Kosa likikufunza sio kosa tena bali ni upya uliokuwa huujui

Feb 4, 2024
67
205
KOSA LIKIKUFUNZA SIO KOSA TENA BALI NI UPYA ULIOKUWA HUUJUI.

Sifa ya makosa ni kutoa adhabu na inaweza isiwe muda huo ulipolifanya kosa ila ni lazima litakuadhibu tu mbeleni hivyo hakuna namna unaweza kukwepa adhabu ya kosa lako.

Taarifa inayopendeza ni kuwa kosa likikupa adhabu nawe ukaona kama funzo basi hilo sio kosa tena bali ni upya ambao ulikuwa huujui hapo kabla na njia pekee ya wewe kuujua huo upya imekuwa ni kupitia kukosea.

Usifanye makosa makusudi hapo utakuwa sasa unatafuta adhabu za kujitakia na yawezekana adhabu hiyo isiwe funzo lolote kwako kwa sababu sio jipya bali ulilijua kabla.

Kwenye mchezo wa mpira timu inafungwa kupitia makosa hiivyo adhabu yake ni kufungwa magoli ila baadaye wachezaji wakimakinika kutafuta walifungwa vipi basi watagundua mbinu zipi wafanye ili wasifungwe tena na hapo itakuwa wamejifunza kupitia makosa na adhabu waliyo adhibiwa.

Japo makosa mengine adhabu yake ni kali na utaadhibiwa tu bila kujali hukuwa ukijua kuwa ni kosa hapo kabla ila ukimakinika zaidi utajifunza tu .Kosa bila adhabu ni ngumu kuwa funzo na kikawaida kosa lisilo na adhabu yawezekana lisiwepo labda tu uamue kutuiona hiyo adhabu.

Ukiona maisha yanakuadhibu Kwenye jambo fulani wewe kaa chini tulia utafute wapi ulikosea.

Mwanasayansi Saul kalivubha.
 
Back
Top Bottom