Kuacha, Kuachana, Kuachwa, Kuachishwa

Walidumu ama walivumilia? Na siku hizi magumu ya ndoa hayavumiliki. Mfano uasherati hauvumiliki pia kwa sababu kuna magonjwa. Nyakati zingine hizi mkuu.
Uvumilivu katika ndoa umeenda wapi? Ukiacha huyo utaempata hana mapungufu?
::
Tuvumiliane katika mahusiano,kama kila mmoja atakuwa ktk ndoa mguu mmoja ndani mwingine nje basi huo ni uhusiano wa mashaka.
::
Wazee wetu walidumu ktk mahusiano(ndoa) kwa miaka zaidi ya 30 au 50 haikuwa na maana walikuwa perfect match,la! Walichukuliana mapungufu.
::
Sikubaliani na haka ka mchezo kama kupata na kuacha.Unaweza lamba sumu ukaenda nayo kwa mwingine hatimaye ni janga la maisha.
%
 
Kwa wale wanaoiamini Biblia, hebu chekini hii - hasa hapo penye wino mwekundu:

[h=1]Marko 10 : 1-52[/h]10.1 Akaondoka huko akafika mipakani mwa Uyahudi, na ng'ambo ya Yordani; makutano mengi wakakutanika tena wakamwendea; akawafundisha tena kama alivyozoea.
10.2 Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamwuliza, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe? Huku wakimjaribu.
10.3 Naye akajibu, akawaambia, Musa aliwaamuru nini?
10.4 Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha.
10.5 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii.
10.6 Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.
10.7 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
10.8 na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
10.9 Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
10.10 Hata nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza habari ya neno hilo.
10.11 Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake;
10.12 na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini.

Marko 10 : 1-52 sw - Swahili Union Bible
 
Kama ni hivyo, bora usiingie kwenye mahusiano kabisa ili usije kuachwa au hata kuacha

Paulo anakubaliana na wewe hapa:
Ninayowaambieni sasa ni mawaidha, si amri. 7 Ningependa watu wote wawe kama mimi nilivyo; lakini kila mmoja anacho kipaji chake kutoka kwa Mungu; mmoja kipaji hiki na mwingine kile.8 Basi, wale ambao hawajaoana na wale walio wajane nawaambia kwamba ni vema kuendelea kuwa kama mimi nilivyo. 9 Hata hivyo, kama mtu hawezi kujizuia basi, na aoe; maana ni afadhali zaidi kuoa kuliko kuwaka tamaa.
10 Kwa wale waliooa ninayo amri, tena si yangu, ila ni ya Bwana: mke asiachane na mumewe;11 lakini kama akiachana naye, basi abaki bila kuolewa; ama la, apatanishwe na mume wake. Mume naye asimpe talaka mkewe.

1 Wakorintho 7: 6-11

1 Wakorintho 7 Swahili NT

Na huyu jee una maoni gani kwake? Companero

I hold it true, whate'er befall;
I feel it, when I sorrow most;
'Tis better to have loved and lost
Than never to have loved at all.

Alfred Lord Tennyson's poem In Memoriam:27, 1850
 
Na watu smart wanaacha hawaachwi.

Yani unakuta mtu anafanyiwa vituko vya kila aina lakini yumo tu anasubiri hadi atupiwe nguo nje.

Raha sana kuacha hasa kuacha mtu alokuwa anajidai mjanja....unampa makavu live...its over...utasikia eeh unasemaje? Its overrrr. Huku unaangalia reaction usoni. Msisubiri kuachwa mtaja kunywa sumu bure...someni alama za nyakati

Yani atakama mtu alikuwa ana mpango wa kukuacha ukimwahi jua umemmaliza...ataumia forever...yani unakuwa umeshusha pride yake vibaya mmno.

Nyumba kubwa,
Hahaaa haaa nimefurahi kusikia hayo toka kwako. Ila binadam tuna tofautiana sana. Mwingine ukimtangazia kumuacha unashangaa anachekelea badala ya kununa na kukuomba urudi. Mhhh, unaweza kujikuta mwenyewe linakuuma badala ya kufurahia.

Kuachwa au kuacha inategemea tu nani mwenye haki kwenye hilo. Yaani ukinitangazia kuniacha, wakati ulishaniboa nilikuwa nakuvumilia tu, yaani mie nitafurahi tu. Kwa wengine kuachwa ndo safi. Mtu kama mie kumuacha mtu najisikia guilty kuwa nimemuumiza. Ila akitangaza yeye kuniacha - mhhh nachekelea.

Yaani haya maisha we acha tu. Hakuna kanuni anayotumika kwa watu wote. Yaani usidanganywe kuwa kuacha ndo kutamu. Kwa wengine kuachwa ndo kutamu kwani wanavumilia tu.
 
Na huyu jee una maoni gani kwake? Companero

I hold it true, whate'er befall;
I feel it, when I sorrow most;
'Tis better to have loved and lost
Than never to have loved at all.

Alfred Lord Tennyson's poem In Memoriam:27, 1850

Rationalizing avoidable pain!
 
Nyumba kubwa,
Hahaaa haaa nimefurahi kusikia hayo toka kwako. Ila binadam tuna tofautiana sana. Mwingine ukimtangazia kumuacha unashangaa anachekelea badala ya kununa na kukuomba urudi. Mhhh, unaweza kujikuta mwenyewe linakuuma badala ya kufurahia.

