Husninyo
Platinum Member
- Oct 24, 2010
- 24,342
- 10,688
heheheh!!! huyu mtoto hajazoea matango, kibamia kinamfaa.Ni kibamia tu Mwajuma...ila ngoja niende kwa Bi. Havijawa nikachanjie tango..
heheheh!!! huyu mtoto hajazoea matango, kibamia kinamfaa.Ni kibamia tu Mwajuma...ila ngoja niende kwa Bi. Havijawa nikachanjie tango..
Nimekustukia wewe... Hebu lipa deni la watu kwanza kabla hujaenda huko kusiko na networkSasa blaza... mambo ya kibinafsi tutajadili pembeni basi. Hata hivyo nlikuwa nakuaga.. naelekea Sumbawanga na kule kama unavojua hakuna 'network'.
kisura apenda urembo, namtaftia na kijora ije full package.
heheheh!!! huyu mtoto hajazoea matango, kibamia kinamfaa.
halafu unajua nasubiri binamu yake akue kue tuje tujitambulishe rasmi. lolOf course.
Tufaha huwa halidondoki mbali na mti wake!
eeeeh, tena atachekelea huyo. tango halifai atiiAlaa kumbe.
Basi ngoja nikitunze.
halafu unajua nasubiri binamu yake akue kue tuje tujitambulishe rasmi. lol
hahahahahahKheeeee!
Kumbe! Sitokaa nikusamehe.
Ulichonifanyia ni kibaya sana. Ndo nini sasa kunificha? Uncle kamaindi....ningeleta hata sippy cup!
.Nilishawahi kwenda Tanzania na kutaka kuadopt mtoto, ila process niliyokutana nayo walinikatisha tamaa.
Watoto wengi Tanzania wanahitaji kuwa adopted ila serikali imeweka sheria kali kana kwamba wanaweza kuhudumia hao watoto.
Niliambiwa kama nataka kuadopt mtoto basi natakiwa nikae Tanzania miezi 6 mfulilizo na hapo ndipo paliponishinda. Vile vile unatakiwa kuwa na nyumba Tanzania hili haina shida. Ila nikae Tz miezi 6,dahhh! Serikali mnatakiwa mbadilishe sheria. Watu tunataka kusaidia kulea watoto ila sheria zenu zinabana sana.
Napenda sana watoto,nina mtoto 1 ila sikuhitaji kuzaa tena sababu nilijua naweza saidia kulea watoto wasiokuwa na malezi bora.
Ila kwa sheria zao za Kubana itabidi nizae tu wa kwangu mwenyewe.
hahahahahah
hamna bana, nataka kuasili. lolMwajuma wewe....makonzi yanakuhusu.
hamna bana, nataka kuasili. lol
Sheria lazima ziwalinde watoto, hata kama hawana wazazi si kigezo cha kuwageuza kwenda kufanyia makafala ya damu ( simaanishi wewe kwamba ndio una nia hiyo).Nilishawahi kwenda Tanzania na kutaka kuadopt mtoto, ila process niliyokutana nayo walinikatisha tamaa.
Watoto wengi Tanzania wanahitaji kuwa adopted ila serikali imeweka sheria kali kana kwamba wanaweza kuhudumia hao watoto.
Niliambiwa kama nataka kuadopt mtoto basi natakiwa nikae Tanzania miezi 6 mfulilizo na hapo ndipo paliponishinda. Vile vile unatakiwa kuwa na nyumba Tanzania hili haina shida. Ila nikae Tz miezi 6,dahhh! Serikali mnatakiwa mbadilishe sheria. Watu tunataka kusaidia kulea watoto ila sheria zenu zinabana sana.
Napenda sana watoto,nina mtoto 1 ila sikuhitaji kuzaa tena sababu nilijua naweza saidia kulea watoto wasiokuwa na malezi bora.
Ila kwa sheria zao za Kubana itabidi nizae tu wa kwangu mwenyewe.
Sheria lazima ziwalinde watoto, hata kama hawana wazazi si kigezo cha kuwageuza kwenda kufanyia makafala ya damu ( simaanishi wewe kwamba ndio una nia hiyo).
Ila wengi hamfikilii in deeply ni kwa nini serikali inaweka sheria ngumu, ukweli ni kwamba ni vigumu kuweza kuyatambuwa malengo ya muhitaji.
Kuna watu wanawafanyia ukatili usiomithilika watoto wa kuwazaa wenyewe, na kuna wengine wanauwa Albino ili wapate utajili, sasa bila kuweka sheria kali watoto hawa wanaweza kudondokea kwenye mikono ya washirikina.
Na hiyo ndio sababu kila baada ya kipindi fulani watu wa ustawi wa jamii huja nyumbani kwako kuona maendeleo ya mtoto uliyemuasili.
Ila mimi binafsi maisha yakiniruhusu kusaidia wenye uhitaji nitachukuwa ndani ya familia maana koo zetu za Kitanzania tunajuwana tumejaa ufukara, ukiwa wewe uko njema 70% ya ndugu wako hohehahe, kwahiyo kwangu nitachukuwa mtoto wa ndugu ninayempenda nitamsaidia kulea mtoto kwa kumpa maisha yanayostahili.
we hamisi mie na umri huu niasiliwe!!Na wewe nani akuasili?
