Kuasili mtoto

Kuasili mtoto

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,503
Reaction score
145,919
Kwa muda mrefu sasa wazo la kuasili mtoto limekuwa likinivutia sana.

Limekuwa likinivutia hadi kunifanya nilifanye kuwa ndo moja ya baadhi ya azma zangu maishani.

Kwamba, ipo siku ambayo si mbali sana kutoka sasa ambapo nitauanza huo mchakato wa kuitimiza hiyo azma.

Msukumo wangu kwenye hili unatokana na ukweli kwamba mimi napenda sana watoto. Na kwa mtaji huo huwa sipendi kabisa kuona watoto wakiteseka kwa namna yoyote ile au kukosa fursa ya kuishi maisha mazuri yenye furaha tele.

Ni ada kwangu kabla sijafanya maamuzi yenye athari ya/za kuweza kudumu kwa muda mrefu, kutulia na kwenda taratibu huku nikitafakari kwa kina yaliyo chanya na hasi, changamoto zilizopo na ambazo zaweza kujitokeza mbeleni na kama naweza kukabiliana nazo bila kuyumba, na kadhalika.

Kwa ufupi, huwa napenda kufanya tathmini kamilifu halafu ndiyo naamua la kufanya.

Sasa hili la wazo la kuasili mtoto nimekuwa nalo kwa muda mrefu. Nimelijadili sana na watu wa kada mbalimbali. Na kusema ukweli majadiliano mengi yamekuwa ni ya chanya na kutia moyo.

Kwa manufaa ya uwazi kuhusu hali yangu ya kindoa, mimi ni kapera. Hali hii ndo moja ya sababu inazonifanya nikawie kufanya kweli.

Manake huwa nafikiria, unapomleta mtoto mdogo kuwa chini ya himaya yako na kumlea pasipo na mlezi wa kike, sijui hayo malezi yanaweza kuja kuathiri vipi makuzi yake. Hilo ndo moja ya changamoto za mbeleni nilizozigusia hapo juu.

Lakini ima fa ima, ipo siku tu nitafanya kweli. Nisipofanya kweli nitajiona kuna kitu kimepungua katika uwepo wa uhai wangu hapa duniani. Na sitaki kuwa na hiyo hali maana itanisumbua kwa kiasi chake. Huwa sipendi kushindwa kutimiza malengo yangu niliyojiwekea.

Sasa basi, kwa vile JF-MMU ni jamvi la wengi na kama wahenga walivyonena, penye wengi pana mengi. Hayo mengi ni pamoja na tajiriba mbalimbali na tofauti za kimaisha.

Na hiyo ndo sababu mahsusi ya mimi kuamua kuuleta huu mjadala hapa. Inawezekana mpo ambao mmeshawahi kuasili watoto. Kama mpo basi naomba mtupe mliyokutana nayo na mnayokumbana nayo.

Au pia huenda kukawepo na watu ambao mliasiliwa. Kama mpo na nyie fungukeni mtupe mliyoyapitia na mnayoendelea kuyapitia.

Hata kama haupo kwenye hayo makundi mawili lakini una mawaidha au mausia mawili matatu ambayo unaweza kuchangia, nasema ahlan wa sahlan.

Ni mimi wenu mtiifu,

Nyani Ngabu bin Kibadiru.
 
Kuasili mtoto ndo ile watasha wanaita...CHILD ADOPTION...au??? kama ni hiyo iweje utamani ku plagiarize kazi za wenzako???. Ushauri wangu, piga kuni upate wa kwako mkuu!!!

Wangu mbona yupo tayari.

Nataka niongeze mwingine ambaye kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake hana fursa na bahati kama aliyonayo huyu wangu.
 
Kwakweli,Hilo wazo hata mimi nimekuwa nalo kwa muda mrefu sana ila nilikatishwa tamaa sana na partner wangu.

Kwanza aliniambia kuna tabia za kurithi anaweza akawa na tabia mbaya ambayo inaweza ikaleta athari katika mahusiano yetu. Pili,mtoto huyo akishajielewa na kufahamu kuwa sisi sio wazazi wake mtazamo wake juu yetu pia unaweza ukabadilika pengine akaona he/she has nothin loose coz sisi sio ndugu zake wala wazazi wake.

Personally,nilipinga sana kwasababu naona hayo ni matokeo tu. So long as atakuwa treated kama wenzie tulionao tusiwaze sana negative outcome but mwenzangu hakulipenda sana hilo wazo.

But @ Nyani Ngabu kama hiki wazo unalo endelea nalo ..Mimi nataman mpaka kesho.
 
Wangu mbona yupo tayari.

Nataka niongeze mwingine ambaye kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake hana fursa na bahati kama aliyonayo huyu wangu.
Lol! kwa kiasi flani sababu yako ina logic, ila kama una mtoto wa kike then ukaasili dume, U will be in trouble.
 