Kuachwa au kuacha inategemea tu nani mwenye haki kwenye hilo. Yaani ukinitangazia kuniacha, wakati ulishaniboa nilikuwa nakuvumilia tu, yaani mie nitafurahi tu. Kwa wengine kuachwa ndo safi. Mtu kama mie kumuacha mtu najisikia guilty kuwa nimemuumiza. Ila akitangaza yeye kuniacha - mhhh nachekelea.

Yaani haya maisha we acha tu. Hakuna kanuni anayotumika kwa watu wote. Yaani usidanganywe kuwa kuacha ndo kutamu. Kwa wengine kuachwa ndo kutamu kwani wanavumilia tu.

Huko sio kuacha wala kuachwa - ni kuachana
 
hahahaa damn strait!!! he who has the last laugh has the power. mapenzi ni power struggle btwin a man and a woman. ndio maana unatakiwa ugegede na kumbwaga demu...wewe ndio utakuwa umeshinda the power battle.
mmmh shauri lako kama ujagegedwa wewe babaa
 
hivi wote tukiacha, nani ataachwa?
Lazima awepo anayeacha na kuachwa.

Mapenzi ya mashindano bora kuachana na mapenzi kabisa.
unajua hata mnapoachana lazima **** mmoja alianzisha mpaka mkaachana.......hapa mimi naona kuna kuacha na kuachwa, kuachana ni hali ya wote wawili (muacha na muachwa) kukubali matokeo, lol!
 
Huko sio kuacha wala kuachwa - ni kuachana

Companero,
OK labda sijakuelewa. Mie naamini yule anayekuwa first mover ndo anayeacha. Sasa kuna situation anayeachwa hata kama bado anapenda - huikubali hali ile ya kuachwa mara na aka-move on.
Yaani furaha ya kuacha ni pale unapoona kuwa uliyemuacha kaumia kwa kuachwa?? labda kama hiyo ndo tafsiri yako...
 
Rationalizing avoidable pain!

Cost-benefits analysis inamuonyesha kuwa benefits ni nyingi kuliko costs zitokanazo

Mie I will go further na kusema, bora hata umtokee na ukataliwe kuliko kutojaribu kabisa
 
Hivi msingi wa thread hii ni nini hasa? huu ndio Uhuru wa kutoa maoni? ni kwa nini usitueleze faida za kutoachana na namna ya kuondoa vitu vinavyosababisha utengano? kweli Shetani anazidi kupata mamlaka kwa watu dhaifu.

Niko Tayari kuachwa hata mara 1000 kuliko kumuacha mtu ninayempenda, ili iweje? siwezi kuchezea feelings za binadamu mwenzangu.

Ukiishi kwa upanga na utakufa kwa Upanga tu, acha hapa na pale utaachwa wewe vile vile.
 
Kwa wale wanaoiamini Biblia, hebu chekini hii - hasa hapo penye wino mwekundu:

Marko 10 : 1-52

10.1 Akaondoka huko akafika mipakani mwa Uyahudi, na ng'ambo ya Yordani; makutano mengi wakakutanika tena wakamwendea; akawafundisha tena kama alivyozoea.
10.2 Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamwuliza, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe? Huku wakimjaribu.
10.3 Naye akajibu, akawaambia, Musa aliwaamuru nini?
10.4 Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha.
10.5 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii.
10.6 Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.
10.7 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
10.8 na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
10.9 Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
10.10 Hata nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza habari ya neno hilo.
10.11 Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake;
10.12 na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini.

Marko 10 : 1-52 sw - Swahili Union Bible
Ni nini Msingi wa kuleta neno hili hapa? i don't get ur point.
 
kukubali kuachwa ni ujinga
ondoka mwenyewe mapema
na usirudi tena
kama mahusiano yalikuwa yakudumu yasingekupa maswali kichwani.ukishaona kitu kinakupa doubt kichwani ,hakielewekieleweki kimbia
 
kukubali kuachwa ni ujinga
ondoka mwenyewe mapema
na usirudi tena
kama mahusiano yalikuwa yakudumu yasingekupa maswali kichwani.ukishaona kitu kinakupa doubt kichwani ,hakielewekieleweki kimbia

Unataka iphone?
 
hahahaa damn strait!!! he
who has the last laugh has the power. mapenzi ni power struggle btwin a
man and a woman. ndio maana unatakiwa ugegede na kumbwaga demu...wewe
ndio utakuwa umeshinda the power battle.

umebalehe lini?
 
Hivi msingi wa thread hii ni nini hasa? huu ndio Uhuru wa kutoa maoni? ni kwa nini usitueleze faida za kutoachana na namna ya kuondoa vitu vinavyosababisha utengano? kweli Shetani anazidi kupata mamlaka kwa watu dhaifu.

Niko Tayari kuachwa hata mara 1000 kuliko kumuacha mtu ninayempenda, ili iweje? siwezi kuchezea feelings za binadamu mwenzangu.

Ukiishi kwa upanga na utakufa kwa Upanga tu, acha hapa na pale utaachwa wewe vile vile.
helo my swiit brother...back to topic..well huyo mtu unampenda kama yeye hakupendi na anakufanyia vituko utabaki tu..? si bora ujiachie kwa mwingine anayekupenda ..? kwanini usubiri meli uwanja wa ndege na bandarini zimejaa tele bwana?
kuna watu kwenye mahuisiano wanakera kwa kweli
 
Back
Top Bottom