Kuanguka Kwa Rostam Aziz; Tafsiri Yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuanguka Kwa Rostam Aziz; Tafsiri Yangu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muke Ya Muzungu, Jul 14, 2011.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kwa jinsi Rostam alivyojivua gamba, inaonekana ana mengi sana moyoni. Tena mazito sana.

  Anaonakena kukerwa na tabia ya viongozi ndani ya chama chake. Ametumia wanasiasa wanaondeleza siasa uchwara. Lakini tukirudi kwenye ukweli wa mambo, Rostam ndiye aliyefanikisha kuingia kwa Kikwete madarakani. Amefanya biashara na Ridhiwani ambaye ni mwanaye Kikwete.

  Je kwa siri zote anazifahamu ndani ya Chama?
  Je Rostam anaondoka kwa amani, au anakuja kuiangusha serikali ya JK pamoja na chama tawala?
  Amesema kwa mananeno yake kwamba kuna mengi yanayoendelea ambayo hata waandishi wa habari hawayajui.

  Je Rostam Azizi ana yapi zaidi?
   
 2. c

  calmdowndear JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 602
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Tusijidanganye

  the entire system is rigged, be it wanasiasa wa upinzani au walioko madarakani. 99% of them wameingia pale kwa pesa na sasa wanatufanya wajinga.

  at the end of the day we all know wanasiasa wetu care less about mtu ambaye hana umeme let alone mwenye internet connection. the are so detached from our daily struggles...be it urasimu wa kupata dawa au basic services or simple things kama vile kumilikishwa ardhi na watu husika.


  Zamani they used to care about JF lakini not anymore.

  At the end of the day our society is becoming more and more of the haves...kuanzia wana siasa mpaka wenye kupata haki mbele sheria.
  thats my view.
   
 3. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  You are absolutely right about that, sir!!
   
 4. m

  maggid Verified User

  #4
  Jul 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,
  Habari kubwa imetufikia; Rostam Aziz kaachia ngazi CCM. Ni habari kubwa. Wengine wanasema, kuwa Rostam amejivua gamba. Kuna wanaodai, kuwa ni CCM ndio iliyojivua gamba. Ni misamiati tu, isikuumize kichwa.

  Nimesoma hotuba ya Rostam akiongea na ’ Wazee wa Igunga’. Imekuwa utamaduni, kama wa enzizile za Mwalimu. Kwenye jambo zito, Mwalimu aliongea na ’ Wazee wa Dar es Salaam’. Sio ndio waliomkaribisha mjini.


  Kuna akina sisi tulio tofauti na wale wanaodhani wanajua. Sie tunajitahidi kujua. Na hapa ni tafsiri yangu ya kuachia ngazi kwa Rostam Aziz. Kwangu mie ilikuwa ni suala la wakati tu; kuwa Rostam hakuwa na njia ya kutokea zaidi ya kukubali ’ kujiporomosha’ mwenyewe kutoka kwenye ngazi. Ndio, ni heri anayeshuka kwenye ngazi kuliko anayeachia ngazi na kuporomoka. Kushuka kwenye ngazi kunaashiria taratibu. Kuna upepo mgumu unavuma ndani ya CCM. Na upepo mwingine huangusha miti mikubwa.


  Na Rostam huyu alikuwa ni sehemu ya ’ mapacha watatu’ kama wanavyojulikana sasa; Rostam , Andrew na Edward. Kuna wanaoanza kuhesabu siku kabla kusikia habari nyingine kubwa; kuwa Edward naye ’ kajiporomosha’ kutoka kwenye ngazi za CCM, kisha afutie Andrew. Yote hayo yanawezekana, lakini, kila inapoisha arobasitini moja , karata huchangwa upya. Hapo huanza arobasiti mpya. Siasa yaweza kuwa kama mchezo wa arobasitini! Na mazingira ya Rostam wa Unyamwezini Igunga yaweza kuwa tofauti na ya Andrew wa Usukumani na Edward wa Umasaini. Burudani ya siasa inaendelea!


