Kubenea ampa onyo kali Nape

Kubenea ampa onyo kali Nape

Kwa hiyo tusiseme kuwa CUF kule huku ZNZ imeshinda uchaguzi qwa urais uliopita!!!!!!!!!!!!!

Serikali inataka kutufumba midomo ili suala hili lipite, tunaweza kushangaa miaka mitano ikapita kila siku tutaambiwa kuwa viongozi wapo katika kikao cha usuluhishi hadi miaka mitano itaisha tunaingia katika uchaguzi tena.

haiwezekani hili jambo liwe na mwisho wake.

kutufunga midomo isiwe ndio njia sahihi ya kumaliza tatizo la ZNZ.
 
Napinga Mawio kufungiwa
lakini naamini Mawio wana upungufu mkubwa wa maadili

Kubenea ni vizuri akajitazama na kujitathimini
ana make headlines for all the wrong reasons....

Mara vyeti vyake vimefanyaje
mara Zitto waparurane
mara yuko katikati ya uchaguzi wa Meya
mara hili.....

wapiga kura wake wanamtazama tu....wasije kumchoka so fast
Ndio upambanaji huo!!
 
Anazungumzia mikakati ya Ccj.pole sana Kubenea kwa kutumika na kubwagwa.
 
Nimekubali kweli ww ni ALWATAN KIZIGO hata Kessy wa Nkasi ni Bora kuliko kubenea???
Mzee ali kessy ni si bora tu kwa kubenea bali bora kwa wabunge wengi tu wa bunge la jamhuri.
Nahili ninalo kuambia nina ushidi nao moja ktk jimbo lililokuwa hoi kimaendeleo ni nkasi.
Lakini leo hii chini ya mbunge kesy jimbo la nkasi linapiga hatua ktk kila nyanja.
Na kama huamini mtafute Ngeleja umulize ubora wa kessy anamjua vizuri sana hasa pale ngeleja alipo kuwa waziri wa nishati.
Kubenea unaweza ukamfananisha na Mbwiga wa mbwiguke wa clauds fm....
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali
Halisi Publishers, Saed Kubenea
pamoja na Mwenyekiti wa
Jukwaa la Wahariri Tanzania
(TEF) Absalom Kibanda
wameionya serikali juu ya
uamuzi wa kulifuta gazeti la
MAWIO uliochukuliwa hivi
karibuni.
Kupitia tangazo la serikali lenye
notisi namba 55, serikali
ilichukua uamuzi wa kulifungia
MAWIO, Januari 15, 2016 huku
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
akisema gazeti hilo limekuwa
‘sugu’ kwa uchochezi tangu
2013.
Kubenea na Kibanda walikuwa
katika kituo cha Polisi cha Kati
ambapo ndiyo Makao Makuu ya
Kanda Maalum ya Dar es Salaam
wakiwasindikiza wahariri Jabir
Idrissa na Simon Mkina
walioitikia wito wa uliotolewa na
jeshi hilo siku tatu zilizopita.
Kibanda amewambia
wanahabari kuwa kitendo cha
jeshi la polisi kuwasaka ili
kuwakamata Jabir na Mkina
ambao ni wahariri ili kuwahoji
huku gazeti la MAWIO likiwa
limefungiwa, kinalenga
kuwatisha waandishi wa habari
nchini na kuzima uhuru wa
habari.
Ameulezea uamuzi huo wa
Waziri mwenye dhamana ya
masuala ya Habari, Nape, kama
uamuzi uliolishitua TEF na
wamewasiliana naye wakielezea
mshituko na masikitiko yao.
“Hatuwezi kuvumilia kufungiwa
kwa vyombo vya habari,
kukamatwa na kunyanyaswa
kwa waandishi, miaka miwili
iliyopita nilitakiwa kujisalimisha
makao makuu ya polisi,
nikafikishwa mahakamani na
nikashinda kesi, naelewa
maumivu ya mapambano haya,”
ameeleza Kibanda.
Kwa upande wake Kubenea,
amesema Serikali kupitia Nape
imechukua uamuzi wa kikatili
dhidi ya gazeti la MAWIO ili
kuzima sauti ya wananchi kwa
hoja zisizo na mashiko ikiwemo
ile ya uchochezi ambayo
imekuwa kisingizio cha
watawala kwa muda mrefu.
“Katika toleo la MAWIO lilimnukuu
Maalim Seif akijitangaza mshindi,
yeye hakuitwa mchochezi, Jecha
amefuta uchaguzi wakati hana
mamlaka ya kisheria wala ya
kikatiba hakuitwa mchochezi ila
gazeti kuandika ushindi
uliotangazwa na Seif
limefungiwa,” ameeleza Kubenea.
Kubenea ameongeza kuwa,
ubovu wa sheria ya magazeti ya
mwaka 1976 umekuwa
ukitumiwa na serikali kuviadhibu
vyombo vya habari vinavyofichua
maovu, huku mahakama
ikithibitisha mara kadhaa kuwa
madai ya uchochezi
yanayotolewa na serikali hayana
mashiko.
“Jabir ni Mwandishi aliyebobea
kitaaluma na uzoefu, ameandikia
magazeti ya Uhuru, Mzalendo,
Majira na New Habari huko kote
hakuitwa mchochezi wala
hakukamatwa.
“Nape alikuwa mmoja wa
waandishi na vyanzo vya taarifa
za MwanaHALISI kipindi hana
madaraka CCM, mbona
alishirikiana na sisi kuibua
maovu kama sisi ni
wachochezi?” alihoji Kubenea.
Jabir na Mkina wamekuwa
wakitafutwa na jeshi la polisi
kwa siku tatu mfululizo tangu
Jumamosi kwa tuhuma za
uchochezi huku jaribio la
kuwakamata likishindikana mara
kwa mara kutokana na kutojua
walipo mpaka walipoamua
kujisalimisha jana.
Mbali ya Kubenea na Kibanda,
walisindikizwa pia na Mhariri
Mtendaji wa gazeti la
MwanaHALISI, Ansbert Ngurumo
pamoja na wakili wao, Fredrick
Kihwelo.
Hapa onyo liko wapi?
Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers, Saed Kubenea pamoja na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) Absalom Kibanda wameionya serikali juu ya uamuzi wa kulifuta gazeti la MAWIO uliochukuliwa hivi karibuni.

