- Thread starter
- #61
Ni kweli kuna Diplomatic Immunity tena sio Ubalozini tu hata kwenye Meli au Ndege zenye Bendera ya taifa lingine.Kufanya hivyo ni kukiuka sheria za kimataifa hasa mkataba wa Vienna
Lakini pia balozi zinaweza kutumia mwanya huo kuvunja sheria kama Utawala Wa Nigeria ya enzi za Buhari ulivyotumia kinga diplomatic bags kumteka Umar Dikko na kumfungia kwenye sanduku kwa nia ya kumrudisha Nigeria kutoka Uingereza hadi Scotland Yard na majasusi wengine walipowashtukia majasusi wenzao wa MOSSAD kutoka Israel na Nigeria waliosuka mpango huo na kuamua potelea mbali wakafungua lile sanduku
By the way :Kova si aliwahi kujigamba kuwa yupo huku si ajitokeze ajibu sasa au anasoma kwa hasira na kuuma meno tu.Kamanda jitokeze basi .Hii ni nafasi ya Mwisho ya kudhihirisha uwepo wako kwenye kizazi hiki cha digitali.Maana uliongea sana
kova mwisho wake umefika,anatumia nguvu nyingi kudhibiti maandamano ya wadai haki huku mlango wa pili anashiriki kuhujumu raslimali za taifa