Kubenea: Kuhamisha stendi ya Ubungo ni ufisadi

Kubenea: Kuhamisha stendi ya Ubungo ni ufisadi

Msulunje

Member
Joined
Oct 6, 2015
Posts
67
Reaction score
35
Ubungo-stand-620x308.png


MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea, amesema anatarajia kupeleka hoja binafsi bungeni ili kuzuia kuhamishwa kituo cha mabasi yaendayo mikoani (UBT).

Kwani kwa kuhamisha kituo hicho ni matumizi mabaya ya fedha za wananchi, Kubeana alitoa kauli hiyo alipofanya ziara katika jimbo hilo, ikiwamo kuwashukuru wananchi kwa kumchagua, kukagua hali ya usafi katika masoko, ikiwamo stendi hiyo ya UBT pamoja na kusikiliza kerombalimbali za wananchi.Alisema ni vema stendi hiyo ikaendelea kuwapo katika eneo hilo, kwa kuwa itasaidia katika kutengeneza biashara nzuri kutokana na kujengwa kwa mradi huo wa mabasi yaendayo haraka(Dart).

Uwepo wa daraja la mabasi yaendayo kwa kasi hapa eneo la Ubungo ni ushahidi kuwa stendi hii ilikuwa inahitajika hapa, hatuwezi kujenga miundo mbinu yote hii kwa pesa za wananchi halafu tukahamisha, hayo ni matumizi mabaya ya pesa za wananchi? alisema Kubenea.

Kadhalika, Kubenea alikagua hali ya usafi na katika eneo hilo la ubungo ikiwa ni pamoja na kukagua katika vyoo , huku akionekana kukerwa na uchafu katika vyoo hivyo.

Kubenea ambaye ni Mbunge wa pili kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kushika jimbo hilo, baada ya kushikiliwa na John Mnyika kwa miaka mitano, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Kibamba, alisema atafanya kazi kufa na kupona ili kuhakikisha kero zote zinatatuliwa.

Aidha, Kubenea ameanza kutekeleza ahadi zake alizoahidi katika kipindi cha kampeni kwa kuanza kuchimba kisima cha maji katika soko la Mabibo kwa garama zake mwenyewe na kuagiza uongozi wa soko hilo kuongea na mawakala wanaohusika na uchimbaji wa visima ili kazi hiyo ianze mara moja.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko la mabibo, Yusuph Kirema alimshukuru Kubenea kwa kuwtembelea na kujua kero mbalimbali, hivyo watampa ushirikiano kwa maendeleo ya wananchi kwenye eneo hilo.
 
ASITULETEE siasa stendi inahamishiwa boko mashamba ya dawasco kuondoa msongamano
 

Kwanza yeye ni nani mpaka azuie stendi isihamishwe?

 
Hiyo iwe standi ya daladala tu. simu 2000 iwe ya daladala za kwenda Bagamoyo
 
ASITULETEE siasa stendi inahamishiwa boko mashamba ya dawasco kuondoa msongamano

Huyu naye kweli kaishaanza siasa, nahisi anatumiwa na wafanyabiashara, stendi ya ubungo inaleta msongamano sana pale, ni bora ihamishwa
 
Hilo eneo ni gareji ya UDA sasa tumeshafufua shirika letu inabidi wapishe gereji irudi hayo mabasi ya mwendokasi yatatengenezewa wapi? Naona anataka kupata 200 za kungilia stendi tu hana lolote.
 
Ww chizi. Tangu lini stand ya mabasi ikawekwa nje ya mji... Tena stand inatakiwa iwepo kariako Au mnaz mmoja.. Ndio city centre.. Au jangwani.. Uwezi kutoa watu mikoa alafu unawashusha boko.. Unasema unaondoa msongamano...tembea huone.. Nenda southafrica.. Pale Johannesburg.. Stand chini tran, mabasi makubwa yote underground.. Na juu ndio hiace.. Na hizo nyingine za abiria.. Mtu akishuka anaweza kwenda kokote... Tatizo miundo mbinu mbovu...naunga Mkono kubenea... Pale pale Ubungo wangeweka underground.. Ingekua poa.....
 
Abiria akitoka miji mikubwa kama.. Nairobi.. Kampala, lusaka "Malawi.. Uwashushe boko.. Basi hamisha pia uwanja wa ndege pale,, upelekwe chalinze ndio akuna msongamano.. Tatizo ni miundo mbinu tu.......
 
unaweza kukuta watu wana ng'ang'ania kuhamisha hiyo stendi kumbe tayari watu wameshapiga dili. tatizo serikalini kila mpango ni dili...m
 
Standi ipelekwe Kibaha...
ni kwa vile hajui tunavoteseka kupishana na mabasi hapo mataa
Acha ushamba wewe, foleni itaisha kwa kuimarisha miundombinu na sio kuhamisha stendi. Pale inatakiwa kujengwa BYPASS ya kuingiza na kutoa mabasi stendi juu kwa juu bila kukutana na madaladala yenu. Magufuli aanze na elimu kukomboa watu kama wewe
 
Kila siku story za kuhama wakati mnapohamia hakuna ht tofali moja lililoezekwa hamjiulizi kwa nini? Watu washafanya yao mjini hapa.... Masabuni angekua mbunge angelifunika hilo kombe maana hiyo dili aliinyuka yeye
 
Back
Top Bottom