Kupitia tangazo la serikali lenye notisi namba 55, serikali ilichukua uamuzi wa kulifungia MAWIO, Januari 15, 2016 huku Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape gazeti hilo limekuwa ‘sugu’ kwa uchochezi tangu 2013.

Kubenea na Kibanda walikuwa katika kituo cha Polisi cha Kati ambapo ndiyo Makao Makuu ya Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakiwasindikiza wahariri Jabir Idrissa na Simon Mkina walioitikia wito wa uliotolewa na jeshi hilo siku tatu zilizopita.

Kibanda amewambia wanahabari kuwa kitendo cha jeshi la polisi kuwasaka ili kuwakamata Jabir na Mkina ambao ni wahariri ili kuwahoji huku gazeti la MAWIO likiwa limefungiwa, kinalenga kuwatisha waandishi wa habari nchini na kuzima uhuru wa habari.

Ameulezea uamuzi huo wa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Habari, Nape, kama uamuzi uliolishitua TEF na wamewasiliana naye wakielezea mshituko na masikitiko yao.

“Hatuwezi kuvumilia kufungiwa kwa vyombo vya habari, kukamatwa na kunyanyaswa kwa waandishi, miaka miwili iliyopita nilitakiwa kujisalimisha makao makuu ya polisi, nikafikishwa mahakamani na nikashinda kesi, naelewa maumivu ya mapambano haya,” ameeleza Kibanda.

Kwa upande wake Kubenea, amesema Serikali kupitia Nape imechukua uamuzi wa kikatili dhidi ya gazeti la MAWIO ili kuzima sauti ya wananchi kwa hoja zisizo na mashiko ikiwemo ile ya uchochezi ambayo imekuwa kisingizio cha watawala kwa muda mrefu.

“Katika toleo la MAWIO lilimnukuu Maalim Seif akijitangaza mshindi, yeye hakuitwa mchochezi, Jecha amefuta uchaguzi wakati hana mamlaka ya kisheria wala ya kikatiba hakuitwa mchochezi ila gazeti kuandika ushindi uliotangazwa na Seif limefungiwa,” ameeleza Kubenea.

