Udahili kozi za Kilimo na Ualimu (arts) zingesitishwa kwanza

JMF

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2013
Posts
1,782
Reaction score
2,843
Sijui kwa takwimu ni idadi gani ya wahitimu wa kozi tajwa hapo juu ambao wameingizwa kwenye soko la ajira toka vyuo vikuu kuanzia mwaka 2015. Idadi ya walimu wa sanaa 74 walioajiriwa kupitia tamisemi haihitaji kuwa na elimu ya takwimu kujua kuwa taaluma hiyo siyo kipaumbele tena kwa sasa.

Ni idadi ndogo sana ikilinganishwa na wanaohitimu kwa mwaka tena kwa chuo kimoja tuu. Miaka ya nyuma (enzi za Kikwete) kilimo na elimu ndo zilikua kipaumbele kiasi kwamba form six walichukuliwa na kupewa mafunzo ya muda mfupi kwenye vyuo vya ualimu na vya kilimo kisha kuajiriwa ili kukidhi mahitaji.

Swala hilo lilipelekea vijana wengi kujikita kusomea fani za kilimo na ualimu kabla ajira hazijafungwa alipoingia Magufuli. Ikumbukwe wakati huo hakuna aliyejua kinakuja kutokea nini mbeleni, hivyo maelfu ya vijana waliendelea kudahiliwa kwenye kozi hizo na kujipa matumaini mengi.

Kozi zilizoonekana haziajiriki kirahisi kama bcom, finance, tax, admn etc leo hii ndio wanaoajiriwa kwa mamia na maelfu TRA na kwingineko ukilinganisha na walimu 74 au maafisa kilimo ambao ajira zao hazikutolewa kabisa.

Kwa upande wa afya nako ni yaleyale, hakuna MD aliyewahi ku hustle mtaani kwakukosa ajira, ila leo hii ni kawaida kumkuta daktari analipwa laki3 na mhindi na matusi juu. Ataenda wapi? Ifike mahali sasa wanaoona mbele wawashauri wadogo zao(zetu) waliopo sekondari na vyuoni kusoma kwa malengo ya kujiajiri. Wasome trend ya ajira nchini na fani wanazoweza kujiajiri nazo kwa urahisi.

Elimu ya ufundi itiliwe mkazo na hamasa kwa vijana. Laasivyo, kitakachofuata ni vijana wengi kukimbilia kusoma udaktari wa meno, utabibu na ualimu wa sayansi kufuatia uhaba wa wataalam hao kwa mujibu wa tamisemi. Hiyo itapelekea lundo la wataalam hao miaka michache ijayo na kusababisha wapitie wanachokipitia waliosomea ualimu na kilimo.
 
Waache watu wasome mana mmekariri kuwa kusoma hizo kozi lazima mpate ajira serikalini..hichi ndicho kina waponza.

Badilisheni mtazamo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Sio kila anaesoma anataka ajira
 
Back
Top Bottom