Kuacha, Kuachana, Kuachwa, Kuachishwa

Kuacha, Kuachana, Kuachwa, Kuachishwa

unajua hata mnapoachana lazima **** mmoja alianzisha mpaka mkaachana.......hapa mimi naona kuna kuacha na kuachwa, kuachana ni hali ya wote wawili (muacha na muachwa) kukubali matokeo, lol!
ni kweli FP ASSUME UMEMFUMANIA MPENZI WAKO UKAAMUA KUACHANA NAE IN REAL SENSE HAPO NANI KAMUACHA MWENZIE
WEWE ULOKUTA HIYO HALI UKAONA HUWEZI KUENDELEA NA MTU ASIE NA ADABU NA FEELINGS ZAKO AU HUYO ALOKUACHA AKAENDELEA KUFUNUA SKETI ZINGINE
 
Last edited by a moderator:
helo my swiit brother...back to topic..well huyo mtu unampenda kama yeye hakupendi na anakufanyia vituko utabaki tu..? si bora ujiachie kwa mwingine anayekupenda ..? kwanini usubiri meli uwanja wa ndege na bandarini zimejaa tele bwana?
kuna watu kwenye mahuisiano wanakera kwa kweli
Hi Mrembo,
Once again pole sana kwa msiba mungu akupe ustahamilivu...

Back to topic u nail it, kwa msingi huu uliojenga wewe hoja nakubaliana na wewe kama mahusiano yapo katika hali hii, imebidi hapa niwe mpole maana umenidhibiti leo kama Tundu Lisu alivyomdhibiti Alluthe Mughwai pale Court of Appeal leo. uko sahihi.
 
ni kweli FP ASSUME UMEMFUMANIA MPENZI WAKO UKAAMUA KUACHANA NAE IN REAL SENSE HAPO NANI KAMUACHA MWENZIE
WEWE ULOKUTA HIYO HALI UKAONA HUWEZI KUENDELEA NA MTU ASIE NA ADABU NA FEELINGS ZAKO AU HUYO ALOKUACHA AKAENDELEA KUFUNUA SKETI ZINGINE
umeona eeeh!
 
Ni nini Msingi wa kuleta neno hili hapa? i don't get ur point.

Utaelewaje ilhali umefunga akili kwa kuhukumu hapa chini?


Hivi msingi wa thread hii ni nini hasa? huu ndio Uhuru wa kutoa maoni? ni kwa nini usitueleze faida za kutoachana na namna ya kuondoa vitu vinavyosababisha utengano? kweli Shetani anazidi kupata mamlaka kwa watu dhaifu.

Niko Tayari kuachwa hata mara 1000 kuliko kumuacha mtu ninayempenda, ili iweje? siwezi kuchezea feelings za binadamu mwenzangu.

Ukiishi kwa upanga na utakufa kwa Upanga tu, acha hapa na pale utaachwa wewe vile vile.
 
Cost-benefits analysis inamuonyesha kuwa benefits ni nyingi kuliko costs zitokanazo


Mie I will go further na kusema, bora hata umtokee na ukataliwe kuliko kutojaribu kabisa

Hiyo cost-benefit analysis yenu ni applicable to everyone (universal)?

Huyo jamaa hapo anaugulia tu kwa maumivu, anajaribu ku-make sense out of his broken heart hence the poetic rationalization of pain as inevitable though he knows it is avoidable!
 
Companero,
OK labda sijakuelewa. Mie naamini yule anayekuwa first mover ndo anayeacha. Sasa kuna situation anayeachwa hata kama bado anapenda - huikubali hali ile ya kuachwa mara na aka-move on.
Yaani furaha ya kuacha ni pale unapoona kuwa uliyemuacha kaumia kwa kuachwa?? labda kama hiyo ndo tafsiri yako...

Tahadhari: Kukataa kuachwa huongeza maumivu ya moyo na machungu moyoni yakizidi huua!
 


