Kuanguka Kwa Rostam Aziz; Tafsiri Yangu

...Siasa ni "ka-mchezo" ka ujanja! Nadhgani nikitumia maneno haya ya kijinga Mh. Rostam anaweza kunielewa vema. Simfahamu sana Rostam Aziz ila kwa kumsoma kwenye "kafsha" mbalimbali na ushiriki wake kwenye siasa za CCM na kwa jinsi alivyoweza kumsaidia Jakaya Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2005 na hatimaye JK kupata ushindi wa "kimbunga". Rostam Aziz anadai siasa za CCM ni "uchwara" kwa kuwa ameharibikiwa na biashara zake za kitaifa na kimataifa...! Hii ni sawa na shairi la "KAKA SUNGURA" lililokuwa linasomwa na wanafunzi wa darasa la tatu enzi zile elimu ilivyokuwa na thamani...sizitaki mbichi hizi, naona nafanyakazi bila faida kujua...! Haya ni maneno ya mtu aliyeshindwa kupambana na kasi ya mabadiliko ya ndani na hanikizo la nje ya chama (CCM) kwa kuwa Riostam amekuwa akijihusisha na siasa kwa kuzinufaisha biashara zake. Hakuna uandishi utakayeacha kumuandika Rostam Aziz kwa jinsi alivyoshiriki kwenye siasa za kifisadi na kuendesha ujambazi wa kiserikali kwa kutumia nafasi zake kwenye CCM na IKULU ambapo ana ushawishi mkubwa sana! Tuachane naye kwani aliwahi kunipigia simu na kuniambia, "kama nataka siasa niache ualimu wa chuo kikuu niingie kwanye siasa; na yeye (Rostam) amekuwa tajiri kutokana na urithi wa wazazi wake na ujanja wake kibiashara..."...Binafsi maneno haya yaliniudhi sana kwa vile mwanasiasa hawezi kutumia nafasi yake kufanya ufisadi...na hata maana ya neno hilo, yaani siasa, ni mwendo murua wa kuwatumikia watu bila ya kufisidi mfumo na au ndani ya mfumo! Kuwapa misaada wananchi wa Igunga na kwengineko huku unafanya ufisadi si siasa bali ni si-hasa inayoambatana na ujambazi wa kiserikali.
 
Roatam siyo mwana siasa bali ni mfanya biashara mjanja aliyeamua kutumia uroho wa madaraka wa wanasisa wetu kujitajirisha.Alitumia uroho na shauku iliyovuka mipaka ya JK kuutaka urais kujinufaisha.

Alitumia umafia wake kubuni njia ya kuiba pesa za EPA kwa ajili ya kampeni za kumuingiza JK madarakani.Kutokana na jinsi alivyosimamia zoezi chafu la kumuingiza JK Ikulu alijihakikishia kinga ya kudumu ya kuhujumu uchumi wa nchi hii akijua kabisa hakuna mwenye ubavu wa kumshitaki.Ni kutokana na kelele za CDM ndizo zilizomfikisha hapo wala kamwe siyo shinikizo la CCM.

Leo hii ndiyo anajua siasa uchwara za maji taka wakati yeye ndiye alikuwa kinara wa kuwachafua wanasiasa walioonekana tishio kwa JK wakati ule.Huyu stahili yake ni kunyang'anywa uraia na kushitakiwa tu, tatizo ni kuwa kwa utawala uliopo kwa sasa ni vigumu kwani ni zao lake Rostam,wakijaribu hivyo hata JK hatoki lazima atinge segerea.
 
Kama kuna Mtu anabisha kuhusu mapacha wa tatu kuondoka naamini sasa amekubali alichokua anasema Nape pamoja na CCM! Kwa hili CCM imeonesha Ukakamavu mkubwa na nia ya dhati kukisafisha Chama hicho! Kweli gamba linavulika! Wamebaki mapacha Wawili! Nashauri CCM iendeleze moto huu kila sehemu na hasa idara za serikali! Pia nashauri vyama vingine viiige mfano wa CCM kuwaondoa Mafisadi ndani ya vyama vyao na kuvipa vyama vyao sura ya kuwa vyama vyenye mlengo wa Kitaifa na sio Vyama vya Watu binafsi,Kikabila au Kiukoo!
 
