Kuacha kuongeza mshahara ni kosa kubwa

Kuacha kuongeza mshahara ni kosa kubwa

Wakati mnaongezwa mishahara sisi wa vijijini tusioajiriwa na serikali tunaongezwa nini!?
Anzisha uzi wako ili upewe jibu na serikali yako ya ccm
Kukaa karibu na waridi mnaanza kunukia... Kudhani nyie tu ndio muhimu.. muongezwe mishahara..
Swala sio kwamba watumishi ni muhimu au sio muhimu infact kiuhalisia watumishi ni muhimu maana kama sio watumishi wenda hata mchepuko wako ungefia leba.

Pia kuongeza mishahara ni swala ambalo lipo kisheria.
Sisi huku kijijini tunataka dawa, barabara, huduma za elimu na masoko. Hatujawahi kuongezwa mishahara tangu uhuru.. nyie kunyimwa miaka hii michache imekuwa nongwa!?
Sasa kama hamna dawa ndio muda mnatakiwa muiondoe madarakani serikali ya ccm.
Plus ni sisi ambao huwa hatuongezwi kitu tinaichangia serikali hiyo hiyo ili iwaongeze mishahara...
Na hao ambao wanataka kuongezewa ndio ambao wanafanya kazi ili wewe upate huduma kama za afya ulinzi elimu na kilimo!! na wasipolipwa wewe hutapata huduma nzuri.
 
Hiyo bei iliyokuwa stabilized ni ya kitu gani? Yawezekana huishi Tz uko UK maana hapa Tanzania pamoja na kutopandisha mishahara ya wafanyakazi bei za huduma na bidhaa zimeendelea kupanda vile mfano mwaka 2015 , mfuko wa saruji hapa kwetu ulikwa ukiuzwa 15,000, lakini leo 18,500. Kilo ya sukari ilikuwa 1600, leo ni 3200 hadi 3500. Bati la Msauzi lilikuwa likiuzwa pic moja 18000 leo ni 21000, Mbao ziliuzwa 4000, leo ni 7500, chumba cha kupanga kilikuwa 15000 per month leo ni 20,000. Baadhi dawa na huduma za matibabu zilikuwa zikigharamiwa na mfuko wa bima, leo zimeondolewa na hivyo mwanachama atalazmika kulipia kwa pesa yake toka mfukoni! Watoto wadogo chini ya miaka 5 walikuwa wakitibiwa bure, leo wazazi wanatakiwa kugharamia matibabu! Haya yote na makali mengine yanaongezeka huku mshahara wa wafanyakazi uko palepale! Hivyo tusilazmishe watu kuamini mambo yasiyo na uhalisia ili kutetea waovu wasiondolewe madarakani!
Watanzania wanapenda kuchezewa gemu za kitoto sana kama ilivyokuwa inafanyika awali wanashindwa kuelewa ya kwamba ni bora zaidi kustabilise bei za kiuduma na vyakula kuliko kuongeza mishahara mf UK salary per 8 hrs ni pounds 12 na pesa nakiwango hiki kimedumu kwa zaidi ya muongo mmoja sasa with no changes ninachotaka kusema hapa ni kwamba serekali inaweza kuongeza mshahara at the same time ikaongeza bei petrol kwa shs 75 ikakuuzia vocha kwa mia 5 ila ikakupunja muda wa maongezi kufidia hili watu wakabaki wanacheka kupanda mshahara kama mazuzu bila kufahamu maumivu yanakuja kwa njia gani #JPM,#CHACHU_OMBARA waone
 
pound 12 kwa 8 hrs ni sawa na hela ngapi za kitanzania? Mtanzania huyu pamoja na kulipa kodi lakini lazima atafute hela nyingine ya kununua maji, kuzoa taka, ulinzi wa sungusungu, kuhonga polisi kwa makosa iliyobandikiwa, na kununua dawa maduka ya dawa. Mfumko wa bei za chakula unapokuwa chini lazima pia uangalie gharama za uzalishaji wa chakula kwa mkulima. Kama bei ya mazao iko chini kuliko bei ya pembejeo na kilimo utakuwa unatengeneza tatizo lingine baya kwa 80% ya watu wanaotegemea kilimo. Maana yake ni sawa na kuwabaka wakulima na wafugaji.
 
