Kitunga Kitunga
Member
- Oct 16, 2015
- 14
- 13
Lowassa siyo mtu sahihi kuwa CDM? umerogwa? Nani mwenye chama? Nani alijiunga na chama siku ya kwanza, ya pili akawa mgombea urais na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama?Hata mkileta maelezo marefu vipi, Lowassa bado sio mtu sahihi kuwepo cdm. Anaweza kurudi tu ccm na kutoa huo ushauri wake mzuri akiwa huko. Ama anaweza kwenda hata TLP na kuongeza nguvu huko na hizo siasa zake. Watavuna watu wengi tu tunaombiwa walimpa kura mpaka cdm ikapata wabunge wengi.
Mbona bado mjajua kilichopo Chadema ....subiri kitifuke ....Kwa wasiofahamu tu ni kwamba Lowasa na Kubenea wana ukaribu wa miaka mingi hivyo inawezekana kabisa anachoongea kina baraka zake
Usidhani ccm kuko salama sana.. Subiri muda utaongeaMbona bado mjajua kilichopo Chadema ....subiri kitifuke ....
Ulipo tupo!Nakubaliana na hoja za Kubenea.
SawaUlipo tupo!
[emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji106] [emoji106] [emoji106]Saed Kubenea
HATUA ya Edward Lowassa, waziri mkuu mstaafu na mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa 2015 ya kukutana na Rais John Magufuli, imezusha taharuki ndani na nje ya chama chake.
Kinacholeta taharuki, ni kauli zake kuhusiana na utawala wa Magufuli. Binafsi, nimewasikiliza wote.
Hata hivyo, naomba niseme machache.
Kati ya mwaka 1995 hadi 2010, Zanzibar ilikumbwa na mkwamo mkubwa wa kisiasa.
Ndani ya visiwa hivyo, uhasama ulitalamaki. Fitina na maonevu mengine lukuki - yalikuwa yameshamiri.
Jemedari la kisiasa Visiwani, Maalim Seif Sharif Hamad, aliamua kukutana na hasimu wake mkuu kisiasa, Rais Amani Abeid Karume.
Mkutano kati ya Seif na Karume, ulifanyika wakati mamia ya wananchi wa Pemba wakiwa ukimbizini nje ya nchi.
Aidha, wakati Maalim anakutana na Karume, makumi ya akina mama walikuwa wamebakwa na kulawitiwa na watu wengine kadhaa walikuwa wamefunguliwa kesi za jinai mahakamani.
Si hivyo tu: Mamia ya wananchi, hasa wafuasi wa CUF walikuwa wamefutwa kazi serikalini.
Wengine kadhaa, wakiharibiwa mali zao, yakiwamo majumba, mashamba na baadhi wakiwa wameachwa wajane kutokana na mateso waliyopata wenza wao.
Maalim alikutana na Karume kimya kimya na bila kushirikisha wenzake kwenye chama.
Alikutana na kuzungumza na Karume na kukataa katakata kutaja kile walichojaliana.
Ilidaiwa kuwa Maalim alichukua hatua hiyo kwa kuwa alihofia kuwa kueleza mapema kile walichojadili; na au wanachokwenda kujadiliana, kungevuruga mikakati yake.
Hata Rais Karume naye hakueleza kuwapo mkutano na Maalim Seif. Hakueleza walichotaka kukizungumza na wala hakusema kile walichokijadili baada ya mkutano wao.
Mkutano kati ya viongozi hawa wawili ulifanyika wakati tayari vyama vya CUF na CCM, vikiwa vimefunga miafaka mitatu ya kisiasa bila mavuno kwa CUF.
Mwasisi wa mazungumzo kati ya Karume na Seif, ni mzee Nassoro Moyo, Eddy Lyami na Mansour Hamid.
Baada ya taarifa za kuwapo mkutano huo kuvuja, wafuasi wa CUF walikuja juu. Walimtukana Maalim Seif matusi ya nguoni.
Nakumbuka katika mkutano mmoja wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kibandamaiti, wafusi wa chama hicho, walimtupia mawe na maganda ya machungwa kiongozi wao huyo.
Kuna mengi ya kueleza juu ya tukio hilo. Lakini itoshe tu kusema, mkutano kati ya Maalim na Karume ndio uliozaa Katiba mpya ya Zanzibar na ndio msingi wa CUF kuingia serikalini katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Hivyo basi, naifananisha ziara ya Lowassa ya jana na tukio hilo la mwaka 2010 Visiwani.
Lowassa amekutana na Magufuli, kipindi ambacho chama chake kiko kwenye mkwamo. Hakiwezi kufanya mkutano wa hadhara.
Kimefika mbali zaidi; sasa hata uchaguzi mdogo hakiwezi kushiriki.
Baadhi ya viongozi wakuu chama badala ya kuwaongoza wanachama, nao wamegeuka kuwa walalamishi.
Ni kwa sababu, CHADEMA ya mwaka 2010 hadi 2014 ya maandamano na mikutano haipo tena.
Katika muktadha huo, njia pekee ya kutoka hapa tulipo ni kujadiliana adui yako. Lowassa amefungua njia hiyo. Ni vema ikatumiwa.
Mwisho
seif alipokutana na shein hakujitokeza hadharani kumsifu shein hata sikunmoja,walifanya mazungumzo kimya kiimya hadi walipotangaza muafaka,huyunwenu kaongea siku moja tu na kumpa sifa jpm kibaoSaed Kubenea

Tuonyeshe mikataba wa manunuzi maana kununua chama si mchezo. Sasa akirudi CCM ataondoka nacho?Kubenea ni takataka tu chadema ni ya Lowassa alinunua pesa nyingi
Hoja iko hapa anayosema Kubenea anahisi hana HAKIKA Maana kama ameenda kwa issue ya Muafaka kwa Vyoyote Viongozi wa Chadema wangejua na hata change kuongea kwenye Press wangekijua Lkn kusema eti alienda kama Maalim SeifLowassa inawezekana hakwenda Ikulu Kama Mwana Chadema au Mwanasiasa kaenda kuzungumza ya Mkwewe Sioi maana Pamela Kawa Kama Mjane Mwaka wa pili huu anakumbatia Mto usiku peke yake
Usisahau demokrasia ni kukubali katika kutofautiana fikra .kumpinga Mbowe,Kubenea au Lowasa ni uditecta uchwaraKwahiyo unadhani Lowasa kaenda kuongea na Magufuli kuhusu Serikali ya Kitaifa au Magufuli aruhusu siasa shindani za kukosoana?
Hahaha.... Poor you.
Nyie ndio umtaiua CDM chama gani hakitaki fikra au mbinu mpya .mwanachama akachangia wazo likajadiliwa .CDM imekuwa kama ccm sasa au !!???Anataka afukuzwe ili agome
Kufukuzika moto uwake Kama NCCR ya Miaka ile
Ulipo tupo vs Bavicha
Wanamtandao wanataka kuteka Chadema baada ya kushindwa huko CCM
Mbona kuna kauli ya Kikwete akikiri kujui kukutana huko baada ya kukutana huko kwa Karume na Seifu .usiongee kitu bila utafiti kwanza [emoji12] [emoji12] [emoji12]
The remaining part of the story sina interest nayo, mi naangazia hayo maneno yenye rangi nyekundu
Sitaki kuamini kuwa CCM, Usalama wa taifa hadi Jakaya walikuwa hawajui
Kama ni kweli basi hiyo ni hatari kubwa sana