Kubenea ameongeza kuwa, ubovu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 umekuwa ukitumiwa na serikali kuviadhibu vyombo vya habari vinavyofichua maovu, huku mahakama ikithibitisha mara kadhaa kuwa madai ya uchochezi yanayotolewa na serikali hayana mashiko.

“Jabir ni Mwandishi aliyebobea kitaaluma na uzoefu, ameandikia magazeti ya Uhuru, Mzalendo, Majira na New Habari huko kote hakuitwa mchochezi wala hakukamatwa.

“Nape alikuwa mmoja wa waandishi na vyanzo vya taarifa za MwanaHALISI kipindi hana madaraka CCM, mbona alishirikiana na sisi kuibua maovu kama sisi ni wachochezi?” alihoji Kubenea.

Jabir na Mkina wamekuwa wakitafutwa na jeshi la polisi kwa siku tatu mfululizo tangu Jumamosi kwa tuhuma za uchochezi huku jaribio la kuwakamata likishindikana mara kwa mara kutokana na kutojua walipo mpaka walipoamua kujisalimisha jana.

Mbali ya Kubenea na Kibanda, walisindikizwa pia na Mhariri Mtendaji wa gazeti la MwanaHALISI, Ansbert Ngurumo pamoja na wakili wao, Fredrick Kihwelo.

- Kubenea anatapa tapa na hela za kutumiwa, anachotakiwa kuelewa ni kwamba sasa kuna Serikali mpya kwanza atafungiwa magazeti yake and next atafungwa yeye mwenyewe, akitaka kuendelea kuwa muandishi wa habari aandike kama magazeti mengine ule uandishi wake wa kutumiwa na kuvuta pesa sasa basi, halafu ajue kwamba hata hao wanaomtuma soon na wao wataionja joto ya jiwe. Kunenea hawezi kumpa onyo Waziri wa Serikali ya jamhuri angekuwa na huo uwezo asingefungiwa maisha hilo gazeti lake la kiudaku daku!!

le Mutuz
 
''Katika toleo la MAWIO lilimnukuu Maalim Seif akijitangaza mshindi, yeye hakuitwa mchochezi, Jecha amefuta uchaguzi wakati hana mamlaka ya kisheria wala ya kikatiba hakuitwa mchochezi''

Maalim Seif kujitangazia ushindi tena kwa takwimu haikuwa busara.naJecha akaamua kuuchinjia baharini uchaguzi..nalo hili sasa linaleta mgogoro mkubwa. Mawio kuwa kipaza sauti cha Seif ni shida.
Huu mkwamo bila busara kutumika utaleta balaa.Moto wake ni kama unaanza kuichoma Zanzibar.
 
Mbona wafuasi wa ccm waliobeba bango la ubaguz wa rangi huko Zanzibar hawakukamatwa? Jeshi la polisi wajitazame upya wafanye kazi kwa manufaa ya nchi sio ya ccm
 
Ndio shida yao ma std iv.
Wewe mwenye PhD umewafanyia mini waliokuzunguka cha kukumbukwa? Afadhali yeye Kubenea Ana watu anaowawakilisha kwa hiyo elimu yake, wewe je? Mwapenda sana kuwa- underate wengine kwa hivyo vijielimu vyenu vya kuungaunga.
Binafsi Kubenea ni rolemodal wa watu wengi kwani ana uthubutu wa kumiliki gazeti na kuwa mbunge. Siyo kupe. Hongera Said Kubenea na puuza wanaojifanya wana akili nyingi na PhD zao za kununua.
 
Wew
Kubenea anatumika vibaya sana, kipindi hicho kubenea alikuwa anatumiwa na nape kumchafua lowassa kwa muda wa miaka 8, leo kubenea katemwa kama big G analalamika. Ila tatizo la kubenea ni shule, anaruka ruka tu lakn elimu hakuna kumkichwa
Wewe mwenye shule kubwa imekusaidiaje na au imeisaidiaje jamii inayokuzunguka au familia yako? Mnaringia kuwa na shule kubwa ilihali haikusaidii. Fikirini kabla ya kubonyeza keypads.
 
