Kukubaliana na huyu ndumilakuwili kwa sababu tu Union Station ya DC iko katikati ya mji ni kuonyesha udhaifu wa kiwango chako cha upeo wa kufikiri. Tembelea pale kwa mara nyengine (kama ulishawahi kabla) uone miundo mbinu iliyoandaliwa wakati wa kukijenga kituo kile. Ni upuuzi kabisa kufikiria kwamba kituo cha ubungo kibaki pale kilipo eti tu kwa sababu vituo kama hivyo vilivyo DC, NY, London, Geneva, Oslo, San Diego, Cape Town na kwengineko viko katikati ya mji. Ni kweli viko katikati ya majiji hayo lakini bado mandhari ya majiji hayo yanapendeza na miongoni mwa vituo ukipita kwa nje hasa kama wewe ni mgeni huwezi kujua kwamba structure unayoiona ni kutuo cha basi/treni/subway.