Kuangalia Tamthiliya vs Michuano ya Kombe la Dunia!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
WanaJF,
Nimekuwa na tatizo kidogo ndani ya familia yangu, hasa wakati huu wa michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea kule Afrika ya Kusini. Mimi napenda kuangalia michuano hiyo kupitia runinga, especially zinapocheza timu za Afrika lakini "ubavu wangu" unapenda sana kuangalia tamthiliya! "Katatizo" hako kako kwenu jamani au ni mimi tu jamani! Natamani niwe naangalia kwa jirani lakini naona haipendezi, inawezekana huko nako kuna "tatizo" kama hilo. Jana niliangalia kipindi kwenye Channel 5 nako walizungumzia "tatizo" hilo na ilisemekana kwamba kuna mama wa familia moja aliamua kununua TV yake mwenyewe ili aendelee kuangalia tamthiliya, huku baba na wakaka wakiangalia michuano ya kombe la dunia! Ama kweli kuna mambo!
 
Tatizo hilo lazima liwepo kwenye jamii.Hata siku moja hatuwezi watu wote kufanana interests.Dawa ndio hiyo kununua tv 2.moja nyumbani nyingine chumbani.Kama pesa shida bora wewe baba uende kuangalia hata kwenye hizi zinaonywshwa na tigo kwenye viwanja vya wazi.au hata kwenye kumbi maalumu huwa wanaonyesha.
 
hilo ni tatizo laweza kuwepo sehemu nyingi ikiwemo kwangu! ni kuvumilia tu ukiweza kuangalia mpira angalia na mama nae akiweza kuchek tamthilia siku inapita. kwani mwisho si july tu!
 
Kweli mkuu,

Hidden Passion ilitaka kunipa kichaa. Wife haambiwi wala hasikii kitu na analazimisha nisiangile mpira. Nikilazimisha kuangalia mpira analalamika hadi nakosa raha. Sasa tumeamua kukata mzizi wa fitina kwa kutafuta TV ya pili. Yeye anatesa na tamthilia zake na mimi nafaidi kombe la dunia. Pia huwa tunakuwa na tatizo wakati wa taarifa za habari. Yeye anapenda kuangalia vipindi vya burudani na hata utabiri wa Shekh Yahaya wakati mimi nataka kupata news. Ni vigumu sana na kitu cha msingi ni kuvumiliana. Kama haiwezekani kuwa na TV 2 basi mnaweza kupeana zamu ingawa watu wa tamthilia wanakuwa wagumu kukubaliana na hilo!
 
Mie niliamua kununua ka Luninga kengine nikaweka room raha jipe mwenyewe...
Lakini sasa tunaenda sambamba kwenye soka mie pia ni mshabiki mkubwa ..tamthilia naangalia marudio siku za weekend
 
Kweli mkuu,
watu wa tamthilia wanakuwa wagumu kukubaliana na hilo!

Kweli kabisa, wako very conservative, imekuwa kama ibada! Shughuli zote zinaachwa, simply kwa ajili ya tamthiliya! Inakera sometimes!
 
WanaJF,
Nimekuwa na tatizo kidogo ndani ya familia yangu, hasa wakati huu wa michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea kule Afrika ya Kusini. Mimi napenda kuangalia michuano hiyo kupitia runinga, especially zinapocheza timu za Afrika lakini "ubavu wangu" unapenda sana kuangalia tamthiliya! "Katatizo" hako kako kwenu jamani au ni mimi tu jamani! Natamani niwe naangalia kwa jirani lakini naona haipendezi, inawezekana huko nako kuna "tatizo" kama hilo. Jana niliangalia kipindi kwenye Channel 5 nako walizungumzia "tatizo" hilo na ilisemekana kwamba kuna mama wa familia moja aliamua kununua TV yake mwenyewe ili aendelee kuangalia tamthiliya, huku baba na wakaka wakiangalia michuano ya kombe la dunia! Ama kweli kuna mambo!

There is no solution for that except to have a second set of TV in your bedroom
 
Lakini wote tunajua kina mama na Tamthilia kina baba na Mpira
Na wote tunapenda kupata kitu ile roho inapenda
Na unakuta siku ya mechi nzuri ndio siku Tamthilia ya jana yake ilikomea sehemu nzuri unataka uone kama Juan Miguel na Onelia wamefikishana wapi na kesi za mtoto Mahita inakuwa kazi kweli kweli...
 
Hapo ndipo panakua pagumu, TV moja na hapo ndani kila mmoja anataka kuangalia program tofauti na mwezake. Mimi inabidi niwe natoka kwenda Pub ya karibu na home kucheki mpira, then unajua tena pub... moja mara ya pili ya baridiiii.. mara ngoma sita home... kanuna tena duuuu !!! we acha ni shughuli wakuuu hapo.
 
Kweli kabisa, wako very conservative, imekuwa kama ibada! Shughuli zote zinaachwa, simply kwa ajili ya tamthiliya! Inakera sometimes!

Mkuu, hii kitu ina addiction ya ajabu. My wife and I became very very close when following one them (SUNSET BEACH) hadi tukatangaza nia! Ilikuwa kila jioni lazima tuwahi na kubanana kwenye kochi tusipitwe. Baadaye nikaona huo ulevi ni hatari nikaachana nao. Kwa mtu aliyewahi kufuatia hizi Tamthiliya anajua kabisa kuwa ni hatari sana kwani huwezi ku-concentrate na kitu chochote muda wake ukishafika, hata uwekewe mtutu!