Una uhakika hayo unayosema (ya kupewa ONYO) hayajafanywa na serikali? Notisi kibao zimesomwa za kutolewa kwa onyo...lakini Mawio ndio kwanza waliendelea kuandika habari zisizokuwa na maadili na zilizojaa uzushi.
kwanini msiwaburuze mahakamani , badala ya kutumia hizi sheria kandamizi zinazosababisha mnyimwe misaada na wazungu mpaka mnakosa dawa hospitalini ?
 
Serikali ijitazame kuhusu sheria ya kufungia magazeti maana inatumia udhaifu uliopo kisheria kwa kulipa visasi vya kipindi cha kampeni hiyo haipendezi nimeanza kuichukia Serikali hii ya awamu hii
 
kwanini msiwaburuze mahakamani , badala ya kutumia hizi sheria kandamizi zinazosababisha mnyimwe misaada na wazungu mpaka mnakosa dawa hospitalini ?
Subiri UKAWA ipate dola ifanye hiyo kazi ya kuburuzana Mahakamani...CCM tuna namna yetu ya kufanya mambo...Hapa kazi Tu.
 
Ukanjanja wa uandishi wa habari unahalalisha kabisa umuhimu wa kuundwa kwa mamlaka itakayo regulate sekta nzima ya habari, yenye kufanana na mamlaka nyingine mfano EWURA na SUMATRA. Mamlaka itaweza kutoa muongozo wa maadili ya vyombo vyote vya habari, na hili jambo linawezekana wala sio ndoto. Ikiwa Waingereza ambao walitutawala wanayo mamlaka ya habari kwanini sisi tushindwe kuwa nayo. Lazima ziwepo standards zinazofahamika kwa wadau wote wa sekta ya habari, ili mambo yasiendelee kujiendea hovyo tu. Wanaofaidika na kutokuwepo kwa mamlaka watalipinga hili wazo lakini siku zote dawa chungu ndio unayomponya mtoto upesi zaidi.
 
Ukanjanja wa uandishi wa habari unahalalisha kabisa umuhimu wa kuundwa kwa mamlaka itakayo regulate sekta nzima ya habari, yenye kufanana na mamlaka nyingine mfano EWURA na SUMATRA. Mamlaka itaweza kutoa muongozo wa maadili ya vyombo vyote vya habari, na hili jambo linawezekana wala sio ndoto. Ikiwa Waingereza ambao walitutawala wanayo mamlaka ya habari kwanini sisi tushindwe kuwa nayo. Lazima ziwepo standards zinazofahamika kwa wadau wote wa sekta ya habari, ili mambo yasiendelee kujiendea hovyo tu. Wanaofaidika na kutokuwepo kwa mamlaka watalipinga hili wazo lakini siku zote dawa chungu ndio unayomponya mtoto upesi zaidi.
 
Napinga Mawio kufungiwa
lakini naamini Mawio wana upungufu mkubwa wa maadili

Kubenea ni vizuri akajitazama na kujitathimini
ana make headlines for all the wrong reasons....

Mara vyeti vyake vimefanyaje
mara Zitto waparurane
mara yuko katikati ya uchaguzi wa Meya
mara hili.....

wapiga kura wake wanamtazama tu....wasije kumchoka so fast
Ninafuraha Dana kuona hili gazeti limefungiwa,tena wangelifuta kabisa
 
Napinga Mawio kufungiwa
lakini naamini Mawio wana upungufu mkubwa wa maadili

Kubenea ni vizuri akajitazama na kujitathimini
ana make headlines for all the wrong reasons....

Mara vyeti vyake vimefanyaje
mara Zitto waparurane
mara yuko katikati ya uchaguzi wa Meya
mara hili.....

wapiga kura wake wanamtazama tu....wasije kumchoka so fast

Maadili maana yake ni nini kwako wewe?
 
Ni wakati wa Kubenea kujikita kwenye ubunge kuwakilisha wapiga kura wake waliomchagua kwenda bungeni
Ni vema wanaogombea Ubunge wawe wanafanyiwa Interview vigezo maalumu viwekwe ili wapelekwe kwa wananchi kuchaguliwa wale tu watakaofaulu kwa kigezo cha kudadavua wajibu wao kama wabunge otherwise tutapoteza miaka 5 watu wako kuhangaika na makesi as Pesa wanazolipwa miposho haitoki CHADEMA bali ni kodi zetu wananchi. What a waste!?!?!?!
 
Back
Top Bottom