 18. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #18
  Dec 24, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  mkuu fidel inawezekana kabisa hao wapambe unaowazungumzia wakawa sio wa kambi ya mwakalinga ila wakawa ni wa kumharibia na njia waliyotumia ni pamoja na kutoa habari za uongo na kupotosha nia ikiwa ni kumchafua mtu.
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Dec 24, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Njaa kali, njaa kitu kibaya jamani hasa kwa n'tu maskini unauza haki yako hivi hivi na kuongea uongo.
   
 20. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #20
  Dec 24, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Well kama kawaida yetu, huwa tunataka kwanza kusikia toka upande wa pili yaani hapa umebaki upande wa Kubenea, sasa yeye aliwahi kusema hapa upanga ni kwa upanga, ajitokeze ili tujue ukweli ulipo!

  - Ingawa sio siri kwamba baadhi ya habari zake katika hii article, knowing Mwakalinga as I do zina walakini, lakini bado tutnampa the benefit of the doubt kama demokrasia inavyotaka, sasa ajitokeze tuone jinsi upanga kwa upanga, kama kweli ni theory of the truth au ni majungu at best!

  Respect.


  FMEs!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...