Mbona madaraja wafamyakazi wanaostahili wanapandishwa! Mwaka jana mwezi wa Mei walipandishwa wanaostahili na mwaka huu wamepandishwa au wewe unataka upandishwaji holela wale wanaostahili waachwe na wapandishwe wasiostahili?

Sawa serikali inakusanya kodi, jaribu kudadavua kwa kusoma bajeti kuu tu utaona kuwa mishahara na ulipaji wa madeni yaliyoiva unachukua zaidi ya nusu ya makusanyo. Hicho kinachobakia ndicho kinapelekwa kwenye huduma za afya, elimu miundombinu nk ili sasa kuongeza uwezo zaidi wa mapato ya kodi. Unafikiri ukiongezwa kiholela mshahara bei za vitu zitabakia jinsi zilivyo? Nakwambia tunaweza kuwa kama Zimbabwe. Unajua kitu kinaitwa hyper inflation?
Hatukuwa Kama Zimbabwe wakati wa Nyerere, mwinyi, Mkapa na kikwete ndio tuwe Leo wakati wa mzee JPM? Hii inamaana kuwa hata miaka 5 ijayo hali kwa wafanyakazi zitabaki zilezile Kama tutamchagua JPM maana ujenzi wa miundombinu bado unaendelea
 
Hiyo bei iliyokuwa stabilized ni ya kitu gani? Yawezekana huishi Tz uko UK maana hapa Tanzania pamoja na kutopandisha mishahara ya wafanyakazi bei za huduma na bidhaa zimeendelea kupanda vile mfano mwaka 2015 , mfuko wa saruji hapa kwetu ulikwa ukiuzwa 15,000, lakini leo 18,500. Kilo ya sukari ilikuwa 1600, leo ni 3200 hadi 3500. Bati la Msauzi lilikuwa likiuzwa pic moja 18000 leo ni 21000, Mbao ziliuzwa 4000, leo ni 7500, chumba cha kupanga kilikuwa 15000 per month leo ni 20,000. Baadhi dawa na huduma za matibabu zilikuwa zikigharamiwa na mfuko wa bima, leo zimeondolewa na hivyo mwanachama atalazmika kulipia kwa pesa yake toka mfukoni! Watoto wadogo chini ya miaka 5 walikuwa wakitibiwa bure, leo wazazi wanatakiwa kugharamia matibabu! Haya yote na makali mengine yanaongezeka huku mshahara wa wafanyakazi uko palepale! Hivyo tusilazmishe watu kuamini mambo yasiyo na uhalisia ili kutetea waovu wasiondolewe madarakani!
Nakubaliana sana na wewe mazao yakanayo na kilimo mbao vyakula sukari bei yake mara nyingi sana hutegemeana na wingi wa uzalishaji wa mazao husika duniani kote lakini serekali za nchi husika hukaa chini na kuona ni jinsi gani ya kufanya ili mwananchi asiumie sana kwenye cement embu tuvuteni subra nyerere dam ikamilike au aongeze mshahara na apandishe bei za mafuta ? chaguo ni letu
 
Maximum capacity utilization huwa haifikiwi wakati wa mwanzo wa biashara, hata wewe ukifungus duka leo hii utapata wateja wachache lakini baada ya miaka kadhaa biashara yako itskuwa na wateja wengi. Ndio maana kuna business plan.
Nikuulize hizo ndege zinaenda tupu bila abiria? Nauli wanayolipa kuna kodi ya serikali yaani VAT, airport tax; pia ndege inatumia mafuta ambayo yanalipiwa kodi kadhaa, vyakula ndani ya ndege vinanumuliwa toka local supplers, wafanyakazi ndani ya ndege, ardhini airpirt kama wa wabeba mizigo, wakata tiketi, walinzi, waomgoza ndege yote haya ni ongezrko la ajira ambapo mwisho wa siku wanafanya manunuzi ya bidhaa kwa hao unaosema hawajawahi kupanda ndege hivyi kusababisha increased demand ya wanachozalisha na pia kupato zaidi. Watalii wanatumia ndege kwa usafiri wa ndani hiyo nayo inaongexa kipato ktk uchumi wa ndani.
Kabla ya corona ATCL Zilikuwa inaenda nje ya nchi kama Comoro, Kenya, Rwanda nk pua kulukuwa na mpango wa kwemda China na india hayo huyaoni? Safari za nje zinaigiza pesa za kigeni hivyo kuchangia kustabilise shilingi.