  Na Watanzania tu mabingwa wa siasa za matukio. Leo ni Rostam. Baada ya wiki moja Rostam si habari tena. Tunasubiri nyingine, labda itakuja ya Edward na baadae Andrew. Na ’ mapacha watatu’ wakishamalizika? Stay tuned; Kuna mpya nyingine itakuja.

  Na Rostam pale Igunga kwa wazee wake amezungumzia ’ Afya ya siasa’ ya nchi. Hakusema kama ni njema au la. Katikati ya mistari kuna tulioelewa alichotaka kusema Rostam. Tena Rostam huyu ambaye kuna wakati iliaminika ndiye yuko nyuma ya ’ mikakati’ ya ndani ya Chama chake.

  Leo kaacha kila wadhifa ndani ya Chama. Lakini usisahau, kuwa Rostam amebaki na ’ hirizi’ mfukoni. Ni kadi ya chama. Mjinga ni yule anayemwondoa Rostam mwenye ’ hirizi’ ya Chama kwenye ’ hesabu’ za mikakati ya CCM.

  Na si amesema mwenyewe; kuwa haikuwa kazi rahisi kwao kuifanya Tabora ambayo ni kitovu cha upinzani kuwa mkoa ambao majimbo yote yanayoongozwa na CCM. Je, Rostam ’ anatishia nyau’ au kuna mtaji anawekeza kwenye ’ nyumba ’ya mchezo wa bao? Na tusubiri tuone.

  Na hii afya ya siasa anayoizungumzia Rostam? Sijui yeye katumia vipimo vya kliniki gani. Mie nitapiga mbizi na kuzama zaidi majini. Na hapa unisome kwa makini . Ndio, kama nchi Watanzania ni kama wagonjwa tunaotafuta tiba. Na tumekuwa ni watu wa kubahatisha tiba kila kukicha. Hata kukimbilia abrakadabra ya kikombe cha ’ Babu wa Lolilondo’ ni kielelezo cha maradhi yetu na kuhangaika kwetu.

  Mgonjwa hukosa faraja na huzidi kuwa na mashaka pale daktari anaposhindwa kufanya diagnos ya ugonjwa husika na kujua ni nini hasa chanzo cha maradhi. Kisha daktari anajaribu kumpa mgonjwa dawa akitumaini tu kuwa huenda ikamsadia. Lakini, mgonjwa hupata faraja na huingiwa matumaini ya kupona pale anapofanyiwa diagnos na daktari anapomtamkia mgonjwa chanzo cha maradhi ya kinachomsibu na dawa anayotakiwa kutumia ili apone.Na ndio sisi Watanzania; tu wagonjwa tunaofanyiwa majaribio ya dawa ya kutuponesha maradhi yetu bila haswa daktari kujua chanzo cha maradhi yetu.


  Nimeandika majuzi tu kwenye Raia Mwema; kuwa Watanzania tunapaswa sasa kuvunja ukimya na kuzungumzia mema na mabaya yaliyopita ili yatusaidie kujenga misingi imara ya taifa letu hata kwa miaka 50 ijayo. Tuna wajibu wa kizalendo wa kutoa ushahidi wetu kwa kusimulia tuliyoyapitia ili waliopo na wajao waweze kuyachukua mema na kutorudia makosa yaliyofanyika nyuma.


  Maana, kuna tulioshuhudia Tanzania iliyokuwa na ustawi na dalili za kuendelea kustawi. Tumeshuhudia pia ni kwa jinsi gani wingu hilo la matumaini lilivyokuwa likipotea kwa kasi ya kutisha na kupisha jua kali lililoleta ukame wa kisiasa na kiuchumi katika nchi yetu.


  Na msingi wa haya yote ni ubaguzi wa kisiasa na kutoruhusu mazingira ya uwepo wa fikra mbadala. Kuwachukia wenye ’ akili’ na walio tayari kuzitumia akili zao kwa manufaa ya nchi yao. Hivyo basi, watu hao hutengwa na mfumo wa uongozi wa kisiasa uliopo.

