Kuacha kazi kumbe kazi!!

Kuacha kazi kumbe kazi!!

Mkuu vingi vilinisukuma...1.Kufanya kazi mazingira mbali na familia wakati kuna umuhimu mkubwa wa mimi kuwepo karibu ili mambo yaende...2.Mazingira magumu ya kazi kwa maslahi duni chini ya manyanyaso makubwa ya mwajiri...3.Kukosa uhuru wa mambo yangu...4.Tangu nimeajiriwa sijawahi ishi maisha ya furaha/peace of mind..........sijawahi juta sababu nachoweza kukitengeneza huku ndo nilichokuwa nakipata kule kwenye ajira...sio kwamba naishi maisha mazuri or labda natoka familia bora..naishi maisha ya kawaida sana,sina hela na familia nayotoka niyakawaida sana...kwangu mimi ckuzote sitaki niishi maisha ya kukosa furaha na kuendeshwaendeshwa na maboss miungu watu na haitakujatokea
Tena kwa Gvt hii, nikuendeshwa hata bila kuzingatia kanuni, afu hakuna kuhoji. Utumwa wachache hatuupendj. Kuishi maisha mapya ni ndoto ya watu wanaohitaji kufanikiwa.
 
mkuu naomba nikushauri baada ya kufatilia Uzi wako kwa siku 2 sasa nimesoma all comments

fanya kitu unachoona kinakupa furaha bila kuangalia hofu za wengine but wao kuwa na hofu juu yako si jambo baya la kukumiza ww au kukufanya usiamue unachotaka et kwa kuwaofia wao

nivigumu kukuelewa ila kadri muda unavyo zidi kwenda wakiona matunda ya maamuzi yako ama kwa hakika watakusifia kwa maamuzi mazuri na yakishujaa...

usiofie kufal
Functional!! Asante mkuu
 
NAFUTA KAULI MKUU. ILA KUNA UMRI UNAFIKA UNAKUA NA UWEZO WA KUCHAGUA YES NA NO KWA WAKATI GANI. EXCUSES MASTER!!
Uko sawa kabisa kuhusu uwezo wa kusema ndiyo/hapana. Ila katika kusema huko ndiyo au hapana hutakiwi kudharau mawazo ya wazazi wako. Kumbuka kuheshimu mawazo ya mtu haina maana ya kukubaliana na mawazo hayo. Lugha unayotumia kuhusu mawazo ya mtu kuna wakati inaweza kuonesha wazi kama unaheshimu au kudharau hayo mawazo.

La muhimu ushaelewa, hapa nilikuwa nakazia tu hii hoja. Kila la heri kwenye mipango yako mkuu.
 
Asante mkuu
 
Huyu amedekezwa na haya ndio matokeo yake wazazi wake watapata tabu sana.
Kama angedekezwa in fact angepumbazika na kazi anayofanya asingeumiza kichwa

Yupo sahihi sana na anacho kiwaza hakuna kitu kibaya kama kufanya shughuli usiyo ipenda ukiangalia sana jamaa ana future ya maisha hataki kuji-frame katika uwalimu tu....
 
Kwaio we mwanaume wa mkoani unataka uache kazi uanze square one au? Iko hivi inakubidi uwe na mradi pembeni wa kukuingizia kipato cha kuweza kujikimu hivyo mradi ukiwa stable hapo unaweza fikiria kuacha kazi, lakini utakapo weza kumudu kuendesha mradi huku unafanya kazi utakua unafanya vitu viwili kwa wakati mmoja hivyo itakua ngumu zaidi kuacha kazi maana unaweza fanya vitu viwili kwa wakati mmoja
 
Kama angedekezwa in fact angepumbazika na kazi anayofanya asingeumiza kichwa

Yupo sahihi sana na anacho kiwaza hakuna kitu kibaya kama kufanya shughuli usiyo ipenda ukiangalia sana jamaa ana future ya maisha hataki kuji-frame katika uwalimu tu....
Mjadala ktk coment yangu ni kudekezwa sio aina ya kazi anayoifanya. Kijana ulielelewa ktk malezi sahihi na mwenye hofu ya Mungu huwezi kamwe kusema wazazi wanarap hii ni dharau.
Hata tukija ktk kazi huwezi kusema haipendi ilihali ilipokuwa anasoma alijua kbs aina ya elimu anayoipata itaishi ktk kazi hiyo aliyoisomea.
Akupe sababu za kuichukia sasa baada ya kuifanya kwa miaka 6 labda itatisaidia.
 
Nimenunua beach plot bagamoyo -mlingotini naanza msingi wa beach resort/bungalow mpaka february niwe naezeka. msimu wa mvua ukija nipande miti kuzunguka shamba zima nije tena mjini kuzichanga.
**Kazi bila kuwa na cha pembeni utakuja kupatwa butwaa za wanasiasa
 
Wakuu heshima yenu. Katika kipindi cha miezi 9 mfululizo nimekua Dilemma kwa kile ninachokiita kushindwa KUACHA kazi. Nakua katika stress, hasa nikianza kuwasikia wazazi wakirap nikigusia suala hilo. Nimeajiriwa serikalini kama mwalimu. Sina shida yoyote kazini, ila nahisi kama muda wangu Wa kuitumikia serikali umetosha na ninatamani sasa kuishi maisha magumu yenye Uhuru ambapo naamini nitauona ubunifu wangu Wa fursa, sipendi kuwa average man, nataka kufikia malengo yangu mengine ambayo hayahusiani na taaluma.

Sikujua kama KUACHA kazi Nako ni kazi. Marafiki, waajiri, wazazi, ndugu, wamekua kikwazi kwa kunipa woga Wa hali ya juu, basi mim hata sina hofu, napenda kuishi hayo maisha wanayoyahofu. Huwa najisikia vibaya sana nikionywa kutoacha kazi, kazi yenyewe sasa nashindwa kuitekeleza vema kwa kuwa nimesha loose interest nayo, sitaki kufukuzwa nataka kuacha, Nimefanya kazi kwa miaka takribani 6, nahisi Nina call nyingine, huwa napenda sana Uhuru, ubunifu na kuthubutu.

Note:
Ukiwa mtumishi unakuwa secured kwa bima ya afya nk, hili ndilo wanalonitisha hasa, ukichanganya na wimbi la vijana mitaani walokosa ajira.

Nina familia, Je, inaweza kuwa kikwazo kwa mipango yangu?

Japo ninasoma sana vitabu, hasa motivational books, pia Business Books ila napima na mazingira halisi niliyopo,
Sio vitabu vinavyonichichea, ila call ndo inanichochea kusoma vitabu hivyo ili kugain more knowledge with confidence.

Nadhani GT watakuwa wananielewa zaidi ya nifikiriavyo.

Lengo langu sitaki kushika mawili. Na nimaamini katika kile nikipendacho kwa sasa.

Long story short, nisaidieni kimawazo.

Angalizi: We teachers and other servants are too coward with inferiority ya future challenge. Msinitishe nipeni strong thoughts.

Samahani kama kuna lugha Kali.
Maswali, ushauri,critics, mapendekezo ya maandiko, videos, quotes, welcome.
Asanteni.

TZ1

Piga chini....
 
Mjadala ktk coment yangu ni kudekezwa sio aina ya kazi anayoifanya. Kijana ulielelewa ktk malezi sahihi na mwenye hofu ya Mungu huwezi kamwe kusema wazazi wanarap hii ni dharau.
Hata tukija ktk kazi huwezi kusema haipendi ilihali ilipokuwa anasoma alijua kbs aina ya elimu anayoipata itaishi ktk kazi hiyo aliyoisomea.
Akupe sababu za kuichukia sasa baada ya kuifanya kwa miaka 6 labda itatisaidia.

Aisee..

Hii ni ultimate level ya kuogopesha....Kama ungekua ndio unatisha mtoto mdogo namna ungetakiwa ufungwe kwa child abuse!

How do you live kwa kuogopa namna hii?

Ogopa Mungu,ogopa wazazi,ogopa everybody....

Spend your life na nguvu zako kufanya kitu ambacho hukipendi,then die a miserable man all the way through!
 
Usijaribu yalionikuta najua mwenyewe nataman huu uzi ningeusoma kabla sjachukua maamuz
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom