kabanga
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 37,506
- 18,872
Kisa kizuri, kinatufundisha uvumilivu...
Niwape experience ya mwanaume mmoja ambaye anakaa Dar ila alioa mwanamke wa Mbeya. Kilichotokea ni kwamba walipooana kwa ndoa mke hakutaka kumhudumia mumewe kabisaa hadi ukatimia mwaka! Mume aliafanya kila jitihada akashindwa. Lakini hakumbaka!Kwa hiyo alifanyaje? Mwaka ulipoisha bila mkewe kumpa keki,jamaa akamwambia mkewe waende Mbeya kuwasalimia wazazi (yaani wakwe wa mwanaume) huku mume akiwa na shangwe kabisa. Mke kafurahi huyo usipime! Safari ikapangwa kisha muda ukafika haoo...Mbeya kwa wazazi wa mke. Walipofika walikaribishwa kwa shangwe wakapewa huduma zote anazostahili mgeni. Hatimaye ukafika wakati wa kuharibu hali ya hewa! Mume akawaambia wakwe kuwa ana maongezi nao. Wakakaa mkao wa kula! Mume akapasua live kuhusu hali ya ndoa yake na mkewe na kwamba amechoka kabisa na kwamba amekuja kumrudisha mkewe kwa wazazi wake kisha arudi Dar akaangalie maisha yake ya baadaye bila mke! Du! Jambo hilo likawashtua sana wazazi! Basi wazazi wakamuuliza binti yao kama yaliyosemwa na mumewe ni kweli akakiri kwa aibu. Ndipo Mama yake akaagizwa akae naye chemba amuhoji sababu ni nini
akakaa naye lakini ikaonekana hana la maana. Kwa kweli walimlaumu sana kwamba amewatia aibu sana. Wakamwamuru amwombe mumewe msamaha akafanya hivyo. Pia wakwe wakamwombea masamaha na kumwomba mume aondoke naye. Lakini mume akakaza uzi kuwa hawezi kuondoka naye! Wakambembeleza huku mama na binti wakiwa wanalia lakini wapi
jamaa hataki kubadili msimamo! Walipombana sana akadai hana nauli ya kutosha watu wawili. Wakwe wakasema hilo sio tatizo nauli watatafuta. Hapo mume hakuwa na hoja tena ila kukubali yaishe! Ndivyo walivyomaliza hicho kizaazaa. Basi mume akarudi Dar na mkewe,mke akaachia asali kwa mara ya kwanza! Ndani ya mwaka mmoja
wakapata mtoto! Mpaka sasa ni mke mume na wana watoto kadhaa!!
Kwa hiyo kama huyo jamaa anaweza kuiga
mfano huu sijui. Nawasilisha.