Kova 'anashiriki' kutorosha Twiga na Madini ya Taifa

otorokoko

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2012
Posts
2,437
Reaction score
157
Ndugu zangu,

Kuna maharamia wa ubalozi wa nchi fulani ambao sitautaja kwa sasa. Wana makazi yao Upanga.Watu hawa wanamiliki twiga na madini ndani ya makazi yao.

Ilipogundulika mwenyekiti wa mtaa aliwaita na kuwahoji lakini katika mazungumzo hayo walimuomba wampe milioni 100 ili asitoe habari polisi,mwenyekiti huyo alikataa akampigia simu kamanda Kova na kumpa taarifa.

Kamanda Kova alifika na baadhi ya waandishi wa habari na kupiga picha wale twiga na madini yaliyokuwepo pale.

Cha kushangasha mpaka leo siku zinaenda wiki zinakata naona kimya watuhumiwa hawachukuliwi hatua.

Vyombo vya habari viko kimya sijui kama wale waandishi waliokuwepo walipigwa mkwara au walipewa hela watulie.

Kamanda Kova naye yuko kimya labda naye kapewa asilimia fulani,mwenyekiti kwa sasa naye katulia kabisa labda naye Kova kamshawishi wamepiga pesa.

Nitoe rai kwa chama changu cha demokrasia na maendeleo walifuatilie suala hili kwa umakini ili waiumbue serikali ya CCM na kibaraka wao Kova.
 
Mawaziri kivuli wa maliasili na utalii na nishati na madini kazi kwenu kufuatilia mambo haya. Kwa pamoja tutashinda.
 
Mbona unamsema Kova wakati kumbe na wandishi wa habari nao wanahusika.
 
Kama imefikia hatua ya kufuga twiga mjini sasa hii ni zaidi ya hatari! Vyombo vyetu vya usalama kimya bize na siasa. Kuna saa unasikia habari mpaka masikio yanawasha.
 
wote wanahusika,watueleze ni kwanini mpaka sasa wako kimya sisi wananchi tuwaelewe vipi?wanaweza kutuaminisha vipi kwamba na wao hawajashiriki uhalamia huo
Mambo yapo katika uchunguzi mkali na intelijensia ina taratibu zake, Usitibue... funika kombe '' !!
 
Kama imefikia hatua ya kufuga twiga mjini sasa hii ni zaidi ya hatari! Vyombo vyetu vya usalama kimya bize na siasa. Kuna saa unasikia habari mpaka masikio yanawasha.
kwa hapa tulipofika serikali na jeshi la polisi wamekumbatia rushwa na hawawezi kuipinga na kuipigia kelele
 
Mpe lokesheni Mch. Msigwa au sugu ilipo nyumba walumowekwa twiga wetu.
 
Mambo yapo katika uchunguzi mkali na intelijensia ina taratibu zake, Usitibue... funika kombe '' !!

kwanini habari hiyo imefunikwa,hatujasikia ikitangazwa?mbona habari nyingine huwa zinatangazwa na wanatupa ahadi za kufanya uchunguzi hii ina nini mpaka wakae kimya?
 
kwanini habari hiyo imefunikwa,hatujasikia ikitangazwa?mbona habari nyingine huwa zinatangazwa na wanatupa ahadi za kufanya uchunguzi hii ina nini mpaka wakae kimya?
Mkuu Abd.Hsni wewe hujui kama hakuna fedha za kampeni ya Uchaguzi... wanakusanya chanduchandu....
 
Msigwa keshageuka kibaraka wa nyarandu sikuizi. PESA MWANAHARAMU
 
Mkuu Abd.Hsni wewe hujui kama hakuna fedha za kampeni ya Uchaguzi... wanakusanya chanduchandu....

raslimali za nchi zimegeuzwa shamba la bibi kila anayejisikia kuchukua anachukua,na serikali imekaa kimya,vyombo vya usalama vimekaa kimya
 
Mbona unamsema Kova wakati kumbe na wandishi wa habari nao wanahusika.
ndugu umejitoa ufahamu?? Wahandishi hawana dhamana kwa jamii inayowazunguka! Wana hiyari ya kuandika au kutokuandika! Wenye dhamana ni kina kova na team yake
 
Mwenyekiti angechukua hizo milioni 100 halafu akawaambie vijana wa bodaboda na machinga wakachukue mali zao
Kesi ya ngedere kapelekewa ....
 
Ukisikia wananchi wanachukua sheria mikononi ujue huchoshwa na vitu kama hivi. Inafika mahali inakosekana maana ya kutoa taarifa kwenye chombo hiki. Ni kama vile mwanchi mtoa taarifa amepeleka neema ya kuhongwa kwa Kova. Hakuna anayejali!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…