Kuachwa kunauma Jamanii usiombe ikikute

Kuachwa kunauma Jamanii usiombe ikikute

Toka Fastjet wanikate nikiwa kwenye msitari, sikuwahi kuwaombea mazuri.

Walikula 120,000/- kiurahisi sana. Na tulikuwa zaidi ya watu 12.

Pole Cleroo, safari ina mitihani mingi sana.

Ila kuachwa au kubaki wakati wewe ushajianda / uko tayari kusafiri inauma mnoo.
 
Na basi lakini sio hayo mapipa yenu teh

Sent using Jamii Forums mobile app

Kuachwa haijalishi usafiri gani, hata lifti ikikuacha unaumia. Yaani umetoka kwenye korido mbio uwahi lifti ile umefika pale lifti hiyoo imeondoka....

Hata daladala ile umelikimbilia kumbe konda hajakuona gari inaondoka.... inuma unasema ningejua nisingekimbilia aahahahahahaa.


Usafiri Kafiri.
 
Kuachwa haijalishi usafiri gani, hata lifti ikikuacha unaumia. Yaani umetoka kwenye korido mbio uwahi lifti ile umefika pale lifti hiyoo imeondoka....

Hata daladala ile umelikimbilia kumbe konda hajakuona gari inaondoka.... inuma unasema ningejua nisingekimbilia aahahahahahaa.


Usafiri Kafiri.
Hahaha tena usiombe unaona daladala ileee inaondoka mbele yako, nyingine huwa inakawia kuja kama nini[emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapendwa,

Habari za kutwa nzima na habari za usiku huu. Nyie jamani kama hujawahi kuachwa usitamani hiyo hali ikukute.
Kuachwa kunauma nyie jamani, yaani moyo unauma, akili inajaa mawazo na majuto, kila mtu unamuona mbaya, huoni kuwa wewe mwenyewe ndo sababu kuu ya kuachwa bali waliokuzinguka....

Uso unakuwa na tahayari, umechokaa hooii... tabasamu hakuna, hasira... unaweza jikuta uko mbele za watu wala huoni kama kuna watu, unavua viatu, unakaa chini kabisa sakafuni bila kujali kwamba utachafuka au laah.

Wakati huo akili si yako tena, unawaza gharama ulizoingia, halafu namna utavyoingia gharama nyingine kuendelea mbele....

Naona bado mnakodoa macho hamuelewi au hamuamini mnachosoma. Wacha nitoe mifano mnielewe vizuri.

Hakuna maumivu makali kama kuachwa na ndege. Yaani ticket yako inakuarifu ndege itaondoka saa nne na nusu asubuhi ila utatakiwa kufika airport saa moja na nusu asubuhi (masaa matatu kabla ya ndege kupaa). Na mlango au dirisha la kufanya usajili wa abiria wanaosafiri litafungwa dakika 40 kabla ya ndege kupaa. (Hapa wamekuacha upige mahesabu mwenyewee ni saa ngapi mwisho ku check in) hii inaonesha hesabu haikimbiwi, kama uliikimbia shule utakutana nayo uraiani huku kwenye maisha. Tena unaipiga kwa kichwa hehehehhehe hatari.

Sasa tujiulize, ni kitu gani kinasababisha mtu aachwe..?? Safari unaifahamu tuseme siku tatu kabla, na muda wa kuondoka uko wazi.....

Nishaona sura kadhaa zinakuja zinatweta kashikilia mabegi huku na kule, kutoka check point hata mkanda na viatu hajavaa ticket iko mdomoni halafu counter ya check in ishafungwa na wafanyakazi hawapo washaondoka...... safari inaishia hapo. Huna hata wa kumuomba ubembeleze wakiruhusu uiwahi ndege.Inauma aiseeh maana yalishanikuta. Mara zote ilikuwa ni uzembe tuu kwa upande wangu sikuwa na sababu maalum.
Halafu kinachouma zaidi, ndege inakuwa bado haijaondoka sema ndo taratibu za usafiri wa pipa.

Nishawahi fukuza basi hadi Kibaha nikapanda nikiwa niko restless nilikuwa na landcruiser mkonge la kazini.

Treni enzi zile naenda jeshini nilidandia behewa la mwisho. Boat tuu ndo sijathubutu kulifukuzia 😅😅😅 hehehehheee.

Ila baadae nikaona huu ni uzembe, nilipohamia nchi za watu ambapo muda ni mali, aiseeh siwezi achwa na gari wala ndege wala basi. Hata appointment nafuata muda mnoo. Ikitokea kuna vikwazo natoa taarifa mapema ili nisiwekwe kwenye list ya no show.

Hahahahaha poleni, kuna baadhi yenu mlishaona eenheee Kasie kaachwa na Dadii.... waapi bado tupo tupo sanaa🤪.

Labda tukifikisha miaka 90 ndo tutaachana hehehehehehhe.

Wewe ulishawahi kuachwa!!?? Ulijisikiaje?? Sababu ya kuachwa ni ipi? Baada ya kuachwa ulifanyaje kuendelea au kukamilisha safari?

Kasie Mahaba Matata.

Acha kabisa, ilimkuta jamaa yangu nilikuja naye kumsindikiza ili mimi nirudi na gari, jamaa alikimbiza gari kama la mashindano, ile tunafika airport, tumepaki, tunashuka, jamaa anakimbia kuingia check in, kwa nyuma naona ndege ndo inaanza kutembea na gurudumu kuchochea tayari kwa take off. mara tunaiona ndege hiyoooooooooooooooooooooooooooooooo!!! Aliisindikiza kwa macho mpaka inapotelea angani akarudisha macho chini kwa huruma.
 
Acha kabisa, ilimkuta jamaa yangu nilikuja naye kumsindikiza ili mimi nirudi na gari, jamaa alikimbiza gari kama la mashindano, ile tunafika airport, tumepaki, tunashuka, jamaa anakimbia kuingia check in, kwa nyuma naona ndege ndo inaanza kutembea na gurudumu kuchochea tayari kwa take off. mara tunaiona ndege hiyoooooooooooooooooooooooooooooooo!!! Aliisindikiza kwa macho mpaka inapotelea angani akarudisha macho chini kwa huruma.


Hahahahaha I can see maumivu alipaliyoyapata......

Kuachwa kunauma.....
 
Nimekuja mbio mbio nikidhani ntakuta bombshell ya habari kuwa Kasie na Dadii sasa ni kaput!

Kumbe wapi!

Kasie kawaacha watu wananing’inia tu. Hawaelewi kinachoendelea.

Ila kuachwa kunauma. Ndivyo nilivyosikia. Haijawahi kunitokea.
 
Back
Top Bottom