Ukianalye backward and forward ya uwepo wa ndege zilizonunuliwa utaona manufaa makubwa sana lakini kwa kuwa mnakariri kama kasuku anachawaambia Lissu ndio maana mnaona ndege hazi a manufaa. Niwaambie tu serikali i kuna planners na wachumi wazuri tu ambao wanapanga mioango ya nxhi hii vizuri usufikiri Rais aluamua tu kununua ndege.
Unayoyaona lei ni matokeo ya Tanzania Development Vision 25 iliyoasisiwa mwaka 1999.

Sasa hivi wakulima wa mikoa yote wanauza mazao yao Dsm sababu ya kuboreshwa miundombinu ya ndege, barabara, reli mambo mliyokaririshwa kuwa ni maendeleo ya vitu. Ndizi za Ngara, nyanya za Songea, dagaa wa kugoma, mchele wa Mpanda, matikiti ya Rukwa, samaki wabichi wa Mwanza, nk yanaletwana kuuzwa Dar.

Nakushauri tafuta mchumi akupige shule kidogo kuhusu abc za uchumi.
Miundombinu na service sector ndiyo key factor ya ukuaji wa kasi wa uchumi wowote ule sababu unafungua potential wealth zilizoko ndani ndani ziweze kuchakatwa na kufikishwa sokoni katika miji au nje ya nchi.
Hayo Mapato yote unayoyasema yangeweza kupatikana kutoka kwa wasafirishaji wengine binafsi Kama precision air, coastal, eureca, superjet, nk badala ya serikali kuacha jukumu lake la msingi la kuhudumia watumishi wake na kukimbilia kufanya biashara. Nani anaishauri vibaya serikali?
 
Nakubaliana sana na wewe mazao yakanayo na kilimo mbao vyakula sukari bei yake mara nyingi sana hutegemeana na wingi wa uzalishaji wa mazao husika duniani kote lakini serekali za nchi husika hukaa chini na kuona ni jinsi gani ya kufanya ili mwananchi asiumie sana kwenye cement embu tuvuteni subra nyerere dam ikamilike au aongeze mshahara na apandishe bei za mafuta ? chaguo ni letu
Mkuu huko kote, ccm na serikali yake wameshashindwa! Wapishe tu wenye mawazo mbadala watuvushe tulipokwama! CCM na serikali yake wamekuwa hawajui kwamba kukaa kando miaka 5 kunaweza kuwasaidia sana kujitathmini na kujipanga upya kuliko kujipanga wakiwa madarakani! Hata katika mechi ya mchezo ni vigumu mno kwa mchezaji kuyaona makosa yake na kujisahihisha , lakini yule aliyeko nje ya uwanja ndo huyaona vema makosa ya walio ndani uwanja!
 
NA IPOSIKU MISHAHARA ITASITISHWA RASMI KWA KIPINDI FLANI, ILIFEDHA HIYO IKATEKEREZE MIRADI YA MAENDELEO KWA MANUFAA YA WATANZANIA WOTE. MAENDELEO SIO KUONGEZA MISHAHARA . SAWAAA, SAAWAA?????
Inawezekana, aliwahi kusema kwenye kampeni zake hakutoa ahadi ya kupandisha mishahara ya watumishi. Je, safari hii umeshasikia ahadi Kama hiyo?
 
Hela hazimwagwi tu katika uchumi bali zinategemea ukuaji wa uchumi husika . Kama ukuaji wa pesa katika mzunguko ni mkubwa kuliko ukuaji wa uchumi kutatokea ongezeko kubwa la bei za bidhaa na huduma hivyo ongezeko halitakuwa na faida yeyote kwa mfanyakazi na wananchi na utarudi hapa kulialia kuwa bei ziko juu. Pili thamani ya shilingi kulinganisha na Dola au Euro na pesa zingine za nje itashuka na kuchochea zaidi uporomokaji wa shilingi.

