Kuazima gari ni ustaarabu?

Cha mtu mavi mambo ya kuazima azima si ustaarabu iwe chochote.

Ulichotakiwa kufanya kama hukujisikia ni kumtosa sio unampa kisha unalalamika na kuwa na wasi pengine anaweza pata ajali na kuwaza mengi kichwani
 
hivi jirani yako akija kukuazima kitu mpaka uje kuuliza jf?!! haujatuambia ulimjibu nini (huenda ulimwongopea), ulitakiwa umpe za macho kuwa "hapana ndugu yangu, hatufahamiani sana hivyo sitakupatia, ni kwa ajili ya usalama wako na wangu pia", lakini kama ni jirani mnafahamiana baba fulani baba fulani sioni ubaya kumpa, otherwise siyo jambo la kujadili saana mpaka jf!!
 

mkuu kuna watu hawana soni wala woga kwenye mali za wengine hata kidogo!

Kwa mali kama hiyo ama yoyote ile, ni lazima kwanza uwe mwangalifu, unaweza kukuta mtu kahamia tu ajifunze mazoea na wewe, baada ya muda tu, anakwapua kila kilicho chako cha thamani.. mjini wapi? shule baba!
 
Kwani gari ina nini usiazime mwenzio? Kama kitu cha maana sana mbona ukifa huzikwi nayo?
Cha msingi
1.mufahamiane,
2.Ajue kuendesha,
3.ujue shughuli anayoenda kufanyia.
Tuache ulimbukeni ukiwa na gari ndo kujiona umemaliza.

Katika watu wenye hoja za kitoto basi Makamee unaongoza.
 
Last edited by a moderator:
Katika watu wenye hoja za kitoto basi Makamee unaongoza.

Kuna mmoja juzi kaazima gari ya rafiki yake kufika kwenye mataa red ikawaka kajifanya ana haraka kuvuka tu kagongwa ubavuni. Mbona alizimia watu wakadhani amekufa kumbe presha juu alipozinduka machozi yanamtiririka anaambiwa shukuru Mungu umepona unalia nini akajibu gari ya watu hii sijui nalipa na nini
 
Last edited by a moderator:
Uchumi wako ni wa kiwango fulani, ndiyo maana huoni tabu kumwazima fyekeo. Uchumi wako ungekuwa wa kiwango fulani kingine usingeona tabu kumwazima gari. Nakublina nawe kwamba jamaa anakosea kujaribu kwenda kinyume na hali zenu za uchumi.

Basi kaazime gari kwa Dewji, au Mengi!
 
thats brilliant mzee.......cha mtu mavi.
kwa kuongezea, hata kama ingelikuwa na wewe huna gari, hilo la kwake unaliacha hapo hapo na unapanda zako daladala.
 
amefanya la maana sana kushare, faida kubwa imepatikana kutokana na komenti za wachangiaji.
kuna wengine walitamani tu kujua mambo ya kuazimana magari na nini cha kufanya.
 
huyo
Heshimu gari baba .gari siyo kiungo mtu anazaliwa nacho.
huyo mtu wa karibu nilishawahi kumuazima gari masaa matano badae kapata nalo ajari tena akiwa amelewa...garama matengenezo ilikuwa 1.2m , wala nusu ya gharama hakuweza kuto.
ukiazimisha gari, u do it for your own risk.ushikaji ndo unatuponza waafrica.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…