Utaelewaje ilhali umefunga akili kwa kuhukumu hapa chini?
Kujuwa kwingi mbele giza, nimekuuliza hivyo kwa sababu kitabu cha Marko na kitabu cha Mathayo vyote vinaongelea hiyo sehemu lakini kwa hitimisho tofauti. unidhaniavyo sivyo na leo nilikuwa nimetenga muda asubuhi kwa ajili ya kusoma Bible angalau vitabu viwili kwenye agano jipya. kwahiyo usiniunder estimate na nakijuwa nilichokuuliza.
 
Kujuwa kwingi mbele giza, nimekuuliza hivyo kwa sababu kitabu cha Marko na kitabu cha Mathayo vyote vinaongelea hiyo sehemu lakini kwa hitimisho tofauti. unidhaniavyo sivyo na leo nilikuwa nimetenga muda asubuhi kwa ajili ya kusoma Bible angalau vitabu viwili kwenye agano jipya. kwahiyo usiniunder estimate na nakijuwa nilichokuuliza.

Elewa basi
 
hi mrembo,
once again pole sana kwa msiba mungu akupe ustahamilivu...

Back to topic u nail it, kwa msingi huu uliojenga wewe hoja nakubaliana na wewe kama mahusiano yapo katika hali hii, imebidi hapa niwe mpole maana umenidhibiti leo kama tundu lisu alivyomdhibiti alluthe mughwai pale court of appeal leo. Uko sahihi.
thax bro hivi case imekuaje? Back to topic
ujue moyo wa binadamu bwana ni kiza kinene.. Kila mtu anaingia kwenye maisha ya mwenzake akiwa na malengo tofauti,pia watu tuna style tofauti na pia kila mtu ana tabia zake.
Siamini katika uvulilivu ila nasisitiza uvumilivu katika mambo ya msingi tu ..ila kama mtu hasomeki kimbia kama ipo ipo tu..maisha ni haya haya .mtu amekukuta na meno yako 32 kwa nini aje kuutesa moyo wako na dunia ina mabilion ya watu?
 
Why talk of breaking up badala ya building up?

Mtazamo wangu wa mahusiano mengi yanayovunjika nowadays ni kutokana na mawazo kama yako ya, 'naingia kwenye huu uhusiano ila the first doubt ntakayopata nasepa!'

We should practice open talk..communication is the key!!! Mahusiano mengi yangekuwa yameokolewa...

Neno la busara hilo mkuu, always watu hufikiria mabaya kuliko mazuri ndio maana mambo yanakuwa mambo, kuvunjika mahusiano inatakiwa tuichukulie kama dharula, tatizo ndio hilo uraiani kuna misemo mingi ya ku-discourage mfano ndoa ndoano, yahitaji moyo kuishi kwenye ndoa.
 
Uvumilivu katika ndoa umeenda wapi? Ukiacha huyo utaempata hana mapungufu? :: Tuvumiliane katika mahusiano,kama kila mmoja atakuwa ktk ndoa mguu mmoja ndani mwingine nje basi huo ni uhusiano wa mashaka. :: Wazee wetu walidumu ktk mahusiano(ndoa) kwa miaka zaidi ya 30 au 50 haikuwa na maana walikuwa perfect match,la! Walichukuliana mapungufu. :: Sikubaliani na haka ka mchezo kama kupata na kuacha.Unaweza lamba sumu ukaenda nayo kwa mwingine hatimaye ni janga la maisha. %
nakubaliana na wewe kwa 100%
 
Kuachwa/kuachika ni kubaya kuliko ambavyo tunasema!! Tena mbaya ukute ule upande unaoachwa bado una mapenzi ya dhati kwa upande unaoacha!!! Siku yakikufika hapa ndiyo utajua utamu wake!!! Ndiyo maana siku hizi mapenzi ya dhati yanapotea sana maana mtu anaogopa asijeachwa!! Mguu mmoja ndani mwingie nje!!!
 
Dawa ni kuwa real tangu mwanzo wa mahusiano, tatizo mtu mwanzoni wanapokuwa bado wapya unamwona mtu wako kama nini sijui, akikukosea humwelezi kisa unaogopa atakuonaje sijui matokeo yake ndio hayo yanayokuja ya kuachwa sijui kuachana. kikubwa ni uvumilivu pia kama kuna tatizo unaliongea mapema kabla halijawa kubwa. Unaweza mwanzoni ulikuwa haupo real, huduma unatoa kubwa kuliko uwezo wako, imefika kama mwaka hivi huduma inapungua mbaya zaidi huzungumzi maana na wanaume wengine anapofulia anakosa amani kabisa mbele ya mwanamke na wengine hata kutongoza hawatongozi (ikifikia hatua kama hii lazima mtu ajiulize mbona zamani ilikuwa hivi, but sasa hivi mambo yanakwenda hivi na mbaya zaidi unakuwa mkali)

Bifu lolote linalotokea lazima lina sababu na sababu inatokea kati ya hao hao waliokuwa katika mahusiano though wachache malimbukeni hudanganywa na watu wa nje ikifika mahala halivumiliki inabidi uchukue hatua ya kuachana sasa lakini si ukiona kituko tu PIGA CHINI unless kama umemfumania hapo CHACHA.
 
thax bro hivi case imekuaje? Back to topic
ujue moyo wa binadamu bwana ni kiza kinene.. Kila mtu anaingia kwenye maisha ya mwenzake akiwa na malengo tofauti,pia watu tuna style tofauti na pia kila mtu ana tabia zake.
Siamini katika uvulilivu ila nasisitiza uvumilivu katika mambo ya msingi tu ..ila kama mtu hasomeki kimbia kama ipo ipo tu..maisha ni haya haya .mtu amekukuta na meno yako 32 kwa nini aje kuutesa moyo wako na dunia ina mabilion ya watu?
Kesi inaendelea tena kesho kwa majibizano ya hoja kabla jopo la majaji hawajapanga tarehe ya kusoma hukumu, ila bila ushabiki Mawakili wa Lema Kimogororo, Albert Msando na Tundu Lisu wamembana vilivyo Wakili wa CCM Alluthe Mungwai, wala huitajiki kuwa mjuzi wa sheria kuelewa ni nini Mahakama ya Rufaa watakachokiamuwa.
Smile Checki updates hapa chini huna haja ya kuifuatilia thread yote utaelewa ni nini kilichojili leo ndani dakika 2 mbili tu.
[h=1]Live Feeds: Kutoka mahakama Kuu ya Rufaa Kivukoni - Rufaa ya Lema, Dec 04, 2012[/h]
 
Last edited by a moderator:
kuachwa/kuachika ni kubaya kuliko ambavyo tunasema!! Tena mbaya ukute ule upande unaoachwa bado una mapenzi ya dhati kwa upande unaoacha!!! Siku yakikufika hapa ndiyo utajua utamu wake!!! Ndiyo maana siku hizi mapenzi ya dhati yanapotea sana maana mtu anaogopa asijeachwa!! Mguu mmoja ndani mwingie nje!!!
ni kosa kumuamini mtu 100% aisee hutoamini watu si watu siku hizi
piga maombi kwa sana
 
Natamani Mungu ayaondoe mapenzi kwa wiki nzima halafu nione binadamu watakuaje.
"
Natamani Mungu aiondoe ngono kwa mwaka mzima halafu nione binadamu wataishi vipi.Hasa wale waliofungua ma-guest kwaajili ya ngono tu.
"
Ila namuomba Mungu atupe binadamu ufahamu wa Upendo ili tuishi kama binadamu!
 
ukiachwa halafu ukapata replacement wala haiumi. ngoma usipopata replacement.

Kakudanganya nani kuna replacement itakayokufanya usiumie??........every person is unique the way alivyoumbwa....huwezi mpata exactly kama uliyemuacha.
Utapunguza machungu tu lakini at the end lazima kumbukumbu za uliyempenda zitakatiza ubongoni now and then japo ulimuacha wewe.

Sio kila wakati solution ni kuacha.......
 
mmmh shauri lako kama ujagegedwa wewe babaa

ah wapi...nigegedwe na viumbe dhaifu over my dead body lol. nyie wanawake bwana ujanja wakati mnatongozwa tuu...ila mkishaingia kwenye chumba nguvu zote kwisha.....
 
Back
Top Bottom