Tatu, hizo flyover, miundombinu na ndege unazoona hazifai kwa uelewa wako wa uchumi sio sahihi; kwani iujenzi wa miundombinu (public works) unachochea ongezeko la ajira na pesa mtaani hivyo kuongeza demand ya vitu mbalimbali na hivyo kufanya uzalishaji wa bidhaa na huduma uongezeke na kupelekea kipato mtaani kuongezeka.

Hayo unayoita naendeleo ya vitu kiuhalisia ndiyo maendeleo ya watu. Sasa hivi DSM tunakula matikiti yanayotoka Sumbawanga kwa sababu ya miundombinu ya barabara na masoko iliyojengwa hivyo kufanya pesa ya wanadsm kutiririka mpaka ndani kabisa remote area; kama barabara za kuunganisha mikoa na wilaya zisingejengwa mazao toka remote areas ya Tanzania yasingefika sokoni Dar au kuuzwa nchi za nje. Leo hii nyama inachinjwa Dodoma na kupelekwa uarabuni ni kwa sababu barabara, viwanja ya ndege vimejengwa hivyo kuchochea ukuaji wa demand ambao unapelekea ukuaji wa uzalishaji katika sekta husika moja kwa moja na pia indirectly katika sekta zingine zinazosapoti sekta husika mfano kama nyumba za wageni, baa za pombe, ukahaba, saluni za urembo, sekta za vifungashio, uchukuzi, dizeli na petroli nk.

Kama unalinganisha pesa za wizi na ufisadi zilizokuwa zinaibwa na wafanyakazi wa serikali na kuja kumwagwa mitaani kupitia matanuzi na maendeleo binafsi hizo kwa sasa hazipo na hazitarudi kamwe. Pesa hizo hizo sasa ndizo serikali inazielekeza katika ujenzi wa miundombinu, zahanati, hospitali, na huduma zingine za kijamii. Mambo ya misheni tawni hayataruhusiwa tena kwa sababu wizi unaumiza wengi na kufaidisha wachache. Hivyo kama ulikuwa unafaidika na mnyororo wa wizi, jipange katika shughuli halali iwe kujiajiri au kuajiriwa.

Tarehe 28 Oktoba tukampigie kura Magufuli na wabunge na madiwani wa CCM ili aendelee kuipaisha Tanzania. Kwa kasi yake nina hakika hadi kufikia 2025 tutakuwa tumeingia higher middle income country status.
Duuuh! ama kweli tumepatwa! haya uliyoandika yanaendana kweli na hali halisi ya Watz!? Miradi inaajiri watu wachache sana ukilinganisha na demand ya ajira nchini. Lazima ifanyike juhudi za maksudi ili kuinua nyanja nyingine za kuzalisha ajira na siyo kuangalia tu upande mmoja wa miundo mbinu.
Tusipofanya hivyo, tutaishia kuiona miundombunu hii kama "white elephants" za Zaire ya zamani. Yaani madude makubwa katikati ya Watu maskini wasiofaidi kabisa midude husika! Tafakari
 
Hivi umeshawahi kujiuliza madhara yanayoweza kuipata mifuko ya hifadhi ya Jamii kwa kutoongezwa mshahara Wafanyakazi na pia kutoajiriwa Wafanyakazi wapya kwa muda mrefu!? Mifuko ya hifadhi ya jamii imeweka kanuni za kupata viwango vya malipo ya pensheni na mafao mengine kulingana na makadirio yanayoangalia mambo yafuatayo:
1. Ukuaji wa Uchumi
2. Ongezeko la ajira litalaoongeza wanachama wa Mifuko.
3. Umri wa kuishi kwa jamii ya Wafanyakazi.
4. Ukuaji wa mapato ya mfuko kulingana na makato toka mishahara ya Wanachama.

