Kozi zenye tija toka VETA

Diwani

JF-Expert Member
Oct 25, 2014
2,672
2,697
Habarini za mihangaiko ndugu wana jamvi.

Langu ni swali tu, ningependa kujua kozi (takribani 3) zeye tija na uhitaji mkubwa katika soko la ajira yaani kuajiriwa ama kujiajiri kwa sasa kutoka VETA.

Ahsante.
Nawasilisha
 
Achana kabisa na ndoto za kusoma ili kuja kuajiriwa, hizo zama hapa Tanzania hazipo tena. Nina uhakika na hizi kozi tatu za Veta za ufundi ukisoma uwezekano wa kujiajiri upo kwa zaidi ya 90%.
1. Ushonaji (Tailoring).
2. Uwashi (Building/Civil).
3. Useremala (Carpentry)
 
Hvi wadau ukiachana na veta kuna chuo kongine kinatoa kozi za office attendant?
 
Mkuu nnapofanya kazi kuna chuo cha VTC, kipo chini ya veta, na kuna baadhi ya masomo nafundisha. Fani 3 ambazo sijaona wanaomaliza wahangaike ni umeme (EL), mechanics (MVM) na ujenzi (MB)
 
1.Umeme
2.Welding
3.Ufundi simu
4.Mechanic (ufundi magari) Hii sio deal kivile kama umeshafika umri wa 25+,Hii inatakiwa mtu aianzie akiwa na umri wa 18yrs mpk akifika 25 Kashakwiva haswaaaaa.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Achana kabisa na ndoto za kusoma ili kuja kuajiriwa, hizo zama hapa Tanzania hazipo tena. Nina uhakika na hizi kozi tatu za Veta za ufundi ukisoma uwezekano wa kujiajiri upo kwa zaidi ya 90%.
1. Ushonaji (Tailoring).
2. Uwashi (Building/Civil).
3. Useremala (Carpentry)

yani nisitegemee kuajiriwa halafu nisomee Uashi?

Nimekuelewa lakini
 
Chuo hiki kipo wapi na ada zake ziko vipi
Kinaitwa Mgulani Vocational Training College, kipo chini ya VETA. Mahali kilipo ni ndani ya Mgulani JKT. Ntakupigia picha fomu yao kujiunga kisha ntaiweka hapa jukwaani, ina maelekezo yote
 
Back
Top Bottom