Mimi hapa simwelewi kabisa kamanda Kova. Mtu anavunja sheria za nchi tena kosa la jinai - kuleta vurugu ndani ya nchi halafu anasema amemwonya mara kadhaa? Maana yake ni nini? Mbona wamachinga wanaohangaishwa mitaani huko hawaonywi mara kadhaa? Ponda ni nani hasa kwenye nchi hii? Kwanza imesemwa mara nyingi kwamba sio mtanzania, kwa nini hakuna chombo kinakanusha au kukubali jambo hili? Unajua kuendelea kunyamazia jambo hili kutainua watu wengine kwa upande wa pili wabaya kuliko ponda wenu siku moja msiyoijua. Kamanda Kova jua kwamba, mnakaa kwenye madaraka kwa muda mnaondoka wanakuja wengine nanyi mtarudi mtaani kuungana nasi. Huku mtaani tutatazamanaje? Ponda huyu mnayemlea leo kwa sababu zenuaidha za kidini au vinginevyo kwa kuwa mna ulinzi kila saa atakuja kuwadhuru kesho humu mtaani, kama si wewe ndugu zako au mali zako. Acheni kulea maradhi.