Sasa, iwapo uchumi unalegelega na ajira zinapungua, lakini wakati huo huo kanuni za malipo ya mafao zilizoandaliwa miaka mingi iliyopita (kwa matarajio ya uwepo wa mapato mazuri ya mifuko kutokana na ongezeko la Wanachama) zikibaki vile vile, Taifa litajikuta likitumbukia katika mgogoro wa vikokotoo kwani Mifuko itakuwa inashindwa kulipa mafao na gharama nyingine kama walivyowaahidi Wanufaika. Hii italeta hali tete miungoni mwa jamii kwani hakuna atakayeelewa sababu hizi wakati wanaelezwa kuwa Uchumi unakuwa na wanaona miradi mikubwa inafanyika nchini.

Jambo kubwa hapa ni kufanya miradi ya maendeleo kulingana na pato la Taifa huku tukiangalia ustawi wa Jamii zetu. Kufanya miradi mingi ndani ya muda mfupi kwa kukimbizana na matakwa ya Kikatiba ya Uongizi wa miaka 10 kwa Rais mmoja itasababisha wananchi kushindwa kuhimili ugumu wa Maisha na inaweza kuleta crisis kubwa sana.

Tufanye mambo kwa ku-balance, Maendeleo yafanyike kwa uwiano sawa na uboreshaji wa maisha ya Watu.
 
mfano, kwa kuhamisha serikali kutoka DSM kwenda Dodoma kutasaidiaje kukuza uchumi wa nchi? Je, ilikuwa lazima kuhamia dodoma, kujenga reli ya kisasa, kujenga bwawa la umeme, kununua ndege 15, kujenga viwanja vya ndege na kununua meli kwa wakati mmoja katika nchi yenye aina ya uchumi kama wetu?
 
Inawezekana, aliwahi kusema kwenye kampeni zake hakutoa ahadi ya kupandisha mishahara ya watumishi. Je, safari hii umeshasikia ahadi Kama hiyo?
AWE AMETOA AU HAJATOA, SISI TUNATAKA MAENDELEO YATAKAYOZALISHA AJIRA ZA WENGI SIO WEWE MLINZI WA SOKO, UNAYEJALI TUMBOLAKO TUUU. HATA WATUMISHI WAKIONGEZEWA MISHAHARA, WALA HAYO SIOMAENDELEO YA UHAKIKA. KUMBUKA MISHAHARA IKIONGEZWA UJUE NA KODI NA BIDHAA ZA MADUKANI ZINAPANDAA PIA.
 
Jamii huwa inapata fedha zao kwenye mzunguko kupitia wenzao wenye ajira, kwakuwa wao hawana njia yoyote ya kupata hela kutoka hazina moja kwa moja. Serikali inatoa fedha hazina kuwalipa watumishi, makandarasi na watoa huduma. Baada ya makundi haya kulipwa ndio wanazipeleka hela hizo kwa wananchi kwa kufanya manunuzi, kutoa michango Kama ya harusi na kuwatumia ndugu zao hela za matumizi na kuufanya mzunguuko wa hela uwepo kwenye jamii.

Ukubwa wa mzunguuko wa pesa unategemea pia ukubwa wa manunuzi ya waliopewa pesa hizo kutoka hazina, yaani wafanyakazi na ukubwa wa manunuzi utakaofanywa na wafanyakazi utategemea pia ukubwa wa malipo waliopewa kutoka hazina, yaani na mwajiri.

Idadi ya watu kwenye ngazi ya familia, mitaa, Kijiji, kata, wilaya, mkoa na taifa inayohitaji pesa huwa inaongezeka kila mwaka, Hivyo, usipowaongezea hela watumishi kwa miaka mitano maana yake watu wote wakioongezeka kwa kipindi hicho Cha miaka 5 watanyang'anya hela hiyo hiyo ya watu waliokuwepo miaka 5 iliyopita na kuufanya mzunguko wa hela uwe mdogo na maisha kuonekana kuwa magumu.