There is no solution for that except to have a second set of TV in your bedroom

Maisha kweli hayana kanuni. Nakumbuka hapa JF kuna mtu alishawahi kushauri kuwa kuweka TV bedroom ni hatari kwani kule ni mahali patakatifu pa bwana kwa hiyo hakuna vurugu yoyote inayotakiwa ili watu wafanye shughuli moja tu ya kumtukuza muumba. Kumbe hilo ni suala la kufikirika au?
 
Hapo ndipo panakua pagumu, TV moja na hapo ndani kila mmoja anataka kuangalia program tofauti na mwezake. Mimi inabidi niwe natoka kwenda Pub ya karibu na home kucheki mpira, then unajua tena pub... moja mara ya pili ya baridiiii.. mara ngoma sita home... kanuna tena duuuu !!! we acha ni shughuli wakuuu hapo.

Hongera sana kama wewe unaishia hapo. Wengine wanajikuta wanaanza kuchungulia chungulia kuku wadogo!
 
Maisha kweli hayana kanuni. Nakumbuka hapa JF kuna mtu alishawahi kushauri kuwa kuweka TV bedroom ni hatari kwani kule ni mahali patakatifu pa bwana kwa hiyo hakuna vurugu yoyote inayotakiwa ili watu wafanye shughuli moja tu ya kumtukuza muumba. Kumbe hilo ni suala la kufikirika au?[/QUOTE]

ni kweli kuwa na TV bedroom haipendezi na ndio hapo mawasiliano baina ya baba na mama yanapotea! imagn pale unapotaka kuongea na mwenzio yy ndo yuko busy na tamthilia! sifagilii kabisa TV kuwekwa bedroom.
 
Lakini wote tunajua kina mama na Tamthilia kina baba na Mpira
Na wote tunapenda kupata kitu ile roho inapenda
Na unakuta siku ya mechi nzuri ndio siku Tamthilia ya jana yake ilikomea sehemu nzuri unataka uone kama Juan Miguel na Onelia wamefikishana wapi na kesi za mtoto Mahita inakuwa kazi kweli kweli...

FL1, mimi nakubaliana na wanaosema ninunue TV2, maana nimejitahidi kujifanya nafuatilia tamthiliya na mimi ili nimfanye aniruhusu kuangalia mpira lakini amekuwa very conservative. Pia mimi ni mtu wa kuangalia sana International News kwenye channel za nje, lakini nazo mara nyingine zinapigwa chini. Hapa solution ni TV2 tu!
 
Hili kweli ni tatizo na hasa mtu ukiwa shabiki wa mpira peke yako ndani ya nyumba na wengine ni wapenzi wa tamthilia inakuwa ni balaa. Watu wanashauri tv ya pili inunuliwe ili kuepukana na tatizo hili lakini sio wote wenye uwezo wa kuongeza tv ya pili. Inabidi kutumia ubabe tu pale inapobidi kwa mfano kuficha remote au kuiharibu kabisa.....ni upuuzi kukosa kutazama mechi kwa sababu ya tamthilia!
 
Hapo ndipo utakuwa umefanya jambo la maana ..naona kama ununue leo vile si unajua zimebakia mechi muhimu sana kuziangalia ..:biggrin1:
 
Hili kweli ni tatizo na hasa mtu ukiwa shabiki wa mpira peke yako ndani ya nyumba na wengine ni wapenzi wa tamthilia inakuwa ni balaa. Watu wanashauri tv ya pili inunuliwe ili kuepukana na tatizo hili lakini sio wote wenye uwezo wa kuongeza tv ya pili. Inabidi kutumia ubabe tu pale inapobidi kwa mfano kuficha remote au kuiharibu kabisa.....ni upuuzi kukosa kutazama mechi kwa sababu ya tamthilia!

Katavi, huo ushauri wako ni hatari sana. Maumivu ya kicha huanza taratibu, na usipomwona Daktari uanweza kuishia kutubu kitu kingine. Hiyo tabia lazima itazaa trauma ambazo zinaweza kuwa vigumu kuzitibu. Kila mtu anathamini anachokipenda na hakuna mwenye haki zaidi ya mwenzake inapokuja kwenye hisia za watu. Kujaribu kukandamizi hisia kutazaa chuki kama za Alqaeda na Osama! Utapenda hayo yatokee kwenye familia yako?
 
kuwa na tv mbili nafikiri ndio mwanzo wa kuanza kupotezeana mawasiliano baina ya baba mama na watoto.

ningesema mwanamke avumilie lakini kuna watu wako addicted kabisa na tamthiliya nitakuwa namuonea. Ningekushauri ununue dvd player yenye ku rikodi.

Tamthilia yake unairikodi kwenye channel nyengine, ukimaliza mpira mnaangalia nyote kwa pamoja. ( hapa kuangalia pamoja jambo la msingi kwa sababu utakuwa ushamkosesha raha ya kuangalia tamthilia LIVE...lol)
 
Hapo pagumu pia. Mimi nilishaapa kwamba sitaangalia tamthiliya tena. Sasa hiyo option haiwezekani kwangu. Nadhani la msingi ni kutafuta suluhu ambayo wote mnakubaliana nayo.
 
dark city .......hujui kuwa waswahili wanasema 'mapenzi ni kudanganyana'?

sasa huwa hutizami kweli ile tamthilia, una hang tu pale ukumbuni maybe na kitabu chako au na gazeti lako (whatever else u want to do), bila ya kuangalia hiyo tamthilia ............mradi akuone tu uko karibu na umemuonea huruma kumkosesha kutizama tamthilia yake kwa wakati aliotaka
 
Back
Top Bottom