Kubadili majina baada ya kuolewa

Kubadili majina baada ya kuolewa

Graca Machel alikuwa mke wa rais wa Mozambique, Samora Machel. Aliolewa na Madiba baada ya mumewe kufariki.
Ndo shida hiyo ya kubadili jina anaishi na mme mwingine anatumia jina la mwingine
akuuuuuu baba ni mmoja wame ni wengi
 
Mi niliongezea jina lake la ukoo, yani natumia jina langu la ukoo wangu kisha ukoo wake, na nafurahia hilo kwanza inanirahisishia mambo yangu mengi
 
Majina hayabadiliki kwenye vyeti ila ile aka inakua hadi kuota mizizi, mfamo lucy ....mtera anaolewa na John ..... Msadu basi kadri muda na love linavyoshamiri inabadilika na kuwa Msadu i.e lucy Msadu mke wa John Msadu.... Inaleta picha nzuri na pia kuleta utambulisho mmoja wa familia.... Sidhani kama ni mfumo dume ila ni ustaarabu wa kiafrika....Wale wenye the Hague yao waje na sera ya kusema familia ibadilishwe na kuitwa MSADUMTERA
 
Ni vizuri lknini,doh hawa wanaume wa siku hizi vigeugeu sana. Yaan unaweza kukaa nae vizuri kwa miaka ya mwanzo ikafika mahali akaanza kukubadilikia mara wanawake mara kipondondo ilimradi amekunyanyasa tuu. Siwaamini sana hawa watu jamani.

'For every action there is an equal and opposite reaction.' Mwanamume hawezi kukubadilikia tu kama huna vitabia visivyokubalika. Mimi mwenyewe siku hizi siwaamini ninyi akina dada.
 
Habari zenu wakuu,

Natamani kufanya hivyo baada ya harusi yangu na mr right wangu. Mama yangu alibadili majina baada ya kuolewa na baba na mpaka sasa bado anatumia majina ya baba.

Pia nimechunguza sana mama zetu wengi wanaitwa kwa majina ya waume wao mfano regina lowasa, Salma Kikwete na wengineo.Naona kama ni heshima sana kwa mume but sijajua madhara ya kufanya hivyo. Pia wazazi sijui watamind mimi kufanya hivyo.

Naombeni busara zenu wandugu.

Matusi hayaruhusiwi please.

Asanteni

Ungetaka kubaki na jina lako basi usingeolewa! Ndoa zina taratibu zake -faida na hasara zake. Hata Mungu alimuumba mtu mke mtu mme akawaita JINA lao ADAM (Soma Mwanzo 5:2). Wote wawili (mme na mke) walipewa jina moja ADAM na Jina la Eva lilitoka kwa Adam -kwa maana ya kuwa Adam ndiye aliyempa mkewe jina la Eva (Hawa) na siyo Mungu.

Ubakie na jina la baba yako kisha tukuite Mrs nani? Daaa!
 
Back
Top Bottom