kujivua gamba huku mtu akiwalalamikia baadhi ya wenzie kuwa ndo chanzo cha yeye kuachia ngazi kunatoa picha ipi mkuu? hakuna ukakamavu hapo hali ni tete.kama huamini subiri uchaguzi mdogo Igunga ndo utaamini.
cdm oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
peoples power-aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
viini macho tu......gamba is an outside attempt to look good, kama kusafisha kaburi kwa nje lakini kule ndani ni mifupa na uozo tu....we want true revolution and not these cheap statements. A true turn around if they dare....nawaambia hiyo hakuna
 
kujivua gamba huku mtu akiwalalamikia baadhi ya wenzie kuwa ndo chanzo cha yeye kuachia ngazi kunatoa picha ipi mkuu? hakuna ukakamavu hapo hali ni tete.kama huamini subiri uchaguzi mdogo Igunga ndo utaamini.cdm oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeepeoples power-aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Uchaguzi mdogo igunga ndio uamini nini?
 
kujivua gamba huku mtu akiwalalamikia baadhi ya wenzie kuwa ndo chanzo cha yeye kuachia ngazi kunatoa picha ipi mkuu? hakuna ukakamavu hapo hali ni tete.kama huamini subiri uchaguzi mdogo Igunga ndo utaamini.cdm oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeepeoples power-aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Huamini kama Rostam kajiuzulu?
 
Kama kuna Mtu anabisha kuhusu mapacha wa tatu kuondoka naamini sasa amekubali alichokua anasema Nape pamoja na CCM! Kwa hili CCM imeonesha Ukakamavu mkubwa na nia ya dhati kukisafisha Chama hicho! Kweli gamba linavulika! Wamebaki mapacha Wawili! Nashauri CCM iendeleze moto huu kila sehemu na hasa idara za serikali! Pia nashauri vyama vingine viiige mfano wa CCM kuwaondoa Mafisadi ndani ya vyama vyao na kuvipa vyama vyao sura ya kuwa vyama vyenye mlengo wa Kitaifa na sio Vyama vya Watu binafsi,Kikabila au Kiukoo!
Hapa wanaotakiwa kusifiwa ni CHADEMA waliowasha moto dhidi ya ufisadi na wala sio Magamba! Kilichobaki sasa ni kumtimua Rostam Aziz kwenye Chama na hatimaye kumfikisha Mahakamani na mwisho afilisiwe ili fedha za Watanzania alizozifisadi zirudi wakati Rostam Aziz akiendelea kunyea debe gerezani! Hapo ndio tutajua kama CCM wamedhamiria kuvua gamba au udanganyifu mtupu!
 
Natafakari hali na nadhalia ya CCM kujivua gamba kwa kuwashauri au kuwalazimisha watuhumiwa wa Ufisadi kujiondoa katika Chama kunamsaidiaje Mtanzania wa kawaida ambaye si mwanachama au mpenzi wa CCM.
Mafisadi ni watu wanaotuhumiwa au kusemekana wameiba pesa za SERIKALI na si pesa za CCM. Kujiondoa kwao CCM na kuendelea kula raha mitaani kunasaidiaje kurudisha pesa za SERIKALI (zetu walipa kodi). Hawa mafisadi kujiondoa CCM ni kusaidia kurudisha imani ya watu kwa CCM ili chama kiendelee kuiba vizuri pesa zetu. Kama hawa watu hawakamatwi, kufilisiwa au kurudisha pesa zetu, hii ya kujiuzulu ni kuinufaisha CCM tu.
Kama wanalazimishwa kutoka katika chama na wanakubali, ina maana wanakubali kwamba wao waliiba pesa za SERIKALI na inabidi wakamatwe mara moja.
 
Pablo alijengea maskini nyumba na kuwasaidia mno watu wenye shida lakini alikuwa drug dealer mkubwa.Rostam amefanya mengi makubwa lakini kwa hela ambayo alikubali kuichafua kwa kuingia kwenye siasa.Ni vizuri sas atueleze kuhusu kagoda na jinsi billioni 33 zilivyogawanywa.
Wana Igunga waliozimia jana wanatkiwa watafakari zaidi.
 
pablo alijengea maskini nyumba na kuwasaidia mno watu wenye shida lakini alikuwa drug dealer mkubwa.rostam amefanya mengi makubwa lakini kwa hela ambayo alikubali kuichafua kwa kuingia kwenye siasa.ni vizuri sas atueleze kuhusu kagoda na jinsi billioni 33 zilivyogawanywa.
Wana igunga waliozimia jana wanatkiwa watafakari zaidi.

dpp kanumba soma hiyo.
 
