Kuadimika kwa bia mkoani Mbeya

Kuadimika kwa bia mkoani Mbeya

Dah! Bia yangu pendwa ya Kilimanjaro imekuwa adimu sana hapa Mbeya. Inabidi nipumzike au kuacha kabisa pombe.
 
Bingwa inazalishwa hapohapo mbeya na haivuki mkoa wa Iringa inacheza nyanda za watu weusi hukohuko zinaadimikaje?

Zingine ni sawa kwa huko zinaadimika sana
Tena hiyo BINGWA imekuwa kama bangi utaisaka kwa tochi nawala hutaipata, mtu akikuona nayo anafanya kukushangaa nalazima akuulize umeipata wapi
 
Tena hiyo BINGWA imekuwa kama bangi utaisaka kwa tochi nawala hutaipata, mtu akikuona nayo anafanya kukushangaa nalazima akuulize umeipata wapi
Bingwa 🤣🤣🤣 chupa kubwa au ndogo ama zote?
 
Bingwa inazalishwa hapohapo mbeya na haivuki mkoa wa Iringa inacheza nyanda za watu weusi hukohuko zinaadimikaje?

Zingine ni sawa kwa huko zinaadimika sana
Sometimes Bingwa inakua bidhaa adimu hasa kama TBL wanataka kupush kinywaji kingine.

Ila hivyo vyote vitatu kutopatikana basi kuna bidhaa wanafosi muiuze walau kidgo.
Ama lah wauzaji wenywewe kwa wenyewe wanafanyiana hujuma ili wauze bei kubwa
 
Bingwa ile ni konyagi dadeki ile sio bia kabisa.
Wanywa bingwa wana code zao utawajua tu 😀😀
 
Sometimes Bingwa inakua bidhaa adimu hasa kama TBL wanataka kupush kinywaji kingine.

Ila hivyo vyote vitatu kutopatikana basi kuna bidhaa wanafosi muiuze walau kidgo.
Ama lah wauzaji wenywewe kwa wenyewe wanafanyiana hujuma ili wauze bei kubwa
Sidhani nina uzoefu mkubwa wa hiki kitu nimefanya kazi na Mzalendo Iringa pale.

Huwa inatokea Bia zinaadimika na viwanda vya TBL vinaanza kufanya mgawo wa pombe kutokana na production kuwa ndogo So labda TBL mbeya wanataka gari 400 ila matokeo yake wanapelekewa 100 ambazo hazitakidhi viwango.

Ajabu ni hapo kwa Bingwa hii inazalishwa mbeya iweje ipotee
 
Bingwa 🤣🤣🤣 chupa kubwa au ndogo ama zote?
Zote..kwanza bingwa ndogo miniliziona maramoja tu mpaka nikashangaa sijui zilikuwa kwenye majaribio izo ndo kabisa sikumbuki mara yamwisho kuziona sokoni ilikuwa lini
 
Sometimes Bingwa inakua bidhaa adimu hasa kama TBL wanataka kupush kinywaji kingine.

Ila hivyo vyote vitatu kutopatikana basi kuna bidhaa wanafosi muiuze walau kidgo.
Ama lah wauzaji wenywewe kwa wenyewe wanafanyiana hujuma ili wauze bei kubwa
Hapa kidogo kuna kamwanga nakapata,sasa ndio watulazimishe tunywe tubia twakike eti castle lite na flyng fish ndo angalau zinapatikana
 
Habari wakuu!

Ni karibu mwezi wa pili sasa mfululizo, upatikanaji wa bia mkoani Mbeya umekuwa changamoto kubwa. Bia kama Bingwa, Safari, na Kilimanjaro zinapatikana kwa nadra sana. Wenzetu wa TBL Mbeya, tafadhali mtujulishe shida ni nini?

Je, wenzetu wa mikoa mingine mnakumbana na changamoto kama sisi?

Bei kwa Kreti endapo ukizibahatisha:
  • Bingwa: 27,000 hadi 29,000
  • Safari na Kilimanjaro: 37,000 hadi 38,500
Sasa hizo bei siyo tatizo sana, shida kubwa ni mzigo kupatikana.
Mkoa wa mara pia Kilimanjaro hazipatikani week ya tatu sasa
 
Back
Top Bottom