Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,503
- 145,919
- Thread starter
- #101
Haya mambo ya kuasili mtoto ni wito si wote tuliobarikiwa, lakini kwa Watanzania wenye moyo wa kuasili mtoto/watoto kuna kitu kimoja bado sikielewi kutoka kwao.
Ukimsoma vizuri mleta mada lengo lake ni kumuwezesha mtoto kupata malezi bora na yanayostahili, lakini papo hapo iwapo utajipa muda wa kumchunguza ukoo wao wapo watoto wa ndugu wanaostahili kabisa huruma yake na wazazi husika watakushukuru kwa kuwatuwa mzigo.
Hi ni free world kila mtu ana haki ya kufanya kila anachojisiki lakini hii charity ni kwa nini isianzie makwetu kwa sababu ndani ya familia zetu kuna wahitaji?
Nimekuelewa kaka lakini nadhani kuna kitu kimoja ambacho labda sikukigusia au sikukiweka wazi.
Ni hivi, pindi nitakapofanya hivyo [kuasili] basi nitachukua asiye na wazazi wala ndugu.
Wapo watoto wa hivyo.
Hao watoto wa ndugu unaowazungumzia wewe, umeshasema kabisa kuwa wana wazazi.
Sasa kama wana wazazi kwa nini mimi nijibebeshe wajibu wao? Si kila mtu awajibike na vyake, au?
Lengo langu ni kuasili mtoto yatima ambaye hajui hata ndugu zake ni akina nani.
And believe you me, that boy or girl will be the luckiest child in the world once he/she becomes my child.
I know how to take care of children.