Ili mzunguko wa pesa uwe mzuri na maisha kuwa nafuu ni lazima yafuatayo yafanyike kila mwaka:

1. Ajira ziongezeke kila mwaka pia kama vile jamii inavyoongekeza pia.
2. Mishahara iongezwe kila mwaka pia Kama jamii inavyoongekeza pia.
3. Watoa huduma serikalini walipwe kwa wakati na waongezeke pia kila mwaka.
4. Juhudi za kuzuia uongezeko la watu lipewe kipaumbele.
6. Uzalishaji kwenye ngazi ya kata, Kijiji, kata, wilaya na taifa lazima uongezeke.
7. Masoko ya uhakika ya bidhaa lazima yawepo na yaongezeke.

Kama mambo haya yasipofanyika usije ukatafuta mchawi, maana mtoto anapolia njaa huwezi kumwambia subiri flyovers zinajengwa, mzazi anapokosa ada ya mtoto hawezi kusubiri ndege zinunuliwe kwanza. Gari yako inapokosa mafuta huwezi kusubiri barabara iishe. Na hii ndiyo maana kila mtumishi bila kuangalia anafanya kazi gani huwa anafurahia sherehe za May day kila mwaka ikiwa na matarajio kuwa huenda kutakuwa na nyongeza.

Kama ukiona mfanyakazi hata awe housegirl ambae hajalipwa au hajaongezewa mshahara anakuchekea ujuwe wazi kuwa anakudanganya.
#NIYEYE2020
 
AWE AMETOA AU HAJATOA, SISI TUNATAKA MAENDELEO YATAKAYOZALISHA AJIRA ZA WENGI SIO WEWE MLINZI WA SOKO, UNAYEJALI TUMBOLAKO TUUU. HATA WATUMISHI WAKIONGEZEWA MISHAHARA, WALA HAYO SIOMAENDELEO YA UHAKIKA. KUMBUKA MISHAHARA IKIONGEZWA UJUE NA KODI NA BIDHAA ZA MADUKANI ZINAPANDAA PIA.
Hiyo ni model gani ya uchumi, au unajisemea tu kutoka kichwani mwako. Hebu tuambie nadharia ya namna bwawa la umeme litakavyoongeza ajira tofauti na kama ungetumia gesi ya msimbati, tuambie namna kuhamia dodoma kulivyonyanyua uchumi wa taifa, tuambie namna kutokuongeza mishahara na kupandisha madaraja kunavyoongeza uchumi wa taifa. Ni kivipi uchumi wabwatu wa mtwara utapata ahueni kwa Serikali kuhamia Dodoma.
 
Duniani kote ni hivoo
 
Duniani kote ni hivoo
Ndio maana Kuna wanaopenda utawala wa majimbo. Utawala wa majimbo unazuia kuchukua Kodi ya kurosho ya mtwara kwenda Kutumika kujenga uwanja wa ndege chato. Na Kodi ya pamba ya Mwanza kwenda kujenga barabara zinazounganisha kata na kata Kilimanjaro. Kama uwanja wa chato Ni muhimu Basi serikali ya Jimbo ndiyo itakayoamua na kutumia rasilimali za Jimbo kuujenga. Kazi ya Serikali kuu itakuwa kujenga viwanja vya ndege vya mikakati ya kitaifa na kimataifa tu Basi.
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
 
Attachments

  • VID-20201017-WA0008.mp4
    12.6 MB
Utawala
Ndio maana Kuna wanaopenda utawala wa majimbo. Utawala wa majimbo unazuia kuchukua Kodi ya kurosho ya mtwara kwenda Kutumika kujenga uwanja wa ndege chato. Na Kodi ya pamba ya Mwanza kwenda kujenga barabara zinazounganisha kata na kata Kilimanjaro. Kama uwanja wa chato Ni muhimu Basi serikali ya Jimbo ndiyo itakayoamua na kutumia rasilimali za Jimbo kuujenga. Kazi ya Serikali kuu itakuwa kujenga viwanja vya ndege vya mikakati ya kitaifa na kimataifa tu Basi.
Utawala wa majimbo ni mbinu mpya ya kuwaruhusu mabeberu kuzigwa inchi zinazoendelea na zilizoendelea. Kwa mfano hapa kwetu Tanzania kuna amani na utulivu na umoja. Utawala wa majimbo wa nini ??
 
Ili ccm ife kila Jambo utokea kwa sababu,
Maendeleo sio kikwazo cha kukiuka katiba
 
Back
Top Bottom