Kuanguka kwa uchumi: Serikali inakosea wapi?

Algore

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
2,097
3,362
1. Uchumi wa Tanzania umeendelea kuzorota siku hadi siku. Na sasa maisha ya wananchi wengi yako taabani.

2. Ni nini serikali imekosea hadi hali ya uchumi wetu kuwa taabani kuliko wakati wowote tokea uhuru.

3. Wakati wa mwalimu Nyerere vitu vilikosekana laki bei haikupanda siyo kwa bidhaa hata huduma pia.

4. Raisi Mkapa alituambia tufunge mikanda akuze uchumi. Na Wote ni mashahidi baada ya muda uchumi ulikua kweli na bei za bidhaa zote zilishuka.

5. Serikali ya Mkapa itakumbukwa kwa kuondoa kodi ya kichwa, tozo za mikokoteni na baiskeli, kufuta leseni za biashara. Ujenzi wa barabara za lami, daraja la mkapa, bunge, mkapa stadium, koboresha mishahara ya wafanyakazi nk.

6. Ni nini kimewakwamisha viongozi wa serikali ya awamu ya sita? Twafa
 
Pia alipunguza sana nafasi za teuzi na kupelekea hadi kufikia u kurugenzi kufanyiwa usaili...

Alikuwa na watu ambao kweli walikuwa na capacity ya kutumia weledi kwenye nafasi zao...

Kosa lake kubwa ilikuwa kutomsikiliza Mwl JKN kuhusu privatization...Angefuata mfano wa raia kupewa kipaumbele na kupewa ujuzi wa kutengeneza mitaji, leo hii nchi yetu ingekuwa pahala pa zuri zaidi...Hasa kama waliofuata baada yake wangeendeleza yale aliyoayaanzisha yeye...
 
Kwa sasa karibu vitu vyote vinaenda kwa utashi wa viongozi na siyo kuongozwa na mifumo, so unfortunate na sisi wengi tunatafuta hisani bila kujua kuwa kama hakuna kitu cha kugawa hisani haitasaidia mtu zaidi ya kupeleka nchi yote shimoni. Maendeleo yanajengwa na kuna kanuni za kufanya hivyo ambazo hazidanganyi.
 
Kilichodumaza nchi hii hadi leo ni kuingiza siasa kwenye utendaji kulikoasisiwa toka enzi za mwalimu na kufanya wanasiasa kuwa na nguvu kupindukia... worse still wanasiasa wengi bado ni vilaza wa kujua kusoma na kuandika na wale wenye phd za mwendokasi, hapo unategemea nini?​
 
1. Uchumi wa Tanzania umeendelea kuzorota siku hadi siku. Na sasa maisha ya wananchi wengi yako taabani.

2. Ni nini serikali imekosea hadi hali ya uchumi wetu kuwa taabani kuliko wakati wowote tokea uhuru.

3. Wakati wa mwalimu Nyerere vitu vilikosekana laki bei haikupanda siyo kwa bidhaa hata huduma pia.

4. Raisi Mkapa alituambia tufunge mikanda akuze uchumi. Na Wote ni mashahidi baada ya muda uchumi ulikua kweli na bei za bidhaa zote zilishuka.

5. Serikali ya Mkapa itakumbukwa kwa kuondoa kodi ya kichwa, tozo za mikokoteni na baiskeli, kufuta leseni za biashara. Ujenzi wa barabara za lami, daraja la mkapa, bunge, mkapa stadium, koboresha mishahara ya wafanyakazi nk.

6. Ni nini kimewakwamisha viongozi wa serikali ya awamu ya sita? Twafa
Umeandika ukweli mtupu ambao watu wengi wakiwemo viongozi wanajaribu kuuficha
 
Tuelezee kidogo unakuaje ili tupate uelewa...Maisha kusaidiana!
Uchumi kuzorota maana yake ni uzalishaji kushuka na huduma kukosekana, na watu kupunguzwa kazi, viwanda na ofisi nyingi kufungwa

Vitu kupanda bei haimaanishi uchumi kushuka, kama ni hivyo basi uchumi wa nchi haujawahi kupanda maana bei ya bidhaa miaka ya 60,70,80,90, ilikuwa chini kuliko ya sasa
 
Vitu kupanda bei maana yake ninj kiuchumi kwamba vimejaa siyo kila mahali unajiokotea tu?

Ila nashukuru kwakujibu kistaarabu...Pengine na mimi nikuongezee maana ya bei...Bei ni makubaiiano ya kati ya mnunuzi na muuzaji, bei hii inategemea uwepo au ukosefu wa bidhaa husika ama kwakuwa hazijazalishwa au kwakua zimezalishwa kidogo...Sasa linganisha na notes zako kisha endelea kutuelimisha tutasaidika
 
Labda tufanye yafuatayo
1. Kuzuia mfumuko wa bei ya vyakula kwa kuwapata elimu wakulima madhara ya uuzaji wa mahindi na mchele nje

2. kudhibiti maduka ya kubadilishia fedha za kigeni maana wameanza tena kale kamchezo kao
3.Kupunguza ujenzi wa miradi mikubwa au kujenga kwa awamu

4.Serikali iweke ruzuku kwenye mafuta ya kupikia na sukari ili bei ishuke sambamba na kurekebisha mfumo wa kodi ya mapato kwenye sukari na mafuta na kodi hiyo iwe rejesho mbadala kwenye madini na uvuvi wa kibiashara na hatifungane aidha pale BOT kwasasa labda Gavana Tutuba afanye yafuatayo ...
 
Pia alipunguza sana nafasi za teuzi na kupelekea hadi kufikia u kurugenzi kufanyiwa usaili...

Alikuwa na watu ambao kweli walikuwa na capacity ya kutumia weledi kwenye nafasi zao...

Kosa lake kubwa ilikuwa kutomsikiliza Mwl JKN kuhusu privatization...Angefuata mfano wa raia kupewa kipaumbele na kupewa ujuzi wa kutengeneza mitaji, leo hii nchi yetu ingekuwa pahala pa zuri zaidi...Hasa kama waliofuata baada yake wangeendeleza yale aliyoayaanzisha yeye...
Ni nini waziri wa fedha, gavana BOT,Waziri wa mipango na uchumi etc wakati Rais Mkapa walifanya hadi uchumi kukua? Kama viongozi hawa bado wapo kwa nini serikali isiende kupata ushauri kwao? Twafaaaa!
 
Back
Top Bottom