Wachimbaji wa madini mererani wachachamaa wapinga soko la madini kuamishwa kwenda Arusha tunasimama na kauli ya Rais Samia

nyamadoke75

Member
Apr 1, 2020
93
288
SAKATA la kutaka soko la Madini ya Tanzanite kufanyika sehemu zote nchini sasa limeingia katika sura mpya baada ya wachimbaji wa madini hayo kusema kuwa wanaongoza agenda hiyo hawana nia njema na Serikali na wachimbaji kwani wametanguliza maslahi yao binafsi.

Wachimbaji hao walisema na kusisitiza kuwa soko la Madini Tanzanite Mirerani limeongeza thamani ya madini hayo na kufanikiwa kuthibiti utoroshaji na wanaotaka soko hilo liondoke katika Mji huo hawana nia njema na serikali na wametanguliza maslahi binafsi hatua ambayo hawataikubali.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Mji wa Mirerani Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji wa Mdogo wa Mirerani,Adamu Kobelo alisema uamuzi wa serikali kujenga jengo la Tanzanite City kwa gharama ya shilingi Bilioni 5 haukufanywa kwa bahati mbaya bali ulizingatia maslahi ya nchi na sio binafsi.

Kobelo alisema agenda isiyo rasmi ya kutengua kanuni kutaka soko hilo lifanyike nchi kote na sio Mirerani pekee inawalaki na inapingana na maagizo ya viongozi wa juu akiwemo hayati Rais John Magufuli,Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa wote waliagiza kwa nyakati tofauti umuhimu wa soko la Tanzanite kuwepo Mirerani.

Kobelo alisema wanaofanya kampeni kupitia mikutano isiyokuwa rasmi ili soko la Tanzanite liondokea Mirerani hawana nia njema na serikali na kutaka madini hayo kuendelea kuuzwa kwa wingi kwa njia za panya na serikali kukosa mapato kitu ambacho wachimbaji hawatakubali.

Naye Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} Wilaya ya Simanjiro,Awadh Yusuph ambaye pia ni mchimbaji yeye alisema kuwa mwenye kutaka soko la Madini ya Tanzanite liondoke Mirerani kwa anawakosea wananchi wa mji huo na pili anawakosea viongozi wote wa juu wa serikali wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Yusuph alisema kwanza agenda hiyo inajadiliwa na watu wasiokuwa wakazi wa Mji wa Mirerani na sio wachimbaji wa Madini ya kutaka soko hilo liondolewe hawana nia njema na wakazi wa Mirerani na serikali kwani wanania ovu hivyo wanapaswa kupuuzwa na soko hilo kubaki katika Mji huo kama serikali ilivyoelekeza.

Wengine waliounga mkono soko la Tanzanite kubaki Mirerani ni pamoja na wachimbaji Jafari Matimbwa na Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mirerani ,Christopher Chengurwa wao walisemaTanzania ni nchi ya tatu Duniani kwa kuuza madini ya Tanzanite ikiongozwa na India na Kenya na ni aibu kwa nchi kwa mwenye migodi Tanzanite ambaye anazalisha hana faida na Madini hayo.

Walisema serikali ya awamu ya tano na sita zote ziliamua soko la Madini ya Tanzanite liwe Mirerani kwani walikuwa wana nia njema kwa wachimbaji na serikali lengo likiwa kudhibiti utoroshaji wa madini hayo sasa wanaibuka kutaka soko hilo liondoke wanapaswa kukemewa na kuacha mara kujadili hilo kwani halina manufaa kwa nchi.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara{MAREMA}, Justn Nyari alipotafutwa na kueleza juu ya mjadala huo yeye kwanza alisema hana taarifa rasmi juu ya hilo na hata akipata taarifa rasmi hataunga mkono hoja hiyo kwani inataka kuiyumbisha serikali ya Rais Samia.

Nyari alisema wanaoanzisha mjadala huo na kutaka kutengua kanuni ya kutaka Madini ya Tanzanite kuuzwa nje ya Mji huo wanapaswa kuangalia zaidi maslahi ya wananchi wa Mirerani na serikali kwa ujumla kwani kupelekwa soko Mirerani na kujengwa kwa ukuta kumeisadia sana serikali kuingiza mapato mara tatu hadi nne kuliko zamani.
20240726_140803.jpg
20240726_145022.jpg
20240726_134056.jpg
 
Back
Top Bottom