kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,197
- 16,868
Jamii huwa inapata fedha zao kwenye mzunguko kupitia wenzao wenye ajira, kwakuwa wao hawana njia yoyote ya kupata hela kutoka hazina moja kwa moja. Serikali inatoa fedha hazina kuwalipa watumishi, makandarasi na watoa huduma. Baada ya makundi haya kulipwa ndio wanazipeleka hela hizo kwa wananchi kwa kufanya manunuzi, kutoa michango Kama ya harusi na kuwatumia ndugu zao hela za matumizi na kuufanya mzunguuko wa hela uwepo kwenye jamii.
Ukubwa wa mzunguuko wa pesa unategemea pia ukubwa wa manunuzi ya waliopewa pesa hizo kutoka hazina, yaani wafanyakazi na ukubwa wa manunuzi utakaofanywa na wafanyakazi utategemea pia ukubwa wa malipo waliopewa kutoka hazina, yaani na mwajiri.
Idadi ya watu kwenye ngazi ya familia, mitaa, Kijiji, kata, wilaya, mkoa na taifa inayohitaji pesa huwa inaongezeka kila mwaka, Hivyo, usipowaongezea hela watumishi kwa miaka mitano maana yake watu wote wakioongezeka kwa kipindi hicho Cha miaka 5 watanyang'anya hela hiyo hiyo ya watu waliokuwepo miaka 5 iliyopita na kuufanya mzunguko wa hela uwe mdogo na maisha kuonekana kuwa magumu.
Ili mzunguko wa pesa uwe mzuri na maisha kuwa nafuu ni lazima yafuatayo yafanyike kila mwaka:
1. Ajira ziongezeke kila mwaka pia kama vile jamii inavyoongekeza pia.
2. Mishahara iongezwe kila mwaka pia Kama jamii inavyoongekeza pia.
3. Watoa huduma serikalini walipwe kwa wakati na waongezeke pia kila mwaka.
4. Juhudi za kuzuia uongezeko la watu lipewe kipaumbele.
6. Uzalishaji kwenye ngazi ya kata, Kijiji, kata, wilaya na taifa lazima uongezeke.
7. Masoko ya uhakika ya bidhaa lazima yawepo na yaongezeke.
Kama mambo haya yasipofanyika usije ukatafuta mchawi, maana mtoto anapolia njaa huwezi kumwambia subiri flyovers zinajengwa, mzazi anapokosa ada ya mtoto hawezi kusubiri ndege zinunuliwe kwanza. Gari yako inapokosa mafuta huwezi kusubiri barabara iishe. Na hii ndiyo maana kila mtumishi bila kuangalia anafanya kazi gani huwa anafurahia sherehe za May day kila mwaka ikiwa na matarajio kuwa huenda kutakuwa na nyongeza.
Kama ukiona mfanyakazi hata awe housegirl ambae hajalipwa au hajaongezewa mshahara anakuchekea ujuwe wazi kuwa anakudanganya.