Kwakweli,Hilo wazo hata mimi nimekuwa nalo kwa muda mrefu sana ila nilikatishwa tamaa sana na partner wangu... Kwanza aliniambia kuna tabia za kurithi anaweza akawa na tabia mbaya ambayo inaweza ikaleta athari katika mahusiano yetu. Pili,mtoto huyo akishajielewa na kufahamu kuwa sisi sio wazazi wake mtazamo wake juu yetu pia unaweza ukabadilika pengine akaona he/she has nothin loose coz sisi sio ndugu zake wala wazazi wake...
Personally,nilipinga sana kwasababu naona hayo ni matokeo tu. So long as atakuwa treated kama wenzie tulionao tusiwaze sana negative outcome but mwenzangu hakulipenda sana hilo wazo.

But @ Nyani Ngabu kama hiki wazo unalo endelea nalo ..Mimi nataman mpaka kesho.

Ahsante sana.

Hayo ya matokeo mimi wala hayanipi shida sana kwa sababu kama nikifanya hivyo, sitakuwa nafanya kwa kutegemea fadhila zake hapo baadaye.

Nikifanya nitakuwa nafanya kwa wema na kwa kiroho safi kabisa.

Akija kuamua kunigeuka hapo baadaye, hilo litakuwa lake na si langu.

Mimi nilitenda wema tu, basi.
 
Hivi kwa sheria za Tanzania, hii kitu inaruhusiwa?. Kuna mtu namfahamu alishataka kufanya kitu kama hiki lakini mlolongo aliokutana nao ilibidi anyooshe mikono!.

Kuna red tape ya kufa mtu au...?
 
Yeah, process ni ndefu kiasi kwamba, unatakiwa uwepo Tanzania kipindi kirefu kuyashughulikia hayo mambo; hii ni kama uko nje ya nchi, ili uweze kulifanikisha suala zima!. Nyani Ngabu!.
 
Jambo jema halina tatizo lolote mimi pia nia azma hiyo na umeweka wazi changamoto ya kutokuwa na mke ila kwangu sioni kama ni zuio kubwa kama unampata ambae tayari ana miaka kama miwili unaweza kukaa nae ukiwa na house girl maisha yanakwenda mpaka ukipata mwenza nae unamwambia huyo ni mtoto wako wa damu sio wa kuasili maana wanawake wetu wengi wao sio wote akili zao wanazijua wenyewe.
Maana hata akiwa wa damu wanamchukia sembuse huyo atamfanya kama ngoma kila la kheri ndugu katika kutimiza hilo.
 
Kwakweli,Hilo wazo hata mimi nimekuwa nalo kwa muda mrefu sana ila nilikatishwa tamaa sana na partner wangu... Kwanza aliniambia kuna tabia za kurithi anaweza akawa na tabia mbaya ambayo inaweza ikaleta athari katika mahusiano yetu. Pili,mtoto huyo akishajielewa na kufahamu kuwa sisi sio wazazi wake mtazamo wake juu yetu pia unaweza ukabadilika pengine akaona he/she has nothin loose coz sisi sio ndugu zake wala wazazi wake...
Personally,nilipinga sana kwasababu naona hayo ni matokeo tu. So long as atakuwa treated kama wenzie tulionao tusiwaze sana negative outcome but mwenzangu hakulipenda sana hilo wazo.

But @ Nyani Ngabu kama hiki wazo unalo endelea nalo ..Mimi nataman mpaka kesho.

Hapo red ndo nilichotaka kumwambia comrade wangu Nyani Ngabu .... Binamu yangu mmoja ambaye hakubahatika kupata mtoto wa kiume aliamua kufanya maamuzi ya kuasili. Na kama unavojua mambo yetu ya kiafrika watu walikuwa wakizungumza chini kwa chini... wengine wakimshangaa kwanini hakuamua kumchukua mtoto wa ndugu maskini ili amlee kama mwanae...

Miaka kadhaa baadae yule mtoto akajua yeye si damu ya wazazi wale. Na wale mabinti warembo aliokuwa akiwaita dada sio dada zake wa damu. Aisee...aliwapiga miti wale mabinti (dada zake) ile kinoma..... Mpaka dingi kuja kushtukia ilikuwa too late. Shughuli ndio ikaanzia hapo, dogo haeleweki na baba hana cha kufanya.

Hapa komredi anapaswa awe makini sana. Kiafrika wanaokuja kuharibu mambo ni ndugu. Ila kama ni kwa huko USA baby, yawezekana mambo yakawa tofauti.

Kiafrika, mambo ya kuasili bado hayajakaa sawa kiviile nadhani kwa sababu tushazoea mambo ya extended families. Ndugu zako maskini watamwonea wivu mtoto uliyemuasili ambaye anakula good time.

Kama alivodokeza komredi, hii ishu kiafrika inahitaji tathmini, ujasiri na uthubutu uliotukuka.
 
Back
Top Bottom