Burhani Omari
Member
- Sep 27, 2022
- 8
- 10
Habari wanaJF!
Niwaombe radhi kwa kimya kirefu hapa JF tangu 2016, kwani nimiongoni mwa Wadau wakubwa wa jukwaaa hili. Awali nilikuwa natumia acc kwa jina Burhani Kassimu, ila kwasasa nina hii acc mpya.
Mnamo mwaka 2016, niliandika uzi hapa wa kuomba ushauri juu ya fani ya masoko na uhusiano yaani Marketing and Public Relations. Na nawashukuru wale wote waliotoa mawazo yao mseto yaan chanya na hasi lakini mwishowe niliamua moja, na chaguo langu liliangukia kwenye kwenye hii fani. Nilisoma toka 2016 mpaka 2019 nilipohitimu pale Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Mabibo.
●Uzuri na Ubaya wa kozi hii kwenye soko la ajira
Fani hii inauzuri na ubaya wake kama ilivyo kwenye kozi nyingine na ikumbukwe hii ni kozi ya biashara, hivyo inakuw na ushindani mkubwa kwenye soko la ajira. Kwanza ningependa kuangazia Uzuri wa kozi hii:
Mosi, uzuri wa kozi hii ni, imebeba fani mbili tofauti yaani Masoko na upande mwingine Mahusiano hivyo unaweza kuwa na chaguo (option) mwenyewe uende upande gani baada ya kumaliza masomo.
Pili, ni miongoni mwa kozi ambayo inaajira nyingi zinazotangazwa kwenye majukwaa ya ajira mfano mabumbe, ajira yako, ajira leo n.k, hivyo ni juhudi zako na umakini katika kuomba/kutafuta kazi.
Tatu, ni fani ambayo inatoa maarifa mengi sana hasa kwa wale ambao wamepanga baada ya kumaliza wajiajiri, kwani unajifunza biashara na masoko kwa ujumla.
Nne, ni kozi ambayo fani zake ni mara chache kukosa idara zake kwenye taasisi mbalimbali, hivyo inauwanda mpana kwenye soko la ajira.
Kwa mchache haya juu ya uzuri wa kozi hii, nihamie upande wa pili
kwa kuangazia changamoto/ubaya wa kozi hii:-
●Changamoto za Kozi hii kwenye soko la Ajira
Mosi, ni kozi ambayo inaushindani mkubwa kwani baadhi ya ofisi/mashirika/makampuni hususani ndogo/madogo na za/ya kati hazizingatiii sana mtu aliyesoma kozi hii kufiti kwenye nafasi, taasisi inaweza ikaopt mtu mwenye kozi nyingine inayoendana na hii na akafit kwenye nafasi mfano, Nafasi ya Marketing anaweza akafit pia mtu aliyesoma Business Administration kwani hata ukiangalia modules zao chuoni wanashare, sasa jiulize kuna vyuo vingapi vinatoa kozi za Marketing au Business Administration? Lakini pia ukiangalia kozi ya Public Relations nafasi yake anaweza akafit mtu wa Journalism au Mass Communications, je ni vyuo vingapi diploma au degree vinatoa kozi ya Journalism au Mass Communications?
Kwa leo ningependa kuishia, ila ningependa kukaribisha maswali au mjadala wowote ule. Ila angalizo ukibisha njooo na facts kwani ambaye utakayebishana nae (mimi) nimesoma hii course na nipo kazini kwasasa.
Ahsante,
Burhani Omari.