Kuachwa kunauma Jamanii usiombe ikikute

Kuachwa kunauma Jamanii usiombe ikikute

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,805
Reaction score
43,230
Wapendwa,

Habari za kutwa nzima na habari za usiku huu. Nyie jamani kama hujawahi kuachwa usitamani hiyo hali ikukute.
Kuachwa kunauma nyie jamani, yaani moyo unauma, akili inajaa mawazo na majuto, kila mtu unamuona mbaya, huoni kuwa wewe mwenyewe ndo sababu kuu ya kuachwa bali waliokuzinguka....

Uso unakuwa na tahayari, umechokaa hooii... tabasamu hakuna, hasira... unaweza jikuta uko mbele za watu wala huoni kama kuna watu, unavua viatu, unakaa chini kabisa sakafuni bila kujali kwamba utachafuka au laah.

Wakati huo akili si yako tena, unawaza gharama ulizoingia, halafu namna utavyoingia gharama nyingine kuendelea mbele....

Naona bado mnakodoa macho hamuelewi au hamuamini mnachosoma. Wacha nitoe mifano mnielewe vizuri.

Hakuna maumivu makali kama kuachwa na ndege. Yaani ticket yako inakuarifu ndege itaondoka saa nne na nusu asubuhi ila utatakiwa kufika airport saa moja na nusu asubuhi (masaa matatu kabla ya ndege kupaa). Na mlango au dirisha la kufanya usajili wa abiria wanaosafiri litafungwa dakika 40 kabla ya ndege kupaa. (Hapa wamekuacha upige mahesabu mwenyewee ni saa ngapi mwisho ku check in) hii inaonesha hesabu haikimbiwi, kama uliikimbia shule utakutana nayo uraiani huku kwenye maisha. Tena unaipiga kwa kichwa hehehehhehe hatari.

Sasa tujiulize, ni kitu gani kinasababisha mtu aachwe..?? Safari unaifahamu tuseme siku tatu kabla, na muda wa kuondoka uko wazi.....

Nishaona sura kadhaa zinakuja zinatweta kashikilia mabegi huku na kule, kutoka check point hata mkanda na viatu hajavaa ticket iko mdomoni halafu counter ya check in ishafungwa na wafanyakazi hawapo washaondoka...... safari inaishia hapo. Huna hata wa kumuomba ubembeleze wakiruhusu uiwahi ndege.Inauma aiseeh maana yalishanikuta. Mara zote ilikuwa ni uzembe tuu kwa upande wangu sikuwa na sababu maalum.
Halafu kinachouma zaidi, ndege inakuwa bado haijaondoka sema ndo taratibu za usafiri wa pipa.

Nishawahi fukuza basi hadi Kibaha nikapanda nikiwa niko restless nilikuwa na landcruiser mkonge la kazini.

Treni enzi zile naenda jeshini nilidandia behewa la mwisho. Boat tuu ndo sijathubutu kulifukuzia 😅😅😅 hehehehheee.

Ila baadae nikaona huu ni uzembe, nilipohamia nchi za watu ambapo muda ni mali, aiseeh siwezi achwa na gari wala ndege wala basi. Hata appointment nafuata muda mnoo. Ikitokea kuna vikwazo natoa taarifa mapema ili nisiwekwe kwenye list ya no show.

Hahahahaha poleni, kuna baadhi yenu mlishaona eenheee Kasie kaachwa na Dadii.... waapi bado tupo tupo sanaa🤪.

Labda tukifikisha miaka 90 ndo tutaachana hehehehehehhe.

Wewe ulishawahi kuachwa!!?? Ulijisikiaje?? Sababu ya kuachwa ni ipi? Baada ya kuachwa ulifanyaje kuendelea au kukamilisha safari?

Kasie Mahaba Matata.
 
Nilishaachwa na ndege sababu ya ubahili na ubishi/ujuaji

Nilikuwa mkoa fulani hivi shule sasa nilikuwa narudi Dar...uo mkoa kutoka hostel ninayokaa hadi airport ni mbali haswaaa na kwasababu baba anaujua umbali wa nilipo na airport akaniambia nichukue tax ili nisisimame simame njiani...ubishi!

Nikajikuta mimi mchumi sana nikasema napanda dala dala ili nisave ela ukicheki tax ni sh 20,000 akati daladala ni sh 900 tu

Kilichonikuta nilifika airport watu washachekiwa na hakukua na namna ya mimi kusaidiwa na ile kampuni mbovu!
 