Vituko vilivyotokea Igunga Mjini Igunga, mara baada ya Rostam kutangaza kujiuzulu, vilisikika vilio vya wazee na wanawake katika mkutano huo.
Watu kadhaa walizirai na kupoteza fahamu, akiwamo Mwenyekiti wa (UVCCM) Nzega, Daudi Ng'honge, na Katibu Mwenezi Kata ya Chabutwa, John Mihayo, Katherine Mabula, Zaina Athman pamoja na wanachama wa kawaida.
Baadhi ya vijana walitupa kadi za CCM wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali.
Baadhi ya mabango yalisomeka hivi: "Jogoo hafi kwa utitiri," "CCJ ni Samwel Sitta, Mwakyembe, Nape Nnauye"; "Wasaliti wa CCM ndio magamba ya CCJ"; "Rostam wakikufukuza, na sisi tunaondoka na wewe"; "Rostam tutakufa na wewe"; "Igunga ya leo sio ya mwaka 1994, Rostam ameleta maendeleo Igunga, hatuishi kwa majungu, CCM No 1"; "Igunga bila Rostam haiwezekani"; na "Rostam Mbunge wa Vitendo sio maneno."

Jamani nchii ndio naamini kwamba tupo bado kwenye shimo la ujinga na ulimbukeni ulio kubuhu! Bado watanzania wenzetu kumbe hawajui hata wako wapi na nini kinachoendelea. Tuache utumwa wa kisasa tafadhali.
 
Ndugu zangu ndiyo bye bye ya CCM, walimpa kijana asiye na hekima kuhandle mambo magumu. Tatizo hapo hekima ya Nape na wazee wa CCM ilikuwa ndogo. hilo swala lingemalizika kirahisi kabisa
1. mwakani wana uchaguzi ndio ulikuwa mda muafaka wa kuwaondoa katika NEC
2. uchaguzi wa 2010 ulikuwa muafaka kuwaondoa katika Ubunge,
3. Wanacheza mchezo wa Chadema, CCM kufa kazi
nimefurahi sana CHADEMA mda wote wao wanashinda tuu katika hoja, hili CCM hawana la kujisifia
 
[h=6]CCM na MAGAMBA walicho iba sio mali ya CCM ni mali ya watanzania na nchi ya tanzania kwa makosa haya yakijinga yaliofanywa na watu wenye akili timamu HAWASTAHILI MSAMAHA labda kifungo cha maisha kazi ngumu na viboko kila siku au kunyongwa hadi kufa...NAJIUZULU NYADHIFA ZOTE PAMOJA NA UBUNGE rostam aziz..(muhubiri 7:7.8)( KWELI JEURI HUMPUMBAZA MWENYE HEKIMA NA RUSWA HUUHARIBU UFAHAMU ).NIMEFADHAISWA SANA NIMESIKITISWA SANA NADHANI TATIZO NI UWAZIRI MKUU leo asubuhi nimemwandikia barua rais ya kuomba kujiuzulu kwaniaba ya serekali ya CCM na chama changu!!!..[/h]
 
Mtasema sana kuhusu Rostam, lakini hakuna hata mmoja anaekuja na "solid evidence" ya dhambi zake. Dhambi zake nnazoziona mimi ni:

1) Rangi yake

2) Dini yake

3) Mafanikio yake kibiashara

4) Mafanikio yake kisiasa


Jana tumeona kwenye TV, sio kitu cha kuambiwa jinsi ukumbi, kama si wote, basi zaidi ya nusu ulivyokuwa ukilia alipoamua kujiuzulu. Tumeona waliobebwa kwenye machela waliozimia. Tumeona waliomchaguwa kuwawakilisha wanavyompenda. Sio siri.

Kataja mafanikio ya jimbo lake, hakuna hata mmoja aliekuja hapa akayapinga hayo. Tunaona watu wamemuandama kwa kuwa tu eti, eti, eti, eti nini? hakuna ajuae. Kafanya uamuzi mzuri sana, sasa endeleeni na maji taka, hakuna yatapowafikisha, yeye huyooooooo. Anakula bata kwa mrija, Ni mfanya biashara wa kimataifa.
 
Back
Top Bottom