Naomba niende kwa mifano kama mwalimu ( jo sina taaluma wala kipaji cha ualimu)
Kuna dada mmoja yeye na mumewe walisikia kwenye kipindi cha radio mschana akiwa na mama yake hali ngumu huko kijijini amefaulu
kuendelea sekondari ila uwezo hakuna. Ikitokea
tuu wakaguswa wakafanya mawasiliano na radio wakampata yule mschana akahamia pale nyumbani kwao baada ya kufahamiana na familia yake pia wakaanza kumsomesha. Hivi
ninavoongea yule binti alishamaliza chuo japo
hajapata kazi ila ni huyo dada na mumewe ndo walimgharimia. Hapo katikati kama ujuavyo malezi ya Vijana aliwasumbua ila walikula nae
sahani moja kama binti yao wa kumzaa ili awe
na maadili mazuri.
Pamoja na hayo naweza sema familia hii inabahati ya kuasili watoto. Wakiwa pamoja kwenye mihanjo yao njiani wakakuta kundi la watu wanashangaa wakajumuika kujua kuna nini. Kumbe ni mtoto mchanga ametupwa na mtu asiyejulikana, walimuonea huruma na wakajitolea kumuasili. Walifatilia taratibu zote na mtoto yule akawa chini ya himaya yao. Wao wenyewe yeye na mumewe walibarikiwa watoto wa kuwaza 4 hivo ukiongeza na hao watoto 2 wa kuasili wanakuwa na familia yenye watoto 6 na si kuwa ni matairi. ... ni familia ya kawaida tuu yenye kipato cha kati.
Mfano wa pili ni huko zamani wakati niko kwetu mtaani mama mmoja aliokota mtoto usiku akiwa kwenye shughuli zake za usiku ( kujiuza) hapa nalazimika kuelezea kiundani kupunguza maswali...
Huyu mama alikuwa na mumewake na walijaaliwa watoto 2. Yule mume baadae akawa mlevi na akawa mtu wa wanawake sana na kumpiga mkewe kila arudipo. Mke yakamshinda akaomba talaka maana mume alifikia kiwango cha kutelekeza familia bila kuihudumia. Huyu mama baada ya kupata talaka yake kwakuwa alikuwa mama wa nyumbani akawa anadai matunzo ya watoto maana mumewe alikuwa ji muajiriwa hivyo alifingua kesi mahakamani. Siku ya hudumu yule baba aliwakana wale wanawe na kusema hawatambui na hatakaa awatunze. Wale watoto wakati wanakanwa mahakamani walikuwa ni wakubwa wa miaka 8 hivyo walielewa kila kitu. Mama ikabidi arudi kwao ambapo ndo mtaani kwetu kulea wanawe mwenyewe na alikuwa mama wa nyumbani. Watoto wale bila kupinga ni wa yule mumewe maana walifanana kama mapapai hata hakimu akasema atakuwa huyu bwana kalogwa si bure.......
Yule mama akili yake ikamtuma ajiuze usiku asee wanawe mwenyewe bila msaada wa baba yao. Siku ya siku akiwa kwenye windo ndo kwa mbaali akamuona mtu (hakumtambua) anatembea kwa kunyata na akaweka kitu chini kisha aka angalia huku na kule kama kuna aliyemuona alipoona hela akainuka na kutimua mbio bila kugeuka nyuma. Yule mama aliyashuhudia yote hayo akavutwa akaone pale kuna nini. Kufika ni kachanga kalikotoka kuzaliwa hata kitovu hajakatwa daah usiku ule ikabidi apigee kelele watu wachache Wakaja wakaenda polisi kutoa taarifa akapata kibali cha kwenda hospitali kisha akarudi nyumbani maana mtoto hakuwa na tatizo lolote. Akawa anaripoti kila siku kituoni polisi na yule mtoto kwa mwezi mzima huku polisi wakifanya uchunguzi kumsaka mwenye mtoto. Bila mafanikio mwisho polisi wakasema je unaweza kumlea mtoto huyu? La tumpeleke vituo vya kulelea mayatima. Ndo yule mama akasema hii ni zawadi kwa Mungu. Akasema atamchukua kama mwanawe.
Hivi niandikavyo yule mtoto yuko darasa la saba na ni mvulana mkubwa tuu maana bado wanaishi pale pale mtaani kwa wazazi wangu mie.
Pole nimeshindwa kufanya muhtahasari wa habari na pole kwa kukuchosha kusoma habari ndefu.
Nikutakie kila la kheri kwenye hilo ulilolidhamiria
Mungu akuongoze na nakuombea baraka tele.
Kasie.
we hamisi mie na umri huu niasiliwe!!
hehehe, hapo sawa, ngoja nitafte wa kuniasili sasa, nisije nikafa na utamu wangu. lolEeh ndiyo...si unakuwa baby ake na naniliu...ye unamwita dady na yeye anakuita baby.