Aiseeh polee, sasa kupata ticket nyingine ya ndege inayofuata ni shughuli.

Kama shekeli hakuna, mabasi yanahusika.
 
Aiseeh polee, sasa kupata ticket nyingine ya ndege inayofuata ni shughuli.

Kama shekeli hakuna, mabasi yanahusika.
Asante
Ile kampuni ya ajabu sana...nilijiliza pale ili wanielewe ila wapi!
 
Asante
Ile kampuni ya ajabu sana...nilijiliza pale ili wanielewe ila wapi!

Yaani hicho ndo kinatilisha hasira zaidi, yaani hakuna hata wa kukusemesha walau kukutia moyo machungu yapungue......

Kinachotia uzito zaidi, namna ya kurudi ulikotoka (nyumbani) ili ujiande na safari nyingine aahahahahahahaha.

Yaani mabegi unayaona mazitooo, sura imetahayariii....

Kasinde.
 
Niliachwa na ndege kwa usistaduu wangu.
Tulikua tunatoka Zanzibar na rafiki zangu tunaenda Mwanza. Tumeshuka na boat wao wakati wanaenda airport mimi nikaenda salon kinindoni kushonea weave. Kuja kushtuka imebaki 30mins kumaliza kucheck inn. Nikakodi pikipiki na uoga wangu wote.
Nafika airport wameshamaliza. Nikajiliza liza mpaka napata akili namjua mkubwa mmoja wa hiyo ndege tayari muda umeshaenda ndege inataka kuruka.
Wakaniambia niongezee hela niondoke jioni yake ila ya kesho yake asubuhi ilikua cheap zaidi.
Nikalipia nikaenda kulala lodge za karibu.
Nilikasirika hadi nikaumwa kichwa.
Mpaka leo sichelewi tena.
Nilipata somo KUACHWA KUNAUMA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani hizo kampuni hazina refund/compensation policies kama uki-miss flight?
 
Ndege co basi la Abood

Yeah inajitaji kitofautisha, ila ukikaa airport wakati unasubiri flight yako huwa nakutana na vioja kama hivi.... saa ingine ni mtu tuu na heshima zake like mmiliki wa kampuni flani unakuta alishaacha gari tazara huko akapanda bodaboda. Kapigwa na upepo shati limeparanganyuka paranganyuka halafu bado kaachwa.....

Ile sura ya kuachwa ndo huwa inatilisha huruma hadi basi.
 
Hello
Niliachwa na ndege kwa usistaduu wangu.
Tulikua tunatoka Zanzibar na rafiki zangu tunaenda Mwanza. Tumeshuka na boat wao wakati wanaenda airport mimi nikaenda salon kinindoni kushonea weave. Kuja kushtuka imebaki 30mins kumaliza kucheck inn. Nikakodi pikipiki na uoga wangu wote.
Nafika airport wameshamaliza. Nikajiliza liza mpaka napata akili namjua mkubwa mmoja wa hiyo ndege tayari muda umeshaenda ndege inataka kuruka.
Wakaniambia niongezee hela niondoke jioni yake ila ya kesho yake asubuhi ilikua cheap zaidi.
Nikalipia nikaenda kulala lodge za karibu.
Nilikasirika hadi nikaumwa kichwa.
Mpaka leo sichelewi tena.
Nilipata somo KUACHWA KUNAUMA

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa ikukute unasalio la kuongezea kukata ticket nyingine na hela ya lodge. Kuna watu wanasafiri kamili kamili hela ya ziada aliyonayo ni ya kula njiani au taxi akifika.

Ndo maana waswahili wakasema safari ni hatua.
 
Kama Mungu tu nilikua na hela ikabidi nilipie ila liniuma laki na 35 yangu sitasahau
Hello

Sasa ikukute unasalio la kuongezea kukata ticket nyingine na hela ya lodge. Kuna watu wanasafiri kamili kamili hela ya ziada aliyonayo ni ya kula njiani au taxi akifika.

Ndo maana waswahili wakasema safari ni hatua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani hizo kampuni hazina refund/compensation policies kama uki-miss flight?

Kwa mabasi hayana refund, airline inategemea ticket uliyokata. Kama ni ya offer inategemea na policy za kampuni husika. Ila mara nyingi hurudishiwi hela bali kuna gharama za kupewa ticket nyingine. Change fee + difference of fair price.
 
Back
Top Bottom