ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,076
- 49,785
Benki ya Dunia wametoka ripoti Yao kuhusu Haki ya uchumi wa Tanzania na Maendelea ya watu
Pamoja na mambo mengine wamesifu uimara wa uchumi wa Tanzania wakisema licha ya mitikosiko ya uchumi wa Dunia Bado uko imara na wanakisia Ukuaji utakuwa 5.1% mwaka 2023 kabla ya kufikia 6% mwaka 2024.
Kuhusu Maendelea ya watu wamedai kwamba kuongezeka Kwa uwekezaji wa Serikali(Public Spending) kwenye Huduma za jamii kumepunguza umaskini zaidi kuliko Nchi zingine walizolinganisha.Na Ili kupunguza umaskini zaidi wakapendekeza Kodi ziongezwe hasa Kwa matajiri na mashirika.
View: https://www.instagram.com/p/CxfHBgIINoz/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
My Take
Binafsi napingana kabisa na dhana ya Kodi,Kodi,Kodi kwamba ndio njia ya kupunguza income inequality na kuondoa umaskini badala yake Serikali iwekeze kwenye kuongeza utajiri Kwa watu wa chini (Wealth creation).
Kwa maana ukiwabana matajiri na mashirika watashindwa kuwekeza na Kuajiri hao maskini.
Serikali msikubali huo Ushauri badala yake rahisisheni mazingira ya biashara Kwa kuondoa vikwazo Kwa watu wa chini vinavyokula mapato Yao ndio itasaidia kuwaondoa kwenye umaskini.
Pili anzisheni mfuko wa dhamana ya bila ya mazao Ili kunapotokea bei kuanguka au majanga yanayoharibu mazao ya watu waweze kufidiwa walau Kwa kuwarejeshea mtaji waliotumia.
View: https://www.instagram.com/p/CxZ2Cd4tGi7/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==