  Na huo ndio msingi wa uwepo w a hoja ya ubaguzi wa kisiasa. Na dhambi hii ya ubaguzi wa kisiasa ndilo gamba gumu la kitaifa tunalopaswa kulivua. Maana, ndio hali yenye kusababisha maradhi yetu mengi kama taifa ikiwamo ufisadi uliotamalaki.
  Maggid,
  Knivsta, Sweden
  http://mjengwa.blogspot.com
  0736 966032
   
 5. n

  nzom Senior Member

  #5
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 168
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  binafsi mpaka sasa sijapata majibu leo hii wakina mama wa igunga kama wale wa galilaya walitokwa na machozi baada ya mbunge kutangaza hatua ya kujiondoa chamani swali la kwanza ni kweli sijui.pili bashe alitangulia siku kadhaa kuandaa tukio la boss wake kuna kundi la vijana lilitangulia kwa bango na kama episode flani waliingia wakiimba kua hatukbali na akina mama wakatoa machozi hadi kuzrai je walikua wanamlilia RA ama tanganyika yako na je wako tayri kwa hilo au hawakuandaliwa ililieni tanganika na kutaka kuikomboa yote kwa umoja wake pamoja na mambo aliyowafanyia wana igunga ila anayo maswali kwa wana jamii wa tanganyika je yatubibidi nasi kulia kwa kumtaka nae arejeshe chenji zetu za kagoda huenda zikapunguza hasira na machungu na akasimama kama razro na kurudisha kile alichochuka bila ya kujua ni haki ya watu wengi sana enyi igunga zililieni nfasi zenu na tanganyika yenu
   
 6. n

  nzom Senior Member

  #6
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 168
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mbuzi anakula alipofungwa si urefu wa kamba yake
   
 7. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,301
  Likes Received: 953
  Trophy Points: 280
  Si angeweka mambo yote hadharani, anaognpa nini?
   
 8. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Rosam A amejiuzulu wadhifa wake wa ubunge na kuliachia jimbo la Igunga wazi. Hivi karibuni tume ya taifa ya uchaguzi itatangaza tarehe ya marudio kwa ajili ya kuziba pengo.

  Tunawaomba wana CDM wote waliopo mitaa ya Igunga kujiandaa kwa uchaguzi huo kwa uhakika wa ushindi ili kuonyesha Serikali ya CCM maisha magumu sio sehemu yao. Nuru mpya, uchumi mpya na elimu bora kwa kizazi cha sasa na kijacho.

  Vile vile Hongera Dr. Slaa kwa kuwakimbiza mafisadi mpaka wanakosa sehemu ya kujificha.
   
 9. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #9
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - Well, ni wakati wa kutoa credit when it is due na it is ok with God too!;

  - Hongera sana Katibu Mwenezi wa CCM; Mheshimiwa Nape kwa kuweza kusimamia ahadi ambayo ilikuwa ni deni tayari, I mean ahadi ya kujivua magamba; leo tumejionea kwa macho kwamba sasa ni kazi hakuna mchezo!

  - HOWEVER: Sasa tunaomba sana hawa magamba wakishatoka wote, waelekezwe kwenye mkono wa Sheria ndipo haki itakuwa imetendeka kwa hili taifa na hasa watoto wetu ambao ndio wanachi wa taifa letu la kesho!

  - Niliwahi kusema huko nyuma kwamba kama Mheshimiwa Nape, ananidanganya kuhusu kujivua, basi nitarudisha kadi ya CCM na kumuomba sana ajiuzulu pia, lakini Nape you have come through kama nilivyosema kwamba kama ungejua kwamba hakuna mabadiliko usingeshika hiyo nafasi, saafi sana kazana sana ndugu yangu, tupo nyuma yako, mabadiliko lazima au tujiuzulu!

  - Sasa huu ufagio ufike mpaka chini kwa maviongozi magoi goi wote safisha, waondoke sasa wale wote waliokuwa wanawashabikia hawa mafisadi, wote waondolewe maaana sasa kichwa chao kimeondoka mkia hauwezi kuwa tatizo!


  Willie @ NYC, USA.
   
 10. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  we kaka mbna unakosa busara? RA KAJITOA KATIKA CHAMA?

  Nape ndo chanzo?

  Kelele za wanamitandao,magazeti,viongoz wa dini vyama vya siasa?

  Release your brainware from magambas idiology!
   
 11. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Rostam and EL are innocent. They are just the victims of a few cheap politicians within CCM like Wangwe, Nape, January, Membe, Mwakyembe et al. who want to solidify their political ambitions as we are heading towards 2015.
  If you think there's any concrete eveidence (not just mere speculations) to sugget so then why in the world the state apparatus and other law enforcement agencies like Takukuru and the anti-graft czar (Hosea) as well as the Attorney General have been so reluctant to prosecute Rostam and Lowassa? If Chenge was found not guilty in the radar scandal then what makes you think RA and EL are responsible for grand corruption allegations?
   
 12. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2011
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Nadhani kujiuzulu haitoshi warudishe pesa za walalahoi walizoiba, pamoja na riba, then mahakamani, ili wapewe mshahara wa ufisadi wao

  Hii mijamaa ndio imerudisha nyuma maendeleo ya hili taifa, naamini lazima tutaendelea kama sheria za nchi zitaheshimiwa na kutobagua. Hata kama ni rais mtaafu ni vema afilisiwe na kupelekwa mahakamani. Mbona mataifa mengine wameweza, Miezi michache rais mtaafu wa Israel amehukumiwa kifungo cha miaka nadhani 6 kwa kosa la kubaka. hapa kwetu mijmaa imeiba mchana kweupe bado inajitetea haijaaiba

  ni vema ikatambua wanakula laana, ambayo wao na vizazi vyao lazzima walipe
   
 13. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  In this country, if you work very hard and bust your as.s off and eventually become very successful then you become a fisadi in the eyes of the people. This legacy of mwalimu's socialism is a poison to the minds of millions of Tanzanians.
   
 14. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hii thread iunganishwe na ile ya Rostam Aziz ya "kujivua gamba". Sioni jipya hapa. Otherwise, tunakuwa na too much duplicated threads discussing the same issue.

  UPDATE: Hapa nilikuwa na refer thread ya Melecela aliyoianzisha separately (post number 9 hapo juu) pamoja na kuwa kulikuwa na thread ambayo ilikuwa inajadili issue hiyo hiyo. Thanks Mod for noting this. Heri kila mtu atoe tafsiri yake kwenye thread moja kama hii badala ya kufungua separate thread.
   
 15. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hii thread iunganishwe na ile ya Rostam Aziz ya "kujivua gamba". Sioni jipya hapa. Otherwise, tunakuwa na too much duplicated threads discussing the same issue. Kila mtu atakuja na tafsiri zake hapa. Wakati tunatoa povu hapa, nyie mlikuwa wapi? Mnasubiri baada ya yeye kujiuzulu ndio mnajidai kuja na tafsiri zenu.

  UPDATE: Hapa nilikuwa na refer thread ya Mjengwa aliyoianzisha separately (post number 4 hapo juu) pamoja na kuwa kulikuwa na thread ambayo ilikuwa inajadili issue hiyo hiyo. Thanks Mod for noting this. Heri kila mtu atoe tafsiri yake kwenye thread moja kama hii badala ya kufungua separate thread.
   
 16. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  It's a pity that in Tanzania, if you work really hard, bust your as.ss off and shake your tail, persevere and eventually become very successful then you are a fisadi in the eyes of the millions of wananchi. Nyerere's ghosts and legacy of socialism still do seem to poison the brains of my fellow Tanzanians.
  It's ok for a rich or even a bogus foreign investor to come and loot this country, but when a local businessman work hard and succeed he's seen as a fisadi!! ha ha ha
   
 17. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  It's not fair for the people of Igunga and Aden Rage as well.....there gonna be taxation without representation
   
 18. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  It's not fair for the people of Igunga and Aden Rage as well.....there gonna be taxation without representation
   
 19. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #19
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  It's not fair for the people of Igunga, Tabora and Aden Rage as well.....there gonna be taxation without representation
   
 20. RAJ PATEL JR

  RAJ PATEL JR JF-Expert Member

  #20
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  C'mon man, when an MP resigns then it's not fair for the constituency represented.
   
Loading...