Ngoromiko
JF-Expert Member
- Sep 15, 2011
- 554
- 175
Kwa majonzi makubwa tumemwaga kitaifa mpendwa wetu Bob Makani (rip). Ameagwa kitaifa kwa sababu amelitumikia taifa letu kwa uzalendo wa hali ya juu.
Nimesikitishwa sana kwa kitendo cha CHADEMA kutanguliza mbele maslahi ya kichama badala ya maslahi mapana ya kitaifa pale walipopamba jeneza la mpendwa wetu na bendera ya chama badala ya Bendera ya Taifa.
Kwa kitendo hicho, wamejenga taswira kuwa Bob ameagwa kichama zaidi na si kitaifa